Msaada kwa kaka huyu!

G M S

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
502
53
Jf members nahitaji mchango wa mawazo yenu katika hili;
nna rafiki yangu ambaye alimaliza elimu ya msingi muda mrefu na baada ya hapo akajikita katika kazi za gereji ni mda mrefu sasa na hata ujuzi katika ufundi wa magari anao wakutosha isipokuwa sasa anasema alitaka japo apate kazi hata ya udereva katika sekta yoyote selikalini alijaribu kwenda chuo(NIT) kutaka kujiunga akaambiwa wanataka mtu aliyefikia elimu ya kidato cha nne nimeona nije hapa kwenu kupata ushauri je kwa elimu yake ya darasa la saba anaweza kujiunga na chuo kitachomuwezesha kupata chet na kazi pia je ni vyuo gani anaweza kwenda?
 
Kwa mfumo wa sasa haiwezekani kabisa kwa mujibu wa kanuni mpya wa NIT
 
Mfumo kwa sasa umebadilika na hasa kama anataka kupata ajira serikalini. inabidi uwe na elimu ya kidato cha nne kuweza kuajiriwa kama dereva au fundi serikalini, hii ni kutokana na kanuni za utumishi za mwaka 2003 na hata sheria namba 8, 2002.

Unaweza kumsaidia kwa kumtambulisha katika 'madarasa ya watu wazima' ambapo elimu ya sekondari(o-levo) ataipata kwa kipindi cha miaka miwili na atafanya mitihani ya NECTA-CSEE. Hii ndo njia rahisi itakayomsaidia kuutumia ujuzi wake 'formally' na kuheshimika
 
Ni kweli mkuu. Ingekuwa ni private sector isingekuwa issue.
 
Ni kweli mkuu. Ingekuwa ni private sector isingekuwa issue.
Inaweza kweli kuwa rahisi huku PS lakini hata sector hii ni pana mno, mfano, nikikuajiri mm kunipeleka kazini na kunirudisha home usalama wa kibarua chako mara nyingi sana haulindwi na sheria kwani nitakuajiri kama tunavyoajiri ma housegirl/boys huku uswahilini (kwa malipo ya tshs45000/=) kikubwa hapa ni kuwa kama atataka awe na usalama wa kuaminika kazini haijarishi ni kwenye public au private sector ni vizuri akajiendeleza kielemu na kwa kweli siku hizi elimu inapatikana kwa urahisi suala zima ni kunia pekee.
kama ameweza kujiendeleza hadi kuwa mahiri katika ufundi haizuii ni kwanini asifanye masomo ya miaka miwili na isije kuwa kigezo hapa ni inglish sekondari kwani majina na vitu vingi vya kiufundi havina majina ya kiswahili
 
..akafanye elimu ya watu wazima,miaka 2 tayari form then kutoka hapo anasonga tu
 
Mwambie anitafute nimuuzie cheti cha form four aende NIT akapige shule.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom