Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,200
4,984
Wakuu,

Kutokana na wadau kadhaa kuja na mijadala anuai inayoonyesha kuwa wanayo mitaji yenye kuanzia kiasi cha TZS 100,000/= hadi TZS 999,999/=, tumeona ni vema tukawa na mjadala mmoja endelevu ambao utatoa mawazo mbalimbali ya jinsi ya kutoka kimaisha ukiwa na mtaji huo.

Aidha, tunashauri usome maoni mbalimbali ya wadau kuweza kupata kujua wengine wametokaje kwa viwango hivi na unaweza kufikiria namna unayoona inafaa kwako. Tumejitahidi kupangilia posts humu kukurahisishia usomaji kwa ufanisi wako.

Asante

1592464042370.png
1592464251351.png


Biashara za kuanzia 100,000 - 200,000

Mkuu njoo nikuelekeze biashara za nguo za ndani za wadada, chupi dazani(12) elfu 30000 unauza 40000, nyingine 36000 unauza 45000 mpk 50000, unaweza kuzifanyia reparking tukafanya sita pia. zipo boksa pia 3 elfu 12000 unauza 15000. Vest na nyingine mzigo kutoka Malaysia na Turkey.
-----
Kua muwazi ni jambo Jema dogo, ila sasa yakupasa kueka wazi details like uko wapi,mjini au kijijini? Unapoishi ni kwako au umepanga? Hii itatusaidia kukushaur ww.

Kwa mfano uko kijijini na unaishi kwenu na Kuna eneo ambalo unaeza fuga kuku wa kienyeji huku unafanya shughuli nyingine kupata pesa ya kuwalishia kuku.

Kama uko mjini let's say Dar, unaeza tafuta kakijiwe ukaanza kukaanga chips kwa Huo mtaji Mdogo ulionao, unaeka chips na unadamka asbh unaanza kukaanga mihogo kwa ajili ya breakfast, saa nne tunaanza menya viazi kiasi kwamba saa tano chips tayar.

Kua msafi na wajali Wateja, naamini hadi umejiunga Jf Basi hata kama hujasoma sana lkn una uelewa mkubwa. Tumia akili yako kua mbunifu.

Katika kufanya yote usimwangalie mtu au kuwaza fulani atakuonaje, cha msingi zingatia unataka Kufika wapi.

Kukutia moyo tu, mm nlishauza chips nkiwa na degree moja lengo likiwa kupata mtaji wa kufungua kampuni ya ujenzi, nliuza for only one year huku nikilima na kufuga broilers ambao pia Nlikua nkiwakaanga hadi Miguu na vichwa vyao (vigondi) na kukamua utumbo wa kuku bila aibu, nliwauza masista duh na braza men kibao bila kujali tena kwa kuwaheshimu.

Boda Boda na dereva bajaji walikua wakiniagiza na kuntumikisha Lakini nliwaheshimu kwasababu ni Wateja, ktk kufanya hiyo kazi sikuwahi kuiwazia degree yangu hata chembe zaid ya kuwazia nataka Kufika wapi.

Baada ya mwaka mmoja nlianza usajili wa kampuni na baadae Mungu akanjalia nkavuna alizeti gunia 156 nkauza kila gunia elfu 54.
Nlitamani niendlee na chips Lakini nkaona hapana ngoja nkaitendee Haki ile degree. Ila kulima sijaacha had wa leo. Namshukuru Mungu ya Jana Si ya Leo.

Nimekupa kidogo tu ili usife moyo na uamini kila kitu kinaezekana
----
Kwanza Weka Aibu Pembeni Maana Itakurudisha Nyuma. Angalia kama Upo Jirani na Shule, Vyuo au Njia Ambazo watu huwa wanapita au kukusanyika kwa Wingi. Fanya Mpango uwe Freelancer wa Mitandao yote ya cm, uwe una kazi ya kusajili line, kutengeneza special number, ku renew line, kuuza vocha n.k.

fight upate mwamvuli mf wa voda, chonga meza ya mbao ya kishkaji na kiti cha mbao, au kama vipo home vifanye viwe vya ofisi .

