Msaada Kwenye Tuta-Kuvuta Umeme wa TANESCO na Gharama zake[power connection] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada Kwenye Tuta-Kuvuta Umeme wa TANESCO na Gharama zake[power connection]

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Shadow, May 8, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wanajf,

  Naomba kujua gharama za kuvuta umeme ndani ya Nyumba. Naomba mchanganuo wote yani Phases zote[zaidi three phase]. Na inachukua muda gani mpaka kupata huo umeme.

  Pili, ningelipenda kuweka underground 'harmor cable', je zinapatikana hapo bongo Darisalama?

  Nimejaribu website ya hawa jamaa [TANESCO] ni kama 'jumba la makumbusho'.

  Natanguliza Shukrani
   
 2. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Jiandae uwe na pesa zaidi ya milioni moja, na inategemea eneo gani nyumba yako ipo kama una nguzo ipo tayari jirani na nyumba itakuwa rahisi kwako.Vile vile pale Tanesco kuna watu wanataka kupewa ahsante kabla ya kazi (inabidi utoe pesa sasa sijui rushwa au asante) Ukifanya vitu hivi utakuwa na umeme ndani ya 2 weeks.
  Kama kuna mtu unamfahamu pale Tanesco pia inaweza kuchukua muda mfupi kufanikiwa kupata.
  Bila kufanya vitu hivyo unaweza kuchukua hata mwaka hujapata umeme.
  Mie sikufuuta 3 phase pale. Ningefuta hizo phase ningekutajia. Ila lile shirika la umeme lina usumbufu sana. Labda sasa watakuwa wamejirekebisha.
  Muhimu mtafute fundi umeme anayefahamika pale Tanesco huyo anaweza kukurahisishia kazi.
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Thanks Pretty.

  Asante sana kwa hizo heads up. Ubarikiwe!
   
  Last edited: May 8, 2009
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  U welcom.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nyie acheni kunitisha
  maana najiandaa kujenga porini hukooo.
  sijui nitavutaje umeme maana neno usumbufu kutoka tanesco lipo kwenye vipengele vya uanzishwaji wa shirika hilo
   
 6. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Gharama za umeme kwa single phase na nguzo moja ni Tshs 1,374,000/=,bila nguzo haizidi TZS1million. Kwa nguzo mbili andaa pesa inayofikia TZS 2.5million na kwa nguzo tatu ama nne inabidi uwe na budget ya pesa isiyopungua 3 to 3.5 million.

  Three phase hiyo ni balaa.kumbuka kuna VAT(ile 20% kodi ya nyongeza ya thamani) humo ndani ya hizo gharama kwa hivyo inapelekea gharama kuwa juu
   
 7. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nijulishe single phase ulivuta kwa bei gani...

  mimi nahitaji nguzo moja tuuu unifikiee...nijulishe mkuu
   
 8. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Andaa TZS 1,374,000/= mkuu wanakuunganishia ndani ya siku 60 (working days).
   
 9. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pretty anasema .......".Vile vile pale Tanesco kuna watu wanataka kupewa ahsante kabla ya kazi (inabidi utoe pesa sasa sijui rushwa au asante)....."
  Halafu watu wa Tenesco wako hapa hapa na wanasoma,maana nilikuta wana internet connection 24/7,ninachojiuliza haziwasumbui statement za aina hii?Ningekuwa mimi ningekwisha hama kampuni hii kama siwezi kuibadili.
  Kiboko yao nenda na recorder,wakikuomba hiyo pesa nenda na hiyo recorded voice kwa MD wao,utaupata in 7 days. Vishoka!vishoka!made in Tanesco-sisi ni ndugu zenu!
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Mkuu hiyo ni culture tayari na siyo kwamba wakuu wao hawajui.
  Mimi niliwahi kulipia umeme, pesa wakaila na risiti nilikuwa nayo.Tulisumbuana sana kwa karibia mwaka, hadi kupeleka ishu wizarani ikatoka amri umeme ukafungwa siku hiyohiyo! Nyie acheni tu!
   
 11. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Duh, Kumbe rushwa imeshafikia kuwa insitutionalized Bongo. Kaaazi kweli kweli.
   
 12. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu, nguzo tayari zipo nje ya nyumba. Kwa hiyo suala lipo kwenye kuconnect huo umeme.
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama nguzo ipo nje ya nyumba, ni just Tsh 460,000 hivi!
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hivi tulifikia wapi na bunge letu kibogoyo kuruhusu makampuni mbadala ya umeme??
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  yes, next level, hivo ndivo nijuavyo, single phase around laki tano yaani kasoro kidogo, na 3 phadse around 1mil.
   
 16. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Samahani wakulu wenzangu.mambo ni yale yale ya umeme,lakini tofauti ni kuwa mimi tayari nilishaunganishwa kitambo lakini natka umeme wa luku ili niondokane na adha.Nitalipia shs. ngapi ili nifungiwe hiyo luku badala ya meter hii ya sasa?
   
Loading...