Msaada kwenye tuta: How to Use Paypal to send money through a CRDB account?

Abdulhalim

Platinum Member
Jul 20, 2007
17,193
3,011
Wadau mwenye mawazo chanya anakaribishwa:

Scenario iko hivi:

I want to start a certain business with my partner. I am thinking of selling my goods/services online and charge via credit cards. How do i link between paypal and my CRDB account? is it possible? if yes, what are the charging mechanism? and what is the cost of doing so? roughly speaking.

Nanguliza shukrani.
 
Salaam Abdulhalim.
Kwa sasa ni ngumu kwa kuwa paypal wana link na Bank za USA tu labda za Ulaya, kwa hiyo kama una credit card itakuwa rahisi au la kama kuna mtu anafaham zaidi asaidie maana hata mimi a/c yangu ya paypal haina funds toka niifungue long tym na tatizo ni hilo la ku add funds.
Hivyo msaada plzzzz
 
Salaam Abdulhalim.
Kwa sasa ni ngumu kwa kuwa paypal wana link na Bank za USA tu labda za Ulaya, kwa hiyo kama una credit card itakuwa rahisi au la kama kuna mtu anafaham zaidi asaidie maana hata mimi a/c yangu ya paypal haina funds toka niifungue long tym na tatizo ni hilo la ku add funds.
Hivyo msaada plzzzz

Mkuu ni vyema umetoa ka-input. Shukran.

Kama jinsi ulivyosema ndivyo kwamba paypal wanalink na benki za US & Europe only, naona inabidi kukaa chini ku-strategize na ku-brainstrom upya.

Duh. kaazi kwelikweli.
 
Hellow!
Kufanya hivyo inakuwa ngumu as you our tz..Kama others walivyosema kuwa na credit card itakurahisishia mambo..
Ni hayo tu!
 
What is Pay pal......Wengine nao waelewe jamani !!

PayPal is an e-commerce business allowing payments and money transfers to be made through the Internet. PayPal serves as an electronic alternative to traditional paper methods such as checks and money orders.
A PayPal account can be funded with an electronic debit from a bank account or by a credit card. The recipient of a PayPal transfer can request a check from PayPal, establish their own PayPal deposit account or request a transfer to their bank account. PayPal is an example of a payment intermediary service that facilitates worldwide e-commerce.
PayPal performs payment processing for online vendors, auction sites, and other commercial users, for which it charges a fee. It sometimes also charges a transaction fee for receiving money (a percentage of the amount sent plus an additional fixed amount). The fees charged depend on the currency used, the payment option used, the country of the sender, the country of the recipient, the amount sent and the recipient's account type. In addition, eBay purchases made by credit card through PayPal may incur a "foreign transaction fee" if the seller is located in another country, as credit card issuers are automatically informed of the seller's country of origin.
 
What is Pay pal......Wengine nao waelewe jamani !!

PayPal is an e-commerce business allowing payments and money transfers to be made through the Internet. PayPal serves as an electronic alternative to traditional paper methods such as checks and money orders.
A PayPal account can be funded with an electronic debit from a bank account or by a credit card. The recipient of a PayPal transfer can request a check from PayPal, establish their own PayPal deposit account or request a transfer to their bank account. PayPal is an example of a payment intermediary service that facilitates worldwide e-commerce.
PayPal performs payment processing for online vendors, auction sites, and other commercial users, for which it charges a fee. It sometimes also charges a transaction fee for receiving money (a percentage of the amount sent plus an additional fixed amount). The fees charged depend on the currency used, the payment option used, the country of the sender, the country of the recipient, the amount sent and the recipient's account type. In addition, eBay purchases made by credit card through PayPal may incur a "foreign transaction fee" if the seller is located in another country, as credit card issuers are automatically informed of the seller's country of origin.

Ok, mkuu shukran kwa kuwaelewesha wengine. Pamoja!
 
Wadau mwenye mawazo chanya anakaribishwa:

Scenario iko hivi:

I want to start a certain business with my partner. I am thinking of selling my goods/services online and charge via credit cards. How do i link between paypal and my CRDB account? is it possible? if yes, what are the charging mechanism? and what is the cost of doing so? roughly speaking.