Ongea na Muuza magazeti jirani na wewe, akufanyie mpango nawe uwe wakala, tengeneza stand ya wavu ya chuma ambayo kwa ubavuni na juu kidogo utaweza kutenga eneo la kuweka pipi, biskuits, karanga, hankerchiefs, pen n.k

Tafuta Deli, tengeneza Maji na Juice za kupima, weka na barafu uwe unafaya biashara zako eidha jiran na maeneo ya njia panda, karibu na shule/vyuo, jirani na maeneo ya sokoni au kwenye mikusanyiko ya watu. Pia waweza omba nafasi mbele ya duka mfano la nguo ukaweka biashara yako huku ukawa unamlipa 500-1000 mwenye frem kila siku.

hapo nimekadiria upo home, friji lipo, blender, kiti meza pia unaweza vitoa home. otherwise gharama za mtaji zinaweza fika hata laki 2 au 3.

Mm nimewaza hayo, Mengine utajiongeza mwenyewe depending na mazingira uliopo. Kila la kheri.
----
Sababu unauza vocha tayari ongezea kwenye biashara yako ya vocha yafuatayo:-
  • magazeti (haya hayaitaji mtaji unachukua kwa wakala ukiuza unakata (tshs 40 yako au zaidi sina uhakika) na yanayobaki unamrudishia wakala
  • sigara, biscuits, pipi, n.k. (huu mtaji wake ni mdogo)
  • juice (tena tengeneza zako mwenyewe) hapo profit margin itakuwa kubwa.., lakini utahitaji zile dumu portable ili uweke barafu ziwe za baridi pia unaweza kuuza na maji
  • Ongea na wafanyabiashara wenye maduka ili hata uweke pesa kidogo rehani (kama laki moja) ili wawe wanakupa bidhaa za kuuza kwa mali kauli, yaani ukishauza unawapa pesa zao na wewe unachukua faida usipouza unawarudishia
  • Karanga (kuna mtu aliniambia hii biashara Tshs 1 inazaa Tshs 1)
  • Sababu Arusha watalii wengi inategemea location yake sababu vilevile unaweza ukaongea na watu wenye ule urembo wa kitamaduni na vinyago ukaweka sample kwenye kijiwe chako ukiuza basi unapata commission yako usipouza basi hauna hasara.
Kumbuka kama umefanikisha kupata mkate wa kila siku kwa kuuza vocha ambazo faida ni ndogo kwa unit moja (basi inaonekana unauza volume kubwa sana) just imagine kama utatengeneza juice zako mwenyewe..., ukipata wateja hao hao wanaonunua vocha ukawaconvince wakanywa juice basi huenda faida ikawa zaidi 300%
----
Mwana,chukua beli moja la mtumba jeans za kiume. Chambua nzuri weka pembeni.zinazobaki piga mnada hata kwa buku buku hata jero.matambala yanayobaki yakatekate wauzie wenye gereji kwa mafungu.

Zile nzuri ulizopata kwa kua upo arusha zipeleke migodini kwa wana aporo uza moja moja.piga ka miezi 2 halafu urudi hapa useme imekuaje.

kwa hapa dar beli zuri unaweza pata kwa tsh160000/-.mia
----
Sijui unakaa maeneo gani lakini kama kuna gereji au soko yaani mahali penye watu wengi. Unaweza ukanunua baiskeli (pia sijui huko itakuwa shilingi ngapi) halafu watu wakawa wanakodisha na kurudisha. Nakumbuka hapa wanatoa 300/= hadi 500/= kutegemeana na umbali. Unaweza weka mbili ukipata watu watano kwa siku kwa kila baiskeli unapata 300x10=3,000 kwa siku. Na hii inakuwa 3,000x20=60,000/= kwa mwezi.
Huu ndio ushauri wangu kwa huo mtaji.
----
Swali la namna hii limekuwa likiulizwa na wengi, kwani watu wengi wanashindwa kubaini fursa ya biashara; hata hapa unaweza usipate majibu sahihi kwa biashara ya kufanya kutokana na vigezo vya fursa ya biashara.

