Msaada: Kwa namna gani naweza kujiunga na JWTZ

Manfighter

Member
Jun 22, 2017
88
43
Ndugu nilihitaji munisadie kuhusu taratibu za kujiunga na jeshi la JWTZ huku naona nimekosa wajuzi wa kunifafanulia.. kwa aliye maliza form six na kufaulu ni zipi taratibu na anaanzaje hadi kufika alipo hitaji... kwa maelezo tu.. hata kidogo naombeni msaada kwa hilo
 
Sasa hivi wanatakiwa kutokea JKT, kuanzia 2013 iliamriwa kua ukimaliza kidato cha sita upitie JKT, ila kama umefaulu kuendelea na chuo unaweza kuahirisha.

Kwa baadhi ya watu walipofika JKT walipanga kubaki huko kungoja ajira (sina hakika kama inawezekana huu mpango)

Wewe kwakua umemaliza kidato cha sita, ulitakiwa uwe umejumuishwa kwenda kama hujajumuishwa nenda kambi iliyo karibu na wewe waambie umemaliza kidato cha sita na haujajumuishwa kwenda JKT
 
Wakuu wa JWTZ na JKT wamesema wazi hakuna kutafutia kazi ya jeshi kwenye media .

Kazi hizo nenda ofisi za mkoa au wilaya au kambi yoyote ya jeshi iliyo karibu nawe utapata utaratibu wote wa kujiunga.

Angalizo, atakayetoa maelekezo katika media basi mkono wa serikali utamfikia alipo
 
Back
Top Bottom