Nanguliza shukrani.

Mkuu,

Unataka kuanza business na partner wako hio nafikiri unasema kwa case ya nchini kwetu Tanzania.

Pili, unataka kuuza bidhaa na huduma online na uwatoze wateja si tu kwa credir card bali pia kwa kutumia debit card.

Sasa nnavyoona mimi ni kwamba unahitaji kuzungumza na CRDB na uwaelezee huo mpango wako na kwamba unataka kufanya hayo ulioeleza hapo awali.

Kwa njia hio utakuwa umepata mwanga kutoka kwa CRDB wenyewe.

Ukimaliza ndio unaweza kuelekea stage ingine ya business venture yako ya ku-set up IT infrastructure ofisini kwako.

Ni hayo tu.
 
Da sikushauri kabisa kutumia paypal tz unaweza ukalia security ya bank zetu iko low sana na pia huduma hiyo ya paypal bongo haipo.
 
Process ya online transaction iko "complex" sana na inachukua muda mfupi sana ingawa inaonekana kama ni mlolongo mreefu.

Mteja anatembelea website na anachagua bidhaa mbalimbali kutoka kwenye shopping cart ulioweka. Kwenye checkout, shopping cart yako ina-submits credit card transaction kwenda payment gateway kwa niaba ya mteja.

Payment gateway inapopokea transaction information, inapeleka data kwenye account yako ya biashara hadi kwa credit card processing bank ambao wanakuwa ni CRDB. (hapa namaanisha kwamba hii bank iwe connected na bank zingine ambazo kwa pamoja zinashirikiana kufanya processing, clearing, na settlement ya credit card transactions.) Sasa sina uhakika kama hali hii ipo kwa banks za Tanzania.

Ok tuendelee benki baada ya ku-process credit card itaangalia na kulinganisha na mtoaji wa kadi ya mteja, ambae ama ataidhinisha au kukataa transaction hio na hapo ndio mteja ataambiwa your card is been authorised au declined.

Ikikubalika taarifa itatumwa kurudi kwa processing bank, ambapo kuna pesa ya mwenye kadi na zitahamishiwa kwako wewe merchant katika akaunti yako Na hata ikikataliwa pia taarifa itatumwa kwa hio processing bank.

Matokeo ya ransaction yanatumwa kwenye payment gateway, ambayo kazi yake ni kutunza taarifa zote na kuzituma kwa mteja na mfanya biashara kwa confirmation and verification.

Na hapo ndio mteja anapata risiti. Na pesa pia kwenye transaction zinakuwa verified kwenye "batching" yako ofisini, na baadae zinaingia kwenye bank account yako.

NB:

Nini maana ya Payment Gateway

Ni application ambayo wewe mfanya biashara unaweka katika IT infrastructure yako ili kuruhusu transactions zilizo salama na unaweza kufananisha na point of sale katika supermarket yoyote ile. Hapo ndio penye kufanyika encriptions kuhusu taarifa kwenye kadi na kadhalika.

Nini maana ya Batching

Ni zile message zinazokuwa zikiingia na kuwa printed katika batching printer yako ofisini na wewe unakuwa ukiingia katika kiofisi chako na kuangalia kama transactions zimekuwa successful.
Tuendelee kuelimishana.
 
Last edited:
Sina uhakika kama Bank za Tanzania ziko intergrated na Paypal, mimi nimekuwa naitumia paypal kwa muda mrefu kwa ajili ya advertisers kwenye websites zangu ila nimeiunganisha na bank account yangu ya hapa US. Labda solution nyingine ujaribu ku-apply Paypal Debit Card ambayo unaweza kutoa pesa kupitia ATM za bongo, ila sijui kuna requirements gani za kupewa hiyo debit card yao. Angalia pia www.authorize.net uone kama wana Payment Gateway utakazoweza kutumia kwa ajili ya biashara yako.
 
Tembelea website ya paypal wameelezea vizuri jinsi ya kufanya ili uweze kulipwa kupitia Paypal na Credit cards zingine. It is doable.Mimi nina account CRDB na nime-link na PayPal hivyo naweza kufanya online shopping ingawaje sijajaribu. Vile vile, kuna companies nyingi tu ambazo zinatoa huduma hizo. Google na utapata info zote
 
Naona baadhi ya maelezo yanafanana na thread ifuatayo ambayo ilijadiliwa kwa kirefu sana Hebu isome.

CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao
Manitoba 19th January 2009, 12:05 PM

Kama una CRDB Visa Card, na ulikuwa unafikiria kuitumia kwenye internet, basi usithubutu kutia sahihi kuiwezesha kutumika mtandaoni (ila kama tu unajua unachokifanya).

CRDB wametoa card mpya zenye nembo ya visa, ambayo wanatangaza kwamba unaweza kununulia vitu mtandaoni. Inaonekana kama ni bonge la wazo mpaka pale utakapogundua jinsi gani zisivyo salama hata kiduchu.

Mtu yeyote mwenye namba ya kadi yako, pamoja na vile vinamba vitatu vya "usalama" vilivyo nyuma, anaweza kuitumia hiyo kadi yako kwenye mtandao bila tatizo lolote. Kwa hiyo ukiitumia kwenye tovuti ambayo si salama, basi ni kama umegawa namba yako kwa watu wengine kujihudumia.

Pia ukiisahau kadi yako mezani, na mtu/rafiki yako/mtoto wako mtukutu/mpenzi wako/secretary wako akapata mda wa kunakili pembeni hizo namba zako, basi pia inakuwa imekula kwako.

Kama ulikuwa unafikiria ile pin yako, basi sahau maana haina kazi kwenye mtandao.

Address Verification
Unaweza ukawa unajiuliza mbona kuna watumiaji wengi tu wa credit cards duniani na wasiwe na wasiwasi hivyo?

Moja ya njia ambayo huwa inatumika kupunguza wizi wa kutumia kadi za wengine ni kufanya uhakiki wa anuani. Kiasi kwamba mtu akiweka oda ya kitu basi oda yake itakubaliwa na kadi kutumika ikiwa tu anuani ya ambapo vitu vya kwenye oda hiyo vitatumwa ni sawa na anuani ya mwenye kadi.

Kwa CRDB hii feature wameifinya, kiasi kwamba mtu yeyote duniani anaweza kutumia kadi yako na kununua na kutuma vitu vyake sehemu yoyote duniani anavyotaka.

Paypal
Kutumia site kama www.paypal.com inaweza kusaidia kuondoa uwezekano wa mtu kukuibia namba za kadi yako online.

Kujiunga kadi yako na paypal sio tatizo, tatizo ni jinsi ya paypal kuihakiki kwamba kweli ni ya kwako.

Paypal wanachofanya ni kukuchaji fedha kidogo (wastani wa 2,000TZS), halafa katika muamala huo wanaweka namba ya siri fulani. Sasa wewe inabidi uangalie statement yako kutoka benki, uione hiyo namba, halafu uwape paypal. Assumption hapo ni kwamba hakuna mtu mwingine anaweza kuona statement yako zaidi ya wewe.

Sasa ndani ya paypal unaweza ukakamilisha taratibu. Ukija CRDB ili kupata tu details za hiyo transaction, jasho litakutoka. Inaweza ukadhani ni kitu simple tu kupata details za transaction (hata mimi nilifikiria hivyo), lakini amini usiamini utashangazwa ... Nimefanya si chini ya trip 10 kwenda CRDB kwa ishu hiii, usihesabu simu, na nimetoka kupiga nyingine sasa hivi ... lol ...

Ningetakiwa niwe nimeshakata tamaa ila tu nataka tu nifuatilie mpaka mwisho waniambie inawezekana au haiwezekani.

Ila kama huu ndio utaratibu, sioni ni jinsi gani wataweza kuwahudumia wateja hata 100 tu wanaotaka kujiunga na paypal. Achilia mbali kwamba hawa watu 100 inabidi wapige kwata CRDB more that 10 times, halafu wawe wanapiga simu mara kwa mara kuwakumbushia CRDB case zao. Na mara nyingi watu unaoongea nao CRDB hata hawaelewi unazungumzia nini.

Makubaliano yako na CRDB ni soo
Ili kuiruhusu kadi yako kutumika online, itabidi utie saini makubaliano yako na CRDB, ambayo yanavipengele ambavyo vinaiondolea CRDB jukumu lolote la kukuhakikishia usalama wako unpotumia kadi yako kwenye mtandao. Kwa hiyo ukiwa online na kadi yako, jua you are on your own.

Kwa watumiaji wengine duniani kuna taratibu za jinsi ya mtu kupinga kuchajiwa transaction ambazo hujazifanya wewe. Na kuna taratibu za jinsi gani utarudishiwa pesa zako.

Mpkataba wa CRDB hauoneshi kama kuna kitu kama hicho. Kwa hiyo mtu akipata details za kadi yako, siku zote itakuwa inakula upande wako.

Kwa hiyo baada ya kuutia saini tu nimehakikisha kadi yangu haiondoki machoni pangu, na pia nahakikisha akaunti hiyo ya CRDB haina vijisenti vingi ... mpaka ntakapomaliza hii exercise.

Hitimisho
Sasa hivi unaweza kutumia kadi yako ya CRDB kwenye mtandao, lakini you do it at your own risk, tena risk kubwa tu.

Kinachonitisha ni kwamba kama kadi yako imewezeshwa kutumika kwenye internet, mtu hana haja ya kukuibia kadi nzima kwa sababu utashtuka, utaripoti, na kadi itafungwa. Anachotakiwa kufanya ni kupata namba za kadi zilizopo mbele, na vile vijinamba vitatu vilivyopo nyuma ya kadi, na inakula upande wako kimya kimya.

Kama umeiwezesha kadi yako kutumika kwenye mtandao, na kama vijinsenti vyako kwenye akaunti yako sio vidogo, na kama huwezi kuitunza details za kadi kiasi hicho, ni vyema ungewaambia waizibe isitumike kwenye mtandao ... or u may have to learn the hard way.
 
Wazee mimi nina hitaji ku add funds tu kwa paypal a/c yangu lakini naona ugumu ni kulifanya hilo tu, lengo ni kuweza kufanya online shopping na baadaye labda kuuza pindi mipango yangu ikamilikapo, je crdb wanaweza saidia hilo?
 
I do have a working CRDB Card and have used it several times online without problem. I am not endorsing CRDB VISA as being safe, no at all.

Like the previous post mentioned, you need to exercise extra care when you use a credit card online. I recommend using PayPal or MoneyBookers as a safe option.

This protects you from exposing sensitive information to unscrupulous online merchants.

However, getting CRDB card to work with PayPal or MoneyBookers is not that easy. You need to follow the below procedures:

1. To work with MoneyBookers, your account should be a USD one, which is pretty easy to set up with CRDB. PayPal however works with both currencies.

2. You need to register for Internet Banking services, which costs you 30,000 Tsh one time fee. No monthly charges.

3. Once you are done with steps 1 & 2 above, PalPay works like a charm and you can enjoy buying things online with confidence.

If you need any other info, just PM me.

If this helps you, please say thanks!
 
GM7!

Hongera kwa kuwakumbusha wanajamii kuhusu payments online without card!! Huduma hii ni hatari haswa ukikutana na fraudsters kwani hata wenyewe CRDB wamehamishia liability kwa mteja kwa hiyo kama wenyewe hawatoi guarantee kuweni waangalifu.

Mimi niliwahi kuchotwa USD kwenye credit card yangu kwa ujinga wangu tu ! Nilimruhusu jamaa atoe Usd 50 Lakini alichukua zaidi ya mara tano for almost five months na siku nimeomba statement nilishangaa kuona hizo un authorised withdrawals na nikakimbilia crdb kUWAOMBA wakasitisha hiyo huduma.

Kama account yako haina pesa nyingi always then jiunge vinginevyo utaimbia ****** au kwa lugha ya siku hizi utafaulia na Bank haina dhamana . It's all at your own risk!
 
Back
Top Bottom