Fursa yeyote ya biashara inategemea na mahali ulipo na uhitaji katika eneo husika. Kwa kufuata vigezo vya fursa ya biashara; unatakiwa kuangalia mahitaji yanayokuzunguka katika eneo ulilopo kutokana na kiasi cha mtaji ulionao.

Kama upo Dar, unaweza kufanya biashara kuuza samaki wabichi au kukaanga katika eneo ulilopo au eneo ambalo hakuna biashara hiyo. Hii unaweza kufanya nyakati za asubuhi na jioni unaweza kuuza supu ya pweza. Hii ya supu ya pweza ndio iwe biashara kuu kwa kukuza mtaji wako. Utahitaji meza, jiko na vyombo; unaweza kufanya uchambuzi yakinifu juu ya hili kwa kwenda feri.
----
Hongera kwa uthubutu wako ulioonyesha kama kweli una nia utafanikiwa..laki moja nayo ni pesa..thamani ya pesa uliyonayo huwezi kuiona mpaka utakapoikosa ama kuitumia..

Kwanza kabisa elewa kuwa kwa maisha ya sasa laki moja inahitaji budgeting kwa kias chake..ila uweke usistadoo pembeni kwanza ndo utafanikiwa..ushauri wangu ni kama ufuatao;
kulingana na hela uliyonayo unaweza kufanya biashara zifuatazo;

Nunua jiko la mkaa.-10000/-
karai la kuchomea maandazi 5000/-
mafuta ya kupikia lit 3...12000/-
mkaa debe 6000/-
unga kg 2 2500/-
hamira 500/-
baking powder 500/-
kibao cha kusukumia 5000/-
kontena ya kuwekea 3000/-
sukari nusu kg 1000/-
Jumla 45,500/-
hivi ni kwa kuanzia tu kwanza utaongeza kadri siku zinavyokwenda..

unaweza kukaanga maandazi ama half keki nzuri..

SOKO
Sijui unaishi.mazingira gani au maeneo gani huko mtaani kwenu sijui kumekaaje ila ninavyojua dar kuna sehemu nyingi sana za chai kila kona cafe zile..wengi huwa wanapelekewa vitafunio wao wanauza na huwa hawatengenez vyote.nakushauri mdogo wangu ongea na mmojawapo wa mhusika wa hivo vihotel mwambie mpango wako wa kupeleka maandazi ama half cake kila siku asubuh.unaweza kumuuzia 200 yeye akauza 300 ama zaid atajua mwenyewkg 2 ua unga inatoa piece 40/30 kwa size ya kawaida hapo ukimuuzia 200/300 una elfu 8-10 kwa siku.unatengeneza kibubu chako ukifika unaiweka hela yote kwenye kibubu kwakua bado una chombeza mtaji ile hela iliyobaki kama 50500/- utaendelea kununua unga na mafuta na mkaa kama ni kutumia na nauli n.k hii ni kwa vile unaanza lazima ujaribu soko likichanganya unaongeza vipimo.

Sehemu nyingine unayoweza kuuza ni kwenye maduka ya kina mangi utakachofanya utanunua unga, mafuta. sukari n.k hapo dukani kwake then yeye anakuuzia bila kukata hela yeyote..hii ndo huwa hivi..

soko lingine unaweza kutembezea majirani zako asubuh majumbani mwao na wakishazoea utaenjoy maana utatafutwa..cha muhim ni ubora wa bidhaa yako tu.

soko lingine unaweza kuweka kastuli hapo nje ya geti na majirani wakiona watanunua tu..

Zingatia kuwa:, usiangalie ni wangapi wanaofanya biashara kama hii kila mtu na bahat yake na ubora wa bidhaa yako..mfano mimi no mfugaji wa kuku karibu majirani wotee shamban kwangi wanafuga lakini nauza mpaka kuku 300 kwa wiki sasa utaona kwann inakua hivi wakat wote tinafuga kuku walewale?

Ukitaka kufanikiwa usichague kazi fanya kile kilichopo mbele yako mradi kiwe halali..ka ni maandazi nimeuza sana na ninaijua sana hii biashara.maana kama una uwezo wa kupata elf 10/15 kwa siku unataka kaz gani tena ndugu? na wakati wapo wanaooga na kukipaka mafuta asubuhi wanatoka na wanarud jioni mshahara elf 50-80 sasa wewe kwa mwez una lak3-4.5

Nipo na vibaby vinanisumbua hapa kidogo nlitaka nikuandikie na biashara nyinginenyingine ila kwa baadae vumilia ntaitembelea tena thread yako.

Kila la kheri na ulete feedback..usikatishwe tamaa thubutu utafanikiwa.


Biashara za mtaji wa kuanzia 300,000-500,000

Kama upo dar na unaweza kupata kasehemu ukaweka meza mtaani kama genge, iyo laki 3 unaweza kuanza kuuza karoti, ndizi, machungwa na nyinginezo za chakula. Bidhaa zako uzinunue mojakwa moja kutoka kwa mkulima. Wala si mbali, nenda apo Ruvu unapata mzigo wa kutosha. Huhitaji ela nyingi sana. Kumbuka tu kwamba laki inajengwa na elfu,milioni inajengwa na laki, nk.

Kwa uchache tu, kwa mfano saivi chungwa 1 wanauza sh. 30 shambani. Ukinunua gunia machungwa kama 1200) ni elfu 36 au tufanye 40 elfu. Weka usafiri kama elfu 10. Garama ya gunia unapata kama elfu 50.

Bei ya gengeni chungwa 1 ni sh. 200. Ukiuza 1200 unapata 1200x200=240,000. Ukitoa garama elfu 50, unabaki na faida ya sh. 190,000. Hiki ni kitu kimoja tu, bado hujaweka karoti. Nafikiri unajua bei ya karoti moja.

Kwa mtazamo wangu, huhitaji mtaji mkubwa ili utoke. Kidogo ulichonacho ukikusanya kwa malengo kitakua kikubwa. Usidharau iyo laki 3, inategemea unaipangilia vipi. Swala ni kujipangia muda tu na wewe kuwa tayari.

Mi nafahamu mtu aliyeanza kufanya biashara ya kuuza mifuko ya rambo Arusha miaka ya 1990 kwa bei ya rejareja, badae kaanza kusafiri kuchukua mifuko hiyo kutoka Zenji na kuiuza kwa jumla Aru. na nairobi, akaongeza biashara ya kuuza nguo, kwa sasa ana ghorofa kariakoo na anasafiri kwenda china kununua mali.

-----
Unaweza kufnya biashara ya loan sharking, kwa kukopesha watu waaminifu wenye shughuli zinazowaingizia kipato kila siku kwa masharti na riba nafuu ila kwa muda mfupi. Mfano ukawa unakopesha kuanzia Tsh 10,000/- hadi Tsh 100,000/- kwa mtu mmoja kwa riba ya 10% kwa wiki au 40% kwa mwezi.

Tafuta mwanasheria au wakili akuandalie mkataba utakaokuwa unawakopesha wateja wako, pia uwe unaandikishiana nao kwa mjumbe, serikali za mitaa au afisa mtendaji wa kata pamoja na mashahidi.

Ukiwa interested niPM nikupe taratibu, sheria, changamoto, mikakati na mbinu za hii biashara.
----
Dogo Kapuku83 pesa yako inatosha kulima eka moja ya nyanya chungu (Yebo yebo). Usihesabu gharama za kazi ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe. Kuna thread humu inahusu kilimo cha Nyanya chungu ifuatilie humu itakusaidia. Limia kwenye maeneo yenye umwagiliaji. Ukianza kuchuma utavuna mzigo wa kujaza canter mara mbili kila wiki. Utapata pesa hadi utashangaa!

Dogo Kapuku83 pesa yako inatosha kulima nusu eka ya Mpunga. Nenda maeneo ya Mvomero, Msowero, Mvumi, Ludewa ukakodi nusu eka. Kwa kuwa nusu eka ni eneo dogo ni wazi shughuri nyingi utazifanya mwenyewe kwa nguvu yako. Pesa yako laki tatu itatosha hadi unaingiza mzigo sokoni naitabaki kwa sababu eka moja ya mpunga kwa kulipia kazi zote hugharimu laki sita hadi saba. Nusu eka ukiitunza kitaalaumu utavuna gunia 15 hadi 18! Gunia la mpunga hutoa kilo 70 ukiuza kwa bei ya sh 1500 utapata sh 105,000/= kwa gunia! Ukiwa na gunia 15 ukiuza mchele utapata 1,575,000/=!

Hicho kipato cha mpunga kinawezekana na hiyo bei ya mchele ni wastani tu! Usithubutu kulima mahindi kwakuwa ni rahisi sana kupoteza pesa yako uliyoihangaikia kuipata. Kilimo cha mahindi kinategemea mvua ni cha kubahatisha sana. Nakutakia safari njema kuelekea kwenye utajiri wako! Ukitaka utaalamu wa mpunga au Nyanya chungu ni PM!
----
Kuna sehemu moja humu humu jukwaani inasema hivi.
kwa mfano.
ukiwa na mtaji wa laki 2.5 unatosha kuanzisha mradi wa mamilions ya fedha baada ya muda mfupi, sharti kuwepo uangalizi wa hali ya juu bila kumwachia kijana wa kazi peke yake maana yeye ni mtu wa mshahara tu.
nunua kuku 25 *10,000=250,000
Makoo (20)
jogoo(5)
Hakikisha unanunua kuku wako wakiwa kutoka kwa wafugaji walioko nje ya mji yaani usinunue sokoni, andaa safari uwafuate huko vijijini.
mara baada ya mwenzi mmoja kuku wote watakua wanataga kwa kuwa na lishe bora.
mwezi unaofuatia kuku wako watakua wanaatamia kwa mtindo huu.
20*mayai10=200 hii ni kwa mwezi na siku chache je miez 4


Biashara za mtaji wa kuanzia 600,000-900,000


Laki 8 ni nyingi sana kama unajicho pevu la tatu la kuziona fursa,binafsi nishaanzaga na mtaji wa Tsh40000(elfu arubain tu) right now nina ROI ya 7m kama faida every two weeks ni ngumu kuamini but thats it..anyway nisikuchoshe

Tafuta washing machine with dry cleaning system, used atleast ichukue kwa 400000 Huna haja ya kununu liquid soap you can make it by your own at your home.

Huna haja ya kukodi frem..tafuts eneo lavwazo hapo nyumbani kwako au chumba cha wazi
Tafuta hosteli na vyuo vyenye mkusanyiko wa watu wengi maeneo ya karibu yako..bandika ads kwamba unafua na kupasi nguo za wanafunzi na watu wengine kwa bei nafuu na ofa maalumu plus nguo za aina yoyote..lets say unafua na kupasi T-shirt na jeans kwa 2500 each@1250 plus ofa ya kufua boxer na vest/sidiria na chupi bure kwa mhusika mmoja..

400000 ivunje kama ifuatavyo: toa 50000 nunua baiskeli toa 100000 ingia mkataba wa miezi mitano kwanza na kijana mdogo kutoka uswekeni ambaye hana ajira wa kumlipa 20000 kila mwezi plus allowance ya 500 kwa kila complete order anayoileta(ya 2500)..mpe baiskel kwaajili ya kuchukua na kurudisha order za watu.huyu kijana usisahau kumpa motisha za malazi chakula na matibabu.
Imebaki 250000:Ivunje kama ifuatavyo

Toa 50000 nunua pasi na perfumes mbili moja ya kike na moja ya kiume(perfume ni mbwembwe tu kwa wateja wako)
Toa 30000 nunua enga za bei rahisi au tafuta muuza mitumba akuelekeze material ya kununua kwa ajili kutengeneza enga za gharama nafuu..hizi enga zitumike kutudukia na kudeliver nguo za watu..ila zisibaki kwa wateja.

