Msaada kwa wataalamu wa sheria na wataalamu wa utumishi

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Rafiki yangu ni mtumishi wa serikalini. Mwaka 2000 aliajiriwa kama Assistant Medical Officer, na baada ya muda alijiendeleza hadi kupata Degree ya Medicine pale Muhimbili University.

Katika kipindi chote akiwa Assistant medical Officer amekuwa akilipwa mshahara kama kawaida, na Baada ya kupata Udaktari badala ya kubadilishiwa scale ya mshahara (sijui makosa gani yalifanyika) akaanza kupata mshahara mwingine kama mtumishi mpya. Inshort, akawa anapata mishahara miwili (mshahara wa Assistant Medical Officer na pia mshahara wa Medical Officer).

Juzi kati baada ya agizo la Mhe Rais kuhusu watumishi hewa, ishu yake ikabainika na akatakiwa kurudisha mshahara wote aliokuwa akipata isivyo halali (mshahara wote wa Assistant Medical Officer) aliokuwa akiupata kinyume cha taratibu. Thanks God, amefankiwa kurudisha mpaka senti ya mwisho

SWALI/HOFU YETU:-
Baada ya kurejesha pesa hizo alizokuwa akichukua illegally, je vyombo vya dola Polisi na PCCB wanaweza kuendesha upelelezi wa jinai dhidi yake?? Na kama wataendesha jinai, watajikita katika vifungu vipi, na vya sharia ipi?

Maana tumeangalia Penal Code tunaona kuwa huyu Bwana angekuwa matatizoni iwapo asingerudisha pesa zote alizokuwa akichukua, labda kosa la kuisababishia hasara serikali lingembana. Na labda tukasema labda jinai ya wizi, ambayo nayo tunaona kama ingridients za wizi zinamkwepa.

Wajuvi wa Sheria na mambo ya utumishi karibuni
 
Kama amelipwa hatachukuliwa hatua zozote. Ila jamaa amekula bata sana aisee kumbe alikuwa akila mishaara miwili, asante sana magufuli kwa hili swala
 
Kama amelipwa hatachukuliwa hatua zozote. Ila jamaa amekula bata sana aisee kumbe alikuwa akila mishaara miwili, asante sana magufuli kwa hili swala
Je, kuficha taarifa si kosa kisheria?

Yaani ulikuwa unajua kuwa mishahara miwili inaingia, then unakaa kimya na kuendelea kuitumbua bila kumjulisha mwajiri wako
 
Anatakiwa ashitakiwe kwa makosa mawili! moja wizi wa pesa ya umma,, kwa nini aliendelea kupokea mishahara miwili kimya kimya bila kumjulisha mwajiri wake? kosa la pili ni ukosefu wa uaminifu katika utumishi wa umma! kuiba na kurudisha hakufuti kosa la wizi! hata kujaribu tuu kuiba bila mafanikio ukibainika ni kosa la jinai
 
Hapo Imetumika Busara Tu Lakn Ilitakiwa Afutwa Kazi Maana Alidhamiria Kufanya Kosa.

Wapo Watumishi Kama Huyo Walikuwa Wanakula Mishahara Mingi Na Walifutwa Sema Tu Wakat Mwingine Busara Inatumika Kama Hivyo Ilivyofanyika Kwmb Alipe Pesa Zote Kisha Yameisha Lakn Hata Kulipa Huko Hakuondoi Kosa Alilofanya.
 
Je, kuficha taarifa si kosa kisheria?

Yaani ulikuwa unajua kuwa mishahara miwili inaingia, then unakaa kimya na kuendelea kuitumbua bila kumjulisha mwajiri wako
Mkuu, labda suala lipelekwe mahakamani lakini kwa sheria za kazi hakuna kitu cha namna hiyo. Sana sana labda anaweza kupewa last written warning. Kwenye code of conduct hakuna kitu kama hicho ulicho uliza
 
Back
Top Bottom