Msaada: Kwa dalili hizi nikamuone Daktari gani na nikapime nini?

Mnabeti vipimo wazee.

Haiwezekani akafanye kila kipimo bhana...
Mkuu kuhusu HIV napima mara nyingi inakuwaga Negative.

Dalili zangu miaka yote ni hizo tu na nafuu naiona nikifanya Mazoezi ya yoga.

Sukari nimepima tena juzi hapa niko poa.

Ila nahisi hii ishu imetokana na Punyeto, nina wasiwasi kuna virutubisho havijabalansi kwenye mwili wangu
 
Mkuu kuhusu HIV napima mara nyingi inakuwaga Negative
Dalili zangu miaka yote ni hizo tu na nafuu naiona nikifanya Mazoezi ya yoga

Sukari nimepima tena juzi hapa niko poa

Ila nahisi hii ishu imetokana na Punyeto, nina wasiwasi kuna virutubisho havijabalansi kwenye mwili wangu
Punyeto inapunguza virutubisho gani mzee baba ?
 
Mkuu kuhusu HIV napima mara nyingi inakuwaga Negative
Dalili zangu miaka yote ni hizo tu na nafuu naiona nikifanya Mazoezi ya yoga

Sukari nimepima tena juzi hapa niko poa

Ila nahisi hii ishu imetokana na Punyeto, nina wasiwasi kuna virutubisho havijabalansi kwenye mwili wangu
Punyeto haina madhara hayo unayoyafikiria mzee.

Una tatizo jengine ambalo linataka utulivu kwa daktari kuligundua,inatakiwa daktari akuchukue history kwa uzuuri kwa kwa urefu mno na kwa utulivu mpaka afikie kwenye kuhisi una matatizo pengine matatu au manne,then vipimo vinaweza kuprove una shida gani

Nimekuuliza haujavimba au haujawahi kuexperience kuvimba kwenye pingili au vidole vyako hasa vya miguu ?

Jee huwaga unapata kama kifafa flani hivi ?

Je huwa unahisi kichwa kizitooo ?

Je huwa hauna tatizo la kuwa na damu ndogo mwilini mwako ?
 
Mnabeti vipimo wazee.

Haiwezekani akafanye kila kipimo bhana.

Mtu mwenye hepatitis sio kawaida kupata complication za huyo jamaa hivyo ni kumsumbua ukimuambie akapime hepatitis wakati hepatitis ina signs zakw specific.

Mtua mwenye HIV sio aghlabu eti awe na complication za huyu jamaa wakati kuna signs maarufu zinajulikana kwa mtu mwenye HIV,na ingekuwa HIV kwa miaka yote sita ingeshajulikana tu.

Hapa ini ulilotaja kwamba akapime kama ini lina tatizo haiwezekani kwa miaka sita yote aumie kwenye sehemu alizotaja tu.

Hata hilo figo halina shida kabisa kwa sababu matatizo ya figo yana dalili zake ambazo ni maarufu zinajulikana na huyu jamaa ni miaka 6 ana tatizo hilo alilotaja.

Hapo akienda kupimwa akakutwa na malaria sio ajabu daktari kilaza akamuambia malaria ndio inasababisha hiyo tatizo😄😄😄.

Watu wa afya waumize kichwa sio kubbeti vipimo mwisho wa siku mtu ana tatizo lile lileeeeee haliishi kumbe kuna tatizo walilisingizia k2amba ndo sababu ya tatizo lingine kumbe walaaaa
acha kuropoka ropka ovyo wakati hujuwi unacho kisema mwambie maradhi yake yanasababishwa na kitu gani?sio kusema maneno kama vile mlevi.
 
acha kuropoka ropka ovyo wakati hujuwi unacho kisema mwambie maradhi yake yanasababishwa na kitu gani?sio kusema maneno kama vile mlevi.
Sawa mkuu.

Ila hakuna katika nyinyi aliyesema kwamba maradhi yake yanasababishwa na kitu gani,badala yake mnabeti tu mara akapime hepatitis mara akapime HIV mara akapime nini sijui..

Huyo jamaa kwa anaetaka kumsaidia akae nae amchukue history yake vizuri sio kumkimbizia kwenye vipimo tuu mkuu..
 
Ushauri mzuri ndugu ila itabidi niwasisitize wapime hivyo vitamin B Na calcium Maana ndo vinavunja system yangu ya neva
Mkuu ukiwa na upungufu wa calcium Ni rahisi kujua viungo vinauma non-stop! Upungufu wa B vitamin huhisi njaa Wala kiu was wakati na ukihisi vitu hivyo hukosa hamu ya kula au kunywa maji
 
Huyu dokta baada ya vipimo kuonesha sina kisukari na presha yangu ipo kawaida kaniandikia nikatumie vidonge hivi
*meloxicam 15mg
*amoxiclav 25mg
*Vitamin B complex
Ngoja Nitumie Labda nitakaa Sawa
Shukrani wakuu
 
Mimi nina wasiwasi sana una tatizo kitaalamu linaitwa rheumatoid arthritis.

Hili ni tatizo ambalo kinga za mwili kimakosa zinavamia maeneo ya joints na kusababisha uvimbe na maumivu ya muda mrefu.

Hasa uliposema kuwa ukifanya mazoezi ndio unapata nafuu na hii ishu ya rheumatpid arthritis(uvimbe na maumivu ya joints) huwa mtu akifanya mazoezi yanayohusisha viungo hupata nafuu.

Hizi ni hisia zangu tu mkuu,
 
Hilo tatizo lina tiba au naweza pata kipimo gani ili kutambua hiyo shida
Shukrani mkuu
 
Unaonekana haupo active physically. Mwili wako umelegea au kukaa mazingira ya uvivu.

Badili chakula unachokula. Ongeza kiwango cha maji unayokunywa , katika diet yako ongeza sana matunda aina zote especially fibered fruits , ongeza protein rich foods. Lakini weka ratiba ya kutembea jioni umbali mrefu usiopungua kilometers 10 per day so ukienda na kurudi ni 20kms per day.

Mazoezi kama pushups , kuruka kamba, na kustretch pia ni kuhimu sana. Usile mavyakula mazito ukashiba sana usiku muda wa kulala. Usilale sana kukomoa kama kulala zaidi ya masaa manane kwa siku.

Amka mapema kama saa kumi na moja ufanye mazoezi kama hayo ya push-up ili kuwarmup mwili ila usisahau kunywa kahawa iliyochanganywa na maziwa asubuhi baada ya warm up exercises. Utaona kama huo mwili utaleta tena fyoko fyoko.

Usisahau kunywa maji kwa wingi yaani nazungumzia lita kuanzia 3 sio chini ya tatu kwa siku.... Usisahau maji. Tena ukijazia na juice za matunda mbali mbali katika hiyo diet itakuwa poa sana.
 
Hilo tatizo lina tiba au naweza pata kipimo gani ili kutambua hiyo shida
Shukrani mkuu
Mkuu kuhusu investigations vipi inafanywa ili kugundua tatizo hilo hapo naomba ukawaone madaktari waulize huu ugonjwa vipi unapimwa ili utambulike kuwa ni positive,watajie huo ugonjwa na hakikisha unaenda spitali kubwa yenye MD ukishindwa hapo nenda kwa specialist wa magonjwa ya mifupa muambie unahisi una tatizo la rheumatpid arthritis mwambie akufanyie vipimo nadhani utapata mwanga kidogo...

Na kuhusu tiba ya kuondoa tatizo moja kwa moja sina hakika na hilo lakini kupunguza ukali wa tatizo kuna dawa za kupunguza uvimbe na maumivu unaweza ukapewa kifupi huitwa NSAID's.

Zaidi nenda kwa daktari kisha muelezee juu ya tatizo nililokuambia..

Unapewaje vitamin B alafu huambiwi shida nini mpaka ukapewa vitamin B.

Amoxclav 25mg au 625mg mzee ?

Sijajua why wamekupa amoxiclav ?

Kuhusu meloxicam ni nzuri pia kwa kutoa maumivu.

Mimi sikubali kupewa dawa bila kuhoji,nikiona daktari naye mbabaishaji dawa hizo situmii kwa sababu najua kanipa kwa kubahatisha mwisho wa siku nephrotoxicity hii hapa...
 
Unaonekana haupo active physically. Mwili wako umelegea au kukaa mazingira ya uvivu.

Badili chakula unachokula. Ongeza kiwango cha maji unayokunywa , katika diet yako ongeza sana matunda aina zote especially fibered fruits , ongeza protein rich foods. Lakini weka ratiba ya kutembea jioni umbali mrefu usiopungua kilometers 10 per day so ukienda na kurudi ni 20kms per day.

Mazoezi kama pushups , kuruka kamba, na kustretch pia ni kuhimu sana. Usile mavyakula mazito ukashiba sana usiku muda wa kulala. Usilale sana kukomoa kama kulala zaidi ya masaa manane kwa siku.

Amka mapema kama saa kumi na moja ufanye mazoezi kama hayo ya push-up ili kuwarmup mwili ila usisahau kunywa kahawa iliyochanganywa na maziwa asubuhi baada ya warm up exercises. Utaona kama huo mwili utaleta tena fyoko fyoko.

Usisahau kunywa maji kwa wingi yaani nazungumzia lita kuanzia 3 sio chini ya tatu kwa siku.... Usisahau maji. Tena ukijazia na juice za matunda mbali mbali katika hiyo diet itakuwa poa sana.
Asante kwa ushauri mkuu
Ila usiniite mlegevu Unazani mazoezi ya cardio hayafai kunifanya active
Nishafanya sana pushup, nimebeba sana mavyuma ila nikagundua hayanisaiidi zaidi kama mazoezi cardio
Mi ni mdau wa Mazoezi muda mrefu na maji nakunywa sana asubuhi Nikiamka naanza na lita 1.5, nikitulia kwa siku hata lita 5 napiga

Matunda nayokula zaidi ni ndizi, nanasi na maparachichi

Mimi sio bonge uzito wangu kwa sasa ni kilo 69, nalala kwa wakati naamka saa 11 alfajiri nakunywa maji mazoezi yanaanza

Mbona majirani zangu hapa hawali diet kama mimi, hawanywi maji ya kutosha na sijawahi kuona wanafanya mazoezi ila hawana shida kama yangu
 
Back
Top Bottom