Msaada kwa huyu binti, anaumia

successor

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
3,078
6,123
Nina rafiki yangu wa kike ambaye tumeshibana sana kiasi ambacho ananishirikisha hadi mambo yake ya kimahusiano. Hivi karibuni amenieleza yanayomsibu/anayopitia kwa sasa.

Ameanza kwa kunieleza kwamba wakati anasoma O-Level (Boarding) alikutana na mwanafunzi wa kiume aliyekuwa anasoma shule ya jirani na aliyokuwa akisoma yeye. Ingawa huyo wa kiume alikua amemtangulia kidato kimoja. Walipendana na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi. Walipendana kiasi cha kupeana ahadi nyingi za kuja kuwa na familia hapo baadae. Na kwa wakati wote walipokuwa kwenye mahusiano wakiwa shuleni, walikutana kimwili mara moja.

Siku zilisogea na hatimaye yule kijana wa kiume akamaliza kidato cha 4 na kurudi kwao Moshi(Mchaga), akamuacha huyu binti anamalizia mwaka wa mwisho, naye akamaliza na kurudi kwao Dodoma(Mgogo). Baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano kati yao. Maana hakuna aliyekuwa na simu.

Huyu binti akafanikiwa kwenda Advance akamaliza na kufanikiwa kwenda chuo. Alipofika chuo bila kutarajia akakutana na yule mpenzi wake akiwa mwaka wa pili. Kilichomshangaza huyu binti ni ile hali ya yule kijana, hakuonyesha kumchangamkia/kufurahi kwa kukutana tena baada ya kupotezana kwa muda wote wa zaidi ya miaka miwili akizingatia kwamba walipendana na kupeana ahadi nyingi tamu. Kwa wakati wote huo binti aliamini ipo siku watakutana na kuendeleza uhusiano wao maana alimpenda yule kijana kwa dhati.

Ni mwaka mmoja sasa tangu wakutane hapo chuoni, maana binti ameingia mwaka wa pili na kijana ndio amalizia mwaka wa tatu, lakini kijana hana muda kabisa na huyu binti kwa mwaka mzima, zaidi ya salamu tu. Amejaribu kumwambia waonane ili waongee lakini kijana haonyeshi kujali kabisa. Amemkumbusha kuhusu uhusiano wao lakini jamaa hana habari. Yaani hana time kabisa na huyu binti.

Kinachomuumiza kumuona kila siku mtu ambaye anampenda sana lakini yeye hajali kabisa. Amekuwa akijaribu kumvuta karibu kimawasiliano kwa kumpigia simu na kumtumia text mara kwa mara lakini imeshindikana. Na kwa sasa ameamua atulie tu maana ni kama amekata tamaa, lakini anaumia sana, anajiuliza maswali bila majibu kwamba ni nini hasa kimempata huyu kijana, kikapelekea akabadilika kiasi hiki. Japo anasema bado ana matumaini kidogo kuwa inaweza kutokea wakarudi kama zamani.

Je, upo uwezekano wa huu uhusiano kurudi tena kama mwanzo????

Kwa kuangalia mtiririko mzima wa hii story, je, yule kijana alimpenda huyu dada kwa dhati???

Na Je, afanye nini???

Hebu wadau jaribuni kutoa maoni yenu kwenye hili, nami nitamfikishia. Hii ni story ni ya kweli kabisa na dada yupo kwenye wakati mgumu sana.

Naomba wakuu mtoe maoni yaliyojaa hekima.

KARIBUNI.
 
Kupoteana aside, rafiki yako needs to realize in general people change and may grow apart as a result. It is immature for her to expect jamaa to still feel the same after all this while just cause she does. It is high time for her to move on :(
 
"kukosa mawasiliano kwa muda mrefu ni hatari kwa afya ya mapenzi"
----Ushauri----
Amfuate huyo kijana kisha aongee kilichopo ndani ya moyo wake kuhusu mapenzi yao ya zamani ili kujua hatima yake (huenda kijana hajui kuhusu mapenzi ya dhati ya binti kwake), mpaka hapo naamini atajua cha kufanya.
 
Hakuna upendo hapo. Huyo binti anapoteza muda. Ameshakua zilipendwa yaani mapenzi ya secondary bado ameyabeba mpaka chuo wakati huko ndio kiwandani kuna vigoli wa kila aina. Naomba umwambie hiyo binti kwamba asiendele kuumiza kichwa kwa mtu ambaye hamjali na hampendi. Mwambie akaze buti kwenye kitabu maana mapenzi yapo ipo siku atapata mtu sahihi na yote yatapita na atasahau.
 
mkuu mwambie asimkazie sana asubiri amalize chuo ndo amtafute, kwa totoz za chuo wote uliwahi kudate nao o level ni ligi za mchangani wakati chuo ni UEFA kabisa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom