Msaada: Kwa dalili hizi nikamuone Daktari gani na nikapime nini?

BANGO JEUPE

JF-Expert Member
Nov 21, 2015
3,060
2,111
Habari Wakuu, Natanguliza Shukrani
Mimi Ni Me Umri Miaka 33
Ni Miaka 6 Naishi Na Hili Tatizo Ila Kwa Sasa Mambo Yamenizidia

*Mwili Wangu Una Maumivu Makali Ya Ndani Kwa Ndani Hasa,Mabega, shingo,nyonga na mgongo na hata kichwa Kuwa Kizito (Sio Maumivu Ya kuminya Bali ni ya ndani mfano Ukinishika shingo Sihisi maumivu, Ila Nikiipa Movement Napata Maumivu)

*Viungo Kukaza Na Kufa Ganzi Hasa Mapaja, Mabega Na Shingo

*Uchovu Na Usingizi wa Mara kwa mara

*Kukosa Umakini Na Kujiamini Na Uwezo Mdogo Wa kumbukumbu

Napata Nafuu Kidogo nikifanya Mazoezi (yoga) Asubuhi (lisaa limoja) , hii Inanifanya Niwe Mtumwa wa Mazoezi, Lasivyo Hali Inakua Mbaya Zaidi.
Wakati Wa Mazoezi Napitia Maumivu Makali Ila Inanibidi Nifanye Ili Kuleta Unafuu

NB: Kuna kipindi niliwahi tumia Vidonge vya Neorotone Nilipata Nafuu ya Muda Mfupi Lakini Hali Ikaendelea

Sijawahi Anguka Wala Kupata Ajali

Nawaza Kwenda Muhimbili Ila Sijui Nikamuone Specialist Gani Au Nikapime Nini!!?

Samahanini Kwa Maelezo Marefu
 
Miaka 6 unaumwa hujaenda hospitali? Ama ulienda lakini matibabu hayakukusaidia?

Anyway, umesema ulitumia dawa za neurotone, na zikakupa nafuu. Hizo dawa ni neuro support, kwa maana hiyo kuna madini yatakuwa yamepungua mwilini mwako.

Kuna uwezekano mkubwa ukawa na Peripheral Neuropathy.
 
Asante sana dokta Nilikua naenda hospital za huku Kigamboni nawaeleza hizo dalili, ndo nikashauriwa nitumie Neurotone
Sasa naona niende Muhimbili

Msaada kwa hizo dallili unazani nikachukue kipimo dokta
 
Asante sana dokta Nilikua naenda hospital za huku Kigamboni nawaeleza hizo dalili, ndo nikashauriwa nitumie Neurotone
Sasa naona niende Muhimbili

Msaada kwa hizo dallili unazani nikachukue kipimo dokta
Mkuu kwanza pole, pili mimi sio daktari japo nipo kwenye field ya afya.

Ila kwa maelezo yako, nadhani itabidi uonane na daktari wa kawaida kwanza (physician) kisha yeye ndio atakudirect kwa specialist anayekufaa kulingana na ugonjwa wako utakuwa umelalia wapi haswa kulingana na signs & syptoms pamoja na examinations atakazokufanyia.

Kama una bima nenda direct muhimbili, kama huna basi pitia hospitali yako unayotibiwaga wakupe referral letter kisha uende MNH.

Manners Maketh Man[/color][/b]
 
Back
Top Bottom