Msaada kwa wale wataalamu wa solar power

Mr Suprize

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
823
845
Habari wadau!
Natumia solar ya mjerumani walt 50 kwa zaidi ya mwaka, solar battery ya maji.
Cha kushangaza solar hii sipati umeme usiku, nikitaka kuchaji simu yangu na za watoto wangu inabidi nichaji mchana pindi jua linapowaka sababu usiku hakuna umeme.

Naomba msaada wenu, Je, Ni kweli solar walt 50 haiwezi kuchaji simu walao 5 tu na kupata umeme KIPINDI CHA usiku walao kuwasha taa/bulb 3 tu?

Na kama inawezekana wapi mimi nimekosea?
 
Chunguza size ya hiyo Battery. alafu ipime kama bado ni nzima. Kwa maelezo yako battery haichaji Kwa hiyo mchana unatumia umeme direct kutoka kwenye PV solar. Sasa kama battery haichaji huenda imekufa na kama ni nzima Basi huenda solar control charger ni mbovu
 
Mkuu hapo yawezekana umeshaovercharge battery lako ndio maana linashindwa kusave moto
 
Chunguza size ya hiyo Battery. alafu ipime kama bado ni nzima. Kwa maelezo yako battery haichaji Kwa hiyo mchana unatumia umeme direct kutoka kwenye PV solar. Sasa kama battery haichaji huenda imekufa na kama ni nzima Basi huenda solar control charger ni mbovu

Ni kweli yawezekana battery imekufa,,coz mwanzon nainunua ilikuwa inatoa umeme ucku mzima,,but saiz ni mchana tu hasa linapowaka jua
 
VP Naweza tumia battery ya pikipiki ya unga kwa size ya solar yangu?
 
Kama umefunga system yako ki-standard, yaani Kutoka kwenye panel kwenda kwenye charge controller, halafu charge controller to battery na charge controller kwenda kwa matumizi ya taa, itakuwa rahisi kujua shida iko wapi.Mchana taa ya kuonyesha panel inafanya kazi (kawaida ni green na iko kushoto) itakuwa inawaka kuonyesha kuwa panel inaleta umeme kawaida. Taa ya kati huonyesha nguvu ya betri. Kama betri iko sawa, itakuwa njano kidogo na ikijaa itakuwa blue, na taa ya tatu ni ya umeme kwenda kwennye matumizi, Hii ikizimika ujue hakuna umeme unaoenda.
Kwa maelezo yako inaonekana betri imekufa, Ukitaka kuhakikisha hilo, jua likwaka hata muda mfupi uaona betri imejaa, lakini jua likipotea tu betri inakuwa down. Ungekuwa mtaalam ningekueleza kuwa betri ikijaa, disconnect panel halafu washa taa utaona zinazimika haraka.
Betri za kujaza maji huwa zikienda chini ya volt 10.6 mara kwa mara, huwa zinakufa hata ukijaza maji upya ni bure. Nakushauri ununue betri isiyotiwa maji (VRLA NON SPILABLE - DEEP CYCLE). Kwa panel uliyonayo ya 50W na matumizi yalivyo, betri yako isizidi 80AH

Usipoelewa niulize, na hata ukishanunua hiyo betri usiifunge kama wewe si mtaalamu, waweza kuunguza charge controller au hata nyumba yako
 
Mkuu sola ya wat 50 inawasha tv?na taangapi?
 
Hello Mr Suprize!
Katika masuala ya solar ni sharti kuwa na nidhamu hasa katika matumizi. Bila shaka kwa mwaka mzima hukupata shida na sasa ghafula shida imeanza. Inaonekana ungependa kupata umeme usiku lakini haiwezekani. Ingawa hujaeleza system yako ilivyo, maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia kupata tena umeme wakati wa usiku. Golden rule kwa solar ni hii: Mchana utatumia nguvu za jua na usiku utatumia AKIBA iliyowekezwa mchana kutwa kwa nguvu za jua katika battery yako! Now the questions:
1. Je panel yako inavuna jua la kutosha kujaza battery yako?
2. Je, afya ya battery yako (servicing) imefanyika kwa ufasaha? -- ni battery ya maji kwahiyo inahitaji service kama cleaning the terminals, checking water level etc
3. Je, battery yako ni A.H ngapi? pengine umetumia wrong battery kwa mwaka mzima na sasa imekufa (haiwezi kutunza/kufanya power banking) ili upate umeme usiku wakati ambapo panel haivuni chochote toka jua.
 
Mkuu sorry yan sielew maana ya ac na dc,,npe maana yake hafu nilete feedback

kwa uelewa wangu umeme WA dc ni umeme kama dry cell yaani WA kwenye betri za redio au torch ambao una positive charge na negative charge lakini umeme WA ac ni umeme kama WA tanesco
 
connection ya umeme ipo hiv..
umeme unatoka kwenye panel unakuja kwenye battery hafu unakuja kwenye invetor then kwenye taa..

Panel=>battery=>invetor=>Bulb

sasa (cjui ni ushamba) nashangaa hyo charger controll ipo au haipo?
 
To Kironde

1)Jua lipo la kutosha kabixa
2)Nmewah badilisha maj mara moja na cleaning za terminalz nafanya mara kwa mara
3)NAdhan ni A.H 50 but cna uhakika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom