Msaada: Kwa wakazi wa Arusha kuna yeyote ana ramani ya barabara mpya inayojengwa?

GIUSEPPE

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
5,281
2,000
Nimeona kuna ujenzi wa barabara mpya unao jengwa kusini mwa jiji la arusha, nimesikia kuwa bara bara hiyo inatokea ngara mtoni kwenda mapaka usa river kupitia kusini mwa jiji. Wakati natoka ISM kuchukua mtoto nikaona ujenzi huo ukiendelea upande wa viwanja vya magereza kando ya uwanja wa ndege arusha, karibu na eneo pafanyikapo maonyesho ya karibu fair.
Kwa wenyeji wa jiji kuna mwenye area map kuonyesha kwenye hiyo barabara inapita?
 

earl

Senior Member
Aug 30, 2012
118
250
Nenda Halmashauri ya Jiji kwenye kitengo cha Survey wanaweza kukupa taarifa zaidi. Mchoro wa hiyo barabara (barabara ya Afrika Mashariki) upo. Itaanzia Maji ya Chai, iteremke ipitie maeneo ya Nelson Mandela University, ije itokee maeneo ya Njiro Kwa Msola, ivuke ipite maeneo ya Sinon, Olasiti, ipandishe hapo maeneo ya Magereza, inavuka na kupita maeneo ya Ngaramtoni ya chini na kutokea maeneo ya Kibaoni - Ngaramtoni.
 

kipuyo

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
1,604
2,000
Mwenye kujua kinachoendelea amwage data,
Arusha kuna uhaba wa barabara zenye maana.
Barabara ya maana kwa sasa ni ile ya Nairobi na ile ya Moshi na umaana wenyewe umesababishwa na Fedha za mfuko wa Afrika ya Mashariki(sijui wamepata wapi hela) ila najua unajengwa na EAC kuunganisha TZ na Kenya.
Kuna kile kipande kidogo cha barabara ya Afrika ya Mashariki kutoka Sanawari mataa mpaka Lilipo jengo la AICC.
Zingine zote ni sifuri.
Ningependekeza ile barabara ya kuelekea Babati na Mikoa ya Kanda ya kati ifanywe double road hadi angalau jiji linapoanzia meneo ya kisongo.
Ile ya Kwenda kwa Morombo nayo ifanywe double road na ile inayoitwa old Moshi road inayoelekea Moshono nayo ifanywe hivyo hivvyo.
Lazima jiji liwe tofauti na miji midogo.
Tuwe na long run middle plan ya barabara hizo.
Plan ya stand ya mabasi ya kisasa iwepo,Singida wamewazidi.
Chadema onyesheni tofati na sio maneno tu.
 

longi mapexa

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
2,790
2,000
hiyo ni arusha by pass road kuondoa magari ya mizigo town inafadhiliwa na benki ya afrika mashariki....kwa maelezo zaidi ingia wikipedia mkuu nadhani nimewasaidia...............#Arusha_republic
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom