Msaada kwa huyu dada

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
573
habari

kuna dada mmoja amenieleza kisa hiki kimemtokea hadi sasa anashindwa aamue nini

huyo dada kaolewa kwa ndoa ya kanisani miaka 11 iliyopita na wamejaliwa watoto 2 ila karibu kuna tatizo kubwa ambalo limemuuza sana . alipata ujauzito na yalikuwa makubalianno yake na mmewe watafuta mwana ili akijifungua aachane na masuala ya uzazi tena,

alipobeba mimba hii yaani ya tatu baada ya mwezi akashangaa mme kidogo kama ameanza kubadilika . ujauzito ulipofikisha miezi 3 na nusu (week ya 16) tatizo ndipo lilipojitokeza, mme alitoka kazini na akapita kwenda kupata moja moto na baridi kama ilivyo ada lakini ilipofika saa nne usiku mme kazima simu na mke alijitahidi kumtafuta mara kwa mara lakini hakumpata .. imefika saa 11 mme kawasha simu na kumpigia mke lakini alikuwa ndo kafika getini. huyo dada alipata mshutuko pamoja na hasira ikapelekea kuanza kutokwa na damu ya hedhi . mwanaume akampeleka hosp na akamwacha na yeye kuendelea na arobaini zake pasipo hata kufuatilia hali ya mwenzake.. yule dada kapata mapumziko pale hosp, mme hakurudi tena kumjulia hali mwenzake. asubuhi ya siku iliyofuata jamaa ndo kaenda hosp na akaambiwa mwenzake anaweza kutoka kurudi nyumban, jamaa kaenda kuommba bili akapewa akalipa akaondoka na kumwambia mwenzake amjulishe akitaka kutoka . aliporuhusiwa mida ya saa nne jamaa akamwambia mke yuko busy sana achukue taksi arudi nyumbani.

jamaa aliporudi usiku sana hakuweza hata kumuuliza mwenzake kuhusu maendeleo yake na wala alivyo muacha hosp zaidi ya yule dada kumjulisha karuhusiwa na jamaa kumwambia achukue taksi jamaa hakuwasiliana na mke wake hadi usiku saa 8 amerudi home . wamekaa kwa wiki mbili bahati mbaya yule dada akiwa nyumbani alianza kutokwa damu mida ya saa 9 alasiri akamjulisha mme kuhusu mabadiliko hayo na pia akamwambia kaongea na dr ameambiwa aende haraka hosp. jamaa kama kawaida akamwambia mwenzake aende hosp anakuja . yule dada amefika hosp akaambiwa mimba imeharibika inabidi kusafishwa haraka kitu alichoweza ni kumpatia dr. namba ya mmewe ili aongee nae kwani yule dada asingeweza kuongea (alikuwa analia tu) jamaa akamewambia dr aendelee na matibabu atakuja . jamaa kaenda hosp saa 4 usiku akamkuta yule dada hajarejewa na fahamu vizuri kwani alisafishwa saa 12 jioni. jamaa baada ya kuambiwa mkewe hajarejewa na fahamu jamaa akaondoka kurudi home.

asubuhi ameenda kumjulia hali mke wake saa 3 na pia kuonan na dr ambaye alimweleza hali ya mkewe na akamwambia anataruhusiwa baadaye kwenye saa nne. jamaa akaomba bili akalipa na kuondoka bila hata kumuaga mkewe. aliporuhusiwa mke ilimlazimu kuchukua taksi na kurudi nyumba ambapo jamaa hakuweza kumpigia hata simu kujua maendeleo yake , na tangu tukio litokee hilo ni kama week 3 zimepita na ndani hakuna mawasiliano kati yako hata maongezi ,. jamaa rudi yake imekuwa ni usiku mkubwa , na mke hajaulizwa ahta maendeleo yake kiafya. mke kakata tamaa anataka achukue hatua hata ya kutengana na mwenzake
 
jamaa ulimbukeni tu unamsumbua huyo.ts paining but huyo dada avumilie tu jamaa atarudi kwake
 
Huyo dada aende kulalamika kwa ndugu za mumewe yaani mkwewe au ndugu wa karibu nahisi watamsaidia
 
kumshauri jambo kwanza tunatakiwa tujue status yake
je ni mfanyakazi au biashara
je anajiamini kuwa hata yeye peke yake anaweza ?
hapo atatusaidia na wachangiajai kutamka kuwa
sasa nenda ukaanze maisha yako tena na watoto wako sehemu
nyingine au la,
ni ngumu sana kama yeye kula na kulala kwakwe anategemea huyo mume then ajiondoe ki urahisi kiasi hicho
lol hizi ndoa sijui kama yangu itafika maana nazidi kusogeza mbele tu.
 
Si amuulize mumewe kuna nini kilichozidi au kupunguwa?

Hii ni habari ya upande mmoja. Kwanza cha kujiuliza, huyu aliyoleta mada kayajuwaje yote haya in details? Kama yu karibu na hii familia kiasi cha kuyajuwa yote haya kinamshinda nini kusikiliza pande zote mbili? Badala ya kuleta ushambenga humu JF angeanza kwa kuwasikiliza mke na mume na angepata solution ya maana badala ya kutuletea habari za upande mmoja.
 
yawezekan huyo jamaa alishafunga kizazi bila kumwambia mkewe,kuonna hiyo mimba ndio kumemchanganya....habari ya asubuhi lakini..
mmhh laikn swaga nyeusi kazianza wakat mimba ishakua kubwa...soma fresh

no justfcation
 
lazima kuna kitu kikubwa sanasana kipo nyuma ya pazia, ongea na huyo dada atakwambia tu
 
Usione soo sema naye, sema nayee
Aache utoto wake, utoto wakee
mwite pembeni mwambie, umwambie
we ndie mpenzi wake, mpenzi wakee

Kama kuna ulilomkosea akweleze, aache kukuchezesha kombolela la moyo. Ye ni mtu mzima


Akiendelea kula bati, kwani hilo bati shing ngapi bwana?? Kula bati hamisha mapenzi kwa watoto songa mbele.
 
mbona hii story ina upande mmoja labda utueleze huyo jamaa kaanza kupat a uchizi lakini kuna sababu na je amejaribu kuongea nae au kuchunguza nini kinaendelea kwenye maisha ya mwenzake kabla ya kuchukua maamuzi
 
kumshauri jambo kwanza tunatakiwa tujue status yake
je ni mfanyakazi au biashara
je anajiamini kuwa hata yeye peke yake anaweza ?
hapo atatusaidia na wachangiajai kutamka kuwa
sasa nenda ukaanze maisha yako tena na watoto wako sehemu
nyingine au la,
ni ngumu sana kama yeye kula na kulala kwakwe anategemea huyo mume then ajiondoe ki urahisi kiasi hicho
lol hizi ndoa sijui kama yangu itafika maana nazidi kusogeza mbele tu.

ni mwajiriwa na yeye kma yeye anaweza kujimudu ila anaangalia suala la watoto maana mtoto wa kwanza ana miaka 9 wa pili ana miaka 5
 
lazima kuna kitu kikubwa sanasana kipo nyuma ya pazia, ongea na huyo dada atakwambia tu

nilijaribu kuongea nae huyo dada maana hata mimi nilimwambie kitu kam hicho lakini si unajua wengi wanapenda kusukuma makosa yote kwa wenzao...
 
Huyo dada aende kulalamika kwa ndugu za mumewe yaani mkwewe au ndugu wa karibu nahisi watamsaidia

hili suala liko kwenye familia na lilianza kitambo kidogo na jamaa kuna vikao anakwepa ..
 
Nadhani mwanaume huyo amebadilika ghafla sana na inaonekana hana time kabisa na mke wake. In fact mi nahisi kama labda huyo mama alimkosea mume wake. kwani alifanya nini siku ya kwanza? siku ile alianza kupata matatizo (concidentely na ndio siku mume alianza kubadilika). labda alijaribu kutoa bila kumshirikisha mume wake? nadhani tuna hitaji version ya mume pia
 
Si kawaida mwanaume kufanya hivyo, hata kama ni mtu wa kucheat sana. Labda jamaa kashtukia mimba si yake kwa namna anazojua yeye. bado kuna siri kubwa ambayo wanajua wenyewe hao wawili.
 
Si kawaida mwanaume kufanya hivyo, hata kama ni mtu wa kucheat sana. Labda jamaa kashtukia mimba si yake kwa namna anazojua yeye. bado kuna siri kubwa ambayo wanajua wenyewe hao wawili.

mkuu tatizo wengi hupenda kuonyesha wamekosewa kuliko kukosea
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom