Msaada kwenye kesi ya dhuluma kazini

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
929
1,276
Wakuu habari za muda huu,

Hapo nyuma niliomba msaada wa kisheria hapa kwenu, nashukuru nilifanikiwa kwa michango yenu, tuliajiriwa kwenye taasisi moja. Wakati tunaanza ajira hatukupewa mkataba tukaambiwa wanaiandaa kwa maana hiyo taasisi ni mpya.

Tukafanya kazi miezi minne mshahara katulipa mwezi mmoja tu,tulipodai chetu akajibu majibu ya kukatisha tamaa.Kwaiyo tukaamua kudai haki yetu ya miezi mitatu, tukatafuta haki yetu taasisi mbalimbali lakini ikawa ngumu maana akiulizwa alikuwa anatukana.

Tukaenda kwa mkuu wa wilaya akaitwa na akakubali anatufahamu na pia tunamdai.Tukakubaliana kwa maandishi akaweka saini yake,akaahaidi atalipa baada ya mwezi mmoja . Muda umefika naona anaanza dadana tena .

Wataalamu wa sheria nisaidieni kwamaana ushahidi pekee nilionao ni maandishi aliyokiri mwenyewe mbele ya katibu tawala wa wilaya na mwanasheria wa halimashauri wakiwa wamemwakilisha mkuu wa wilaya pia hao wote kwenye makubaliano wameweka saini zao.

Je swali langu kwenu ushahidi huu unatosha Mimi kupata haki yangu nikienda mahakamani au kuna mbinu nyingine mnaweza kunisaidia?

Karibuni
 
Nenda CMA na documents zote ulizdn nazo, utapata msaada na taratibu. FULL STOP
 
Kama ulivyoshauriwa na mdau hapo juu. Nenda katika Tume ya Usuluhishi na Maamuzi(CMA), wao ndio wanamamlaka kisheria kusikiliza na kutoa maamuzi ya migogoro ya kazi.

Kwa Mkuu wa Wilaya ni vizuri, kwani ni short cut, lakini hawezi kutoa maamuzi (orders) pale ambapo ahadi aliyoitoa hajaitekeleza.

Mwisho wa siku atakushauri pia urudi CMA!
 
Back
Top Bottom