Msaada kwa mwenye uelewa kuhusu jambo anisaidie

Bulaya001

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
5,868
6,480
Salute all comrades

Usiku wa kuamkia leo ktk hali isiyokuwa ya kawaida nilikuwa naugulia maumivu ya kikohozi kikavu(ninacho takribani siku ya nne kufikia leo) tena jana kilikuwa ni kikohozi kweli kweli, kiliambatana na Mafua yaliyovuja mithiri ya chemchem ya mto Nile (joke). sasa basi kikohozi hiki kipo kama jinamizi fulani yaani mida ya mchana ni cha kawaida ila usiku sasa ile naingia TU maghetto yaani kinasumbua kinyama, kiukweli nishazoea hii hali.

Basi usiku huo wa kama saa8 hivi jamaa chumba cha jirani kanigongea mlango akitaka nifungie(alijua nipo macho kutokana na kusikia nikikohoa) basi kagonga pale kama mara tatu hivi ya nne nikawa nimefungua baada ya kujielezea yeye ni jirani yangu, akawa kaniambia kuwa kaona mwizi wakati anaenda toilet baada ya kumpiga touch, mwizi yule alitoka mbio na kuacha mali zote zikiwa chini kwa hiyo kaniita tukushuhudie, basi bwana nikawa nimemuelewa tukaongozana kwa kuwa haikiwa mbali ni nyuma tu ya nyumba yetu tukawa tumeviona, kama sikosei zilikuwa ni mfuko mitatu wa kwanza ulikuwa na sabuni hizi nyeupe za kufuria (B29), mfuko wa pili ulikuwa na soda mchanganyiko na energy, na mfuko wa tatu ulikuwa na mafuta ya mwilini pamoja na ya nywele.

Baada ya majadiliano ya dk kadhaa tukawa tumekubaliana vitu vile tuviweke ndani ya nyumba ya mshikaji pakipambazuka basi kwa yeyote atakaye tuambia ni mali zake, ama tukasikia kuna wizi mahala basi tumpatie mhusika. Tukawa tumevichukua hadi ghettoni kwa mshikaji na kuviweka, me nikazama kwangu, niliendelea kukohoa mpaka alfajiri ndipo usingizi ulinichukua nimekuja kustuka ulikuwa ni kama saa5 hivi, nikawahi kwenda kufungua duka langu kisha nikarudi tena kwangu(maana si mbali na job) nimetulia kama dk kadhaa mwenye nyumba akanigongea nikamsalimia then nikasubiri aniambie sababu ya wito wake (ikumbuke wakati wote huo sina habari kabisa na ule wizi wa usiku) basi akawa kaniambia jirani yetu kaibiwa kwa hiyo tujitahidi kuwasha taa zetu za nje wakati wa usiku, nami nikamdakia kuwa jirani yangu kamuona mwizi usiku, basi nikawa nimemweleza kama ilivyo na jinsi tulivyo tunza mali ile ya wizi, basi bwana mwenye nyumba ikabidi amtaarifu balozi naye akamwambia mwenye mali wakawa wamemfuata jamaa aliyekuwa na mzigo ule, bila shida mwenye nyumba akawakabidhi mali yao nikajua yameisha.

kitu kilichonifanya nilete Uzi huu ni kuwa jioni nimeenda maghetto ghafla balozi akaniuliza wee ndie kijana wa mchana kwenye lile suala la wizi?? nikajibu ndio basi akaniambia kesho asubuhi ya saa mbili kuna kikao wewe pamoja na huyu mwenzako mnatakiwa muwepo..ktk pitapita zangu na kunasa za kunyapia inasemekana eti sie tunataka kuhusishwa na msala huu maana kuna baadhi ya vitu vimepelea.

Msaada wako kwangu ni mmoja TU je, nitaukwepa vp huu msala hiyo kesho asubuhi endapo mazingira yatatuweka hatiani, japo me nina jambo moja la kunilinda kuwa sikutoa taarifa mapema kwa sababu nimeamka mda ukiwa umeenda sababu ya haya maradhi yanayoniandama, je ikitokea hoja hiyo wameikataa nitaunda hoja gani nyingine ambayo nitaonekana sina hatia, maana kwa jinsi navyowajua wabongo na hali hii ngumu mtaani ya ugumu wa maisha lazima kuna fungu kubwa litatajwa ili waokoe hasara yao pia wajipatie pesa ya kitonga.

Ndugu yangu mwana JF ushauri wako ni muhimu kwangu kwenye kikao hicho cha kesho

Msichukulie poa maana sio wote walio jela wako kule kwa makosa halali, wengine huenda kizembe kwa makesi ya ajabu ajabu kama haya!
 
Hapo aliyeibiwa hana akili wala ustaarabu.
Suala la vitu kupungua hilo mnalichomoa hilo la pili utalisolve kama ulikuwa abnormal ukasahau kutoa taarifa mapema.
Hata mahakamani mfikishane aache njaa.
 
Hapo aliyeibiwa hana akili wala ustaarabu.
Suala la vitu kupungua hilo mnalichomoa hilo la pili utalisolve kama ulikuwa abnormal ukasahau kutoa taarifa mapema.
Hata mahakamani mfikishane aache njaa.
sio kwamba kufikishana mpaka huko kote ni kama kupotezeana mda wa kutafuta pesa mkuu???
 
Aliyeibiwa analiwa kiboga aisee, si angewashukuruni hata kwa hivyo vichache alivyovipata?
yeye hapo kaunga dots za kiboya eti huenda na sie tumeshilikiana na wale jamaa, why hatukutoa taarifa mapema/usiku ule ule kwa mwenye nyumba...
 
Back
Top Bottom