Toa 30000 tengeneza kijikabti au sanduku nyuma ya ile baiskeli kwaajili ya kucollect na kudeliver order za watu.
Imebaki 140000 toa 50000 ingia mkataba na muuza maji wa karibu yako kuchukua dumu tatu kwa hesabu ya 750 kila siku za kazi kwa muda wa miez miwili..NB:Kama una'access na maji ya bure hii ni salama yako

Imebaki 90000 toa 40000 kwaajili ya kununua liquid soap materials pamoja na jiki material ya kutengeneza jiki nyumbani..
Imebaki 50000 toa 35000 iweke iwe pesa ya kulipia gharama za umeme kwa kipindi cha atleast mwezi mmoja na nusu..na 15000 kwaajili ya yale mabandiko ya printed white paper kama matangazo NB:inabidi wewe na yule kijana muwe nembo muhimu ya kuitangaza biashara yenu msitegemee mabandiko tu.

Kilichobaki ni kuanza kazi na kusubiri mvua ya wateja itakayo kuwa ikimiminika hapo ulipo..
Zingatia huduma nzuri kwa wateja wako.Na pia zingatia ulichowekeza na utakachokuwa ukikipata kama faida...pia zingatia ghatama nafuu kwakila huduma ya kuzisafisha nguo za wateja wao..lengo ni kuwa'outstand major dry cleaning franchises na kuprovide huduma kama yao ila kwa bei nafuu..Zaidi ya hapo SEE YOU AT THE TOP..WISHING YOU ALL THE BEST ;)
----
Ok sasa fanya hivi :
1. tafuta sehemu nzuri ya kufunya hiyo biashara kwanza usilipie wala kuanza kusema utafanya hiyo biashara ila zunguka angalia hilo eneo ulilolichagua kwa kulifanyia utafiti kama watu hapo wakiwekewa chipsi wataonyesha mwitikio.

2. angalia nani mwingine hapo jirani na yeye anafanya biashara ya chipsi na je anafanikiwa wapi na anashindwa wapi?

3.ww ukifungua hapo biashara ni nn ufanye kuboresha biashara yako zaidi ya mwenzio na kama hakuna mwingine hapo, basi ni vipi utawafanya watu waanze kuja kwako.

4. ubora wa huduma je utauweza kulingana na hayo mazingira yako.

Mwisho ufanye tathimini je ! mtaji wako utatosha ? na nguvu kazi yako ? huo sasa ndo uchambuzi yakinifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Du kwa mtaji huo?ningeweza kusema ufungue shoe shine lakin hauta tosha,basi fanya hiv nenda JF saccos iweke hiyo hela ugenerate three time upate angalao laki 6 labda utaweza fanya kitu.

Mitaji kama hii inahitaji biashara ya kupita mikononi, yaani ununue kwa producer na uuze kwa mlaji bila kukaa na bidhaa , ukishaanza kununua vitendea kazi vya biashara yako basi hutafika uendako.
 
Mitaji kama hii inahitaji biashara ya kupita mikononi, yaani ununue kwa producer na uuze kwa mlaji bila kukaa na bidhaa , ukishaanza kununua vitendea kazi vya biashara yako basi hutafika uendako.
Mkuu hiyo biashara ya mikononi ndio me naitaka,nimeisha anza na vocha,naona haiko vibaya sana,so nataka kuzifanya za aina mbalimbali nctegemee ya aina moja tu.
 
mkuu hakuna biashara duniani inayoanzishwa na mtaji kamili
anunue atakavyoweza vingine ataazima
Mkuu mimi kila nikiiangalia laki 2 aisee naona bora jamaa akomae na vibarua aiongezee kwanza, haka kamtaji kwa kujiajiri mwenyewe bado naona kama ni ndoto aisee!

Sababu tatizo ni kwamba hakuna biashara ambayo inapick up katika start up stage, sasa usishangae jamaa akaja akapoteza laki 2 badili ya kuiongeza hiyo laki 2, na am sure jamaa kajituma vya kutosha kupata hiyo laki 2 so bora aikeep na akomae na vibarua tu.
 
Sababu unauza vocha tayari ongezea kwenye biashara yako ya vocha yafuatayo:-
  • magazeti (haya hayaitaji mtaji unachukua kwa wakala ukiuza unakata (tshs 40 yako au zaidi sina uhakika) na yanayobaki unamrudishia wakala
  • sigara, biscuits, pipi, n.k. (huu mtaji wake ni mdogo)
  • juice (tena tengeneza zako mwenyewe) hapo profit margin itakuwa kubwa.., lakini utahitaji zile dumu portable ili uweke barafu ziwe za baridi pia unaweza kuuza na maji
  • Ongea na wafanyabiashara wenye maduka ili hata uweke pesa kidogo rehani (kama laki moja) ili wawe wanakupa bidhaa za kuuza kwa mali kauli, yaani ukishauza unawapa pesa zao na wewe unachukua faida usipouza unawarudishia
  • Karanga (kuna mtu aliniambia hii biashara Tshs 1 inazaa Tshs 1)
  • Sababu Arusha watalii wengi inategemea location yake sababu vilevile unaweza ukaongea na watu wenye ule urembo wa kitamaduni na vinyago ukaweka sample kwenye kijiwe chako ukiuza basi unapata commission yako usipouza basi hauna hasara.
Kumbuka kama umefanikisha kupata mkate wa kila siku kwa kuuza vocha ambazo faida ni ndogo kwa unit moja (basi inaonekana unauza volume kubwa sana) just imagine kama utatengeneza juice zako mwenyewe..., ukipata wateja hao hao wanaonunua vocha ukawaconvince wakanywa juice basi huenda faida ikawa zaidi 300%
 
Sababu unauza vocha tayari ongezea kwenye biashara yako ya vocha yafuatayo:-
  • magazeti (haya hayaitaji mtaji unachukua kwa wakala ukiuza unakata (tshs 40 yako au zaidi sina uhakika) na yanayobaki unamrudishia wakala
  • sigara, biscuits, pipi, n.k. (huu mtaji wake ni mdogo)
  • juice (tena tengeneza zako mwenyewe) hapo profit margin itakuwa kubwa.., lakini utahitaji zile dumu portable ili uweke barafu ziwe za baridi pia unaweza kuuza na maji
  • Ongea na wafanyabiashara wenye maduka ili hata uweke pesa kidogo rehani (kama laki moja) ili wawe wanakupa bidhaa za kuuza kwa mali kauli, yaani ukishauza unawapa pesa zao na wewe unachukua faida usipouza unawarudishia
  • Karanga (kuna mtu aliniambia hii biashara Tshs 1 inazaa Tshs 1)
  • Sababu Arusha watalii wengi inategemea location yake sababu vilevile unaweza ukaongea na watu wenye ule urembo wa kitamaduni na vinyago ukaweka sample kwenye kijiwe chako ukiuza basi unapata commission yako usipouza basi hauna hasara.
Kumbuka kama umefanikisha kupata mkate wa kila siku kwa kuuza vocha ambazo faida ni ndogo kwa unit moja (basi inaonekana unauza volume kubwa sana) just imagine kama utatengeneza juice zako mwenyewe..., ukipata wateja hao hao wanaonunua vocha ukawaconvince wakanywa juice basi huenda faida ikawa zaidi 300%

Jitahidi kufuata ushauri aliotoa hapa maana ndivyo hata mie nafikiria. Si vema kuanzisha biashara nyingi ambayo inaweza kukuongezea gharama za uendeshaji, bora hii ya vocha uendelee nazo na papo hapo ongeza bidhaa nyingine kama livyoshauri mdau hapo juu hadi mtaji wako uongezeke.

Usifanye haraka kujenga ghorofa, bora weka msingi imara kwanza. Sipendi kuongelea mengi nisijechafua hayo aliyokushauri mdau.
 
59 Reactions
Reply
Back
Top Bottom