Msaada kwa mfanyabiashara yeyote aliye Dar es Salaam nitatoa asante ya Tsh milioni tatu cash

Wana JF
Ninaishi Dar es Salaam. Nina ardhi ya kutosha Mpwapwa, Kongwa, Malinyi na Kilombero. Baada ya kufanya research ya kutosha, nimeamua niingie kwenye kilimo na ufugaji mkubwa wa kisasa ili kupunguza msongo wa kusubiria mshahara mwisho wa mwezi. Tractor nimeshaagiza Japan lipo njiani linakuja. Nina mpango pia wa kuwa na mashine ya kuvunia mpunga hapo baadaye. Kukamilisha mradi huu ili uweze kuanza,ninahitaji mkopo wa Tsh Ml. 80 mpaka Ml.100. Dhamana ninazo namaanisha Hati za nyumba zangu 4 hapa Dar es Salaam. Nimejaribu kupita katika baadhi ya Benki, wanasema wao wanakopesha wafanyabiashara wakati mimi si mfanyabiashara. Hivyo natafuta mtu yeyote ambaye ni mfanyabiashara mwenye transactions nzuri za walau Ml 10 kwa kila mwezi, nimpe Hati ya nyumba yangu moja aende Acces Bank akakope maana Acces Bank wanakubali mtu kukopa kwa dhamana ya mtu mwingine. Likikamilika hilo asante yangu nitatoa Tsh.Milioni 3 cash
Hivyo naomba kwa yeyote mwenye sifa hiyo, anitafute kwa namba ya simu 0767 87 60 86 ili tufanye mchakato
Shukrani

kaka hiyo riba utaiweza au umepanga kuiachia nyumba nn lakini. poa maana kilimo na hujawi lima mbona mtihani
 
Nyumba Dsm ni mtaji mzuri sana kama una nyumba nne,uza moja yenye thamni ya juu upate mtaji,kufanya bizness kwa mkopo ni majanga ndio mwanzo wa kutafuta pressure/ulcers/kisukari/stroke etc!
 
Wana JF

Ninaishi Dar es Salaam. Nina ardhi ya kutosha Mpwapwa, Kongwa, Malinyi na Kilombero. Baada ya kufanya research ya kutosha, nimeamua niingie kwenye kilimo na ufugaji mkubwa wa kisasa ili kupunguza msongo wa kusubiria mshahara mwisho wa mwezi. Tractor nimeshaagiza Japan lipo njiani linakuja. Nina mpango pia wa kuwa na mashine ya kuvunia mpunga hapo baadaye. Kukamilisha mradi huu ili uweze kuanza,ninahitaji mkopo wa Tsh Ml. 80 mpaka Ml.100. Dhamana ninazo namaanisha Hati za nyumba zangu 4 hapa Dar es Salaam.

Nimejaribu kupita katika baadhi ya Benki, wanasema wao wanakopesha wafanyabiashara wakati mimi si mfanyabiashara. Hivyo natafuta mtu yeyote ambaye ni mfanyabiashara mwenye transactions nzuri za walau Ml 10 kwa kila mwezi, nimpe Hati ya nyumba yangu moja aende Acces Bank akakope maana Acces Bank wanakubali mtu kukopa kwa dhamana ya mtu mwingine. Likikamilika hilo asante yangu nitatoa Tsh.Milioni 3 cash.

Hivyo naomba kwa yeyote mwenye sifa hiyo, anitafute kwa namba ya simu ili tufanye mchakato.

Shukrani

Suspicious comments while letting innocent comments through
 
Hizo hati ni zako kweli au ni za nyumba ya mtu
mwingine ? Maana kama una hati kweli Benki hawashindwi kukukopesha fedha ndogo kama hizo
Anachosema ni kweli. Bank zetu bado hovyo sana. Hawakopeshi kma dhamana ya kuweka aldhi,nyumba,gari au assets nyingine. Nimewahi taka just 10m kwa haraka na ningerudisha ndani ya 2months.nikawapelekea gari ya sh 25m na kadi yake. Wakakataa!
 
pia hata mimi nakushauri uende TIB, wakikuzingua tafuta leseni ya biashara yeyote uwe nayo. Suala la mzunguko wa benk ninaamini kwa jinsi maelezo yako ulivoyatoa utakuwa ni mteja wa benki yeyote ile hpa tanzania, so huwa baadhi ya benk hukubali kuwaonesha mzunguko wako hata wa benki nyingine na si lazima uwaoneshe mzunguko wa benki unayoikopa. pia mabenki mengi hv sasa wanachokiangalia zaid ni dhamana zako mzee hayo mambo mengine ni fomalite tuu.hizo m3 zako ni her wale maafisa mikopo ili usiwe na lawama na mtu, kopa mwenyewe. nakushauri ukikosa TIB nenda CRDB ukikosa labda NMB hayo mabenk mengine riba zao mhhh af wnadai kinyama.
 
Wana JF
Kwa mlionishauri niende TIB Bank dirisha la kilimo nimeenda leo. Mlolongo wa pale si wa kitoto. Masharti ni mengi zaidi ya ya World Bank kama si IMF.Kwa mliohoji kuhusu uhalali wa hati ni kwamba nyumba zote zina hati na Hati zipo kwa jina langu mimi mwenyewe na si jina la mtu mwingine. Kwa walionishauri suala la kuuza nyumba moja nimeafiki wazo hilo so natangaza kuuza nyumba moja iliyopo eneo la Madale kwa bei nzuri tu. Kiwanja kina ukubwa wa Square Meter 1203 na hati ya umiliki ya miaka 33.
Kwa aliye serious tuwasiliane
Shukrani
 
Wana JF
Kwa mlionishauri niende TIB Bank nimeenda leo pale Mlimani City. masharti ya kupata mkopo ni mengi na magumu kama ya World Bank kama si IMF. Kwa mlioniuliza kama Hati zina jina langu au za mtu mwingine jibu ni kwamba nyumba ni za kwangu na zote zina Hati yenye majina yangu. Si za kurithi wala kuwa share na mtu. Suala la partnership bado sijalifikia lakini mwenye mawazo hayo namkaribisha. Kwa mlionishauri niuze nyumba moja nimekubaliana na wazo hilo hivyo natangaza kuuza nyumba yangu moja iliyopo Madale yenye ukubwa wa eneo wa Square Meter 1203. Bei ni maelewano lakini nafuu. Kwa aliye serious tafadhali tuwasiliane
Shukrani
 
Wana JF
Kwa mlionishauri niende TIB Bank dirisha la kilimo nimeenda leo. Mlolongo wa pale si wa kitoto. Masharti ni mengi zaidi ya ya World Bank kama si IMF.Kwa mliohoji kuhusu uhalali wa hati ni kwamba nyumba zote zina hati na Hati zipo kwa jina langu mimi mwenyewe na si jina la mtu mwingine. Kwa walionishauri suala la kuuza nyumba moja nimeafiki wazo hilo so natangaza kuuza nyumba moja iliyopo eneo la Madale kwa bei nzuri tu. Kiwanja kina ukubwa wa Square Meter 1203 na hati ya umiliki ya miaka 33.
Kwa aliye serious tuwasiliane
Shukrani

Kwanza nikupongeze kwa kuwa mtu unayekubali kuchukua ushauri was wengine .... pili umenifurahisha sana kwa kuamua kwenda TIB na kujionea mwenyewe halafu ukajipima lipi ufanye ..... Kubwa zaidi ni maamuzi magumu uliyofikia kuamua kukonvert asset yako into liquid finance

Stay focused your dream will come true

I wish you all the best mkuu

Nitaomba kwa manufaa ya wote uendelee kutupatia updates hapa jamvini kwa yanayojiri katika mwendelezo wa plans zako za kilimo

God bless you
 
Ila mkuu Acess mikoani wanakopesha wakulima hebu wacheki watakupa taarifa nzuri
 
Back
Top Bottom