Msaada: Kwa wakazi, wenyeji na wanaoijua Mbeya

Saint Murano

Member
Mar 31, 2019
97
264
Habari ndugu zangu.

Mimi niko Mbeya, ni mgeni nimefika kwa mara ya kwanza kwa nia ya kutafuta maisha, Sasa basi hapani nilipo nina laki tano 500,000 kama mtaji.

Msaada ninaohitaji toka kwenu ndugu zangu mnisaidie wazo la biashara au biashara inayoweza kunilipa kwa huo mtaji hapa jijini Mbeya.

Asanteni sana naomba msaada wenu ndugu wa kimawazo.
 
Broo Am sorry.
Why Mbeya?? Umetokea wapi kwenda mbeya?
Mm nadhani tekeleza kilichokupeleka huko. Maana sitaki kuamini umejikuta tuu uko mbeya najua una mipango iliyokupeleka huko
 
Upo mbeya sehemu gani,
Kuna maeneo yanahitaji ufungue banda la chipa kama upo jirani na vyuo,ufanye umachinga kwa kutembeza viatu na nguo hasa za kike,
Nunua viatu vya kiume vizuri nenda navyo tunduma katembeze,au vya kike nenda navyo kwenye minada msimu huu vinauzika sana viatu vya shule hasa wanafunzi kwenye minanda,yeboyebo usisahau kule vijijini.
Ukiweza nunua flash na memory card weka nyimbo za bongoflava nenda nazo kwenye minada utauza.
 
Hili ni moja ya wazo sahihi kabisa

Ila anatakiwa aseme mbeya sehemu gani yupo

Asije akawa yuko chunya akasema mbeya
 
Kama mbeya Mjini Nenda kyela saizi ni msimu wa dagaa nyasa.,kanunue dagaa wakavu faida utapata ila kabla ya Kwenda tafuta soko japo soko kubwa ni chunya, Zambia and na sumbawanga.
 
Laki 5,ndio ya kula na kulala?Coz hutegemei kupata faida mara tu unapoanza hizo business,nenda Minadani kwanza ujirithishe kama kuna biashara
 
Back
Top Bottom