Msaada:kwa anayefahamu kuhusu ebay

Olsea

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
452
249
HABARI ZENU WAKUU NATUMAINI WOTE MU WAZIMA,NINAOMBA MSAADA WA MAWAZO KWA YEYOTE YULE ANAYEFAHAMU HAYA MAMBO YA KUNUNUA VITU ONLINE,NI KWAMA NIMENUNUA DC ADAPTER KWA AJILI YA LAPTOP YANGU KUPITIA eBAY NA NIMESHALIPIA LAKINI NAONA IMESHAPITA MWEZI NA WIKI CHACHE HADI LEO SIJAIPATA,SASA NILIKUA NAOMBA KWA YEYOTE YULE MWENYE UELEWA NA HAYA MAMBO NATAKIWA NIFANYE NINI?
 
we ulitaka uipataje? uliwapa physical adress yako? mlikubaliana mzigo utafika vipi? au just umenunua tu ukadhan watakuletea
 
we ulitaka uipataje? Uliwapa physical adress yako? Mlikubaliana mzigo utafika vipi? Au just umenunua tu ukadhan watakuletea

niliwapa address mkuu kwa hiyo ilitakiwa ufike address inapoelekeza.
 
HABARI ZENU WAKUU NATUMAINI WOTE MU WAZIMA,NINAOMBA MSAADA WA MAWAZO KWA YEYOTE YULE ANAYEFAHAMU HAYA MAMBO YA KUNUNUA VITU ONLINE,NI KWAMA NIMENUNUA DC ADAPTER KWA AJILI YA LAPTOP YANGU KUPITIA eBAY NA NIMESHALIPIA LAKINI NAONA IMESHAPITA MWEZI NA WIKI CHACHE HADI LEO SIJAIPATA,SASA NILIKUA NAOMBA KWA YEYOTE YULE MWENYE UELEWA NA HAYA MAMBO NATAKIWA NIFANYE NINI?

Sina hakika mahala ulipo,ila Kwa jinsi ninavyofahamu mimi, mara nyingi bidhaa zinazouzwa eBay huwa hazisafirishwi kuelekea maeneo mengi ya Africa,isipokuwa endapo muuzaji ameeleza wazi kwamba anaweza kuship to Africa.

Kwamaana hii, unaweza kuangalia kwenya account yako ya eBay kama hiyo bidhaa inaonekana imeshakuwa shipped, kama imeandikwa ipo shipped unaweza pia kucheki ni kampuni gani inayosafirisha huo mzigo na pia cheki tracking code ya huo mzigo wako, kisha uwasiliane na kampuni inayosafirisha kwa kuwapa tracking code kisha watakwambia huo mzigo ulipo.

Endapo huo mzigo haujakuwa shipped, au hakuna tracking code basi unaweza kumuuliza muuzaji atakwambia mzigo wako ulipo.

Endapo muuzaji hakupi ushirikiano wa kutosha,ndio unaweza kwenda stage ingine kwa kufungua malalamiko kwa eBay.

Inabidi ufahamu kwamba, kama ulifanya malipo kwa PayPal kuna uwezekano mkubwa sana kurudishiwa hela yako endapo utakuwa hujapata mzigo wako.ila kma umelipa kwa njia zingine huwa kuna kuwa na matatizo sana unapohitaji kurudishiwa hela.
 
Asante kwa maelezo mkuu,wacha nifuatilie ingawa wakati nanunua ilionesha kwamba wanai shipp worlwide.
 
Pole sana. Maelezo ya mdau yapo vizuri sana. Ila kabla hujafungua malalamiko yako kwa ebay, wasiliana na Muuzaji wa bidhaa hiyo kwanza kimweleza kuwa hujapata bidhaa yako.
Pia kama ulitumia PO BOX. fuatilia kwenye ofisi za posta lilipo hilo sanduku maana Hata mimi nilisha agiza na watu wa posta hawakuweka ile nyaraka ya kupokea mzigo kwenye sanduku langu mpaka nilipoenda kuwauliza na ikaonekana mzigo ulikuwa na zaidi ya wiki tatu tangu upokelewe hapo kwao.
 
Sina hakika mahala ulipo,ila Kwa jinsi ninavyofahamu mimi, mara nyingi bidhaa zinazouzwa eBay huwa hazisafirishwi kuelekea maeneo mengi ya Africa,isipokuwa endapo muuzaji ameeleza wazi kwamba anaweza kuship to Africa.

Kwamaana hii, unaweza kuangalia kwenya account yako ya eBay kama hiyo bidhaa inaonekana imeshakuwa shipped, kama imeandikwa ipo shipped unaweza pia kucheki ni kampuni gani inayosafirisha huo mzigo na pia cheki tracking code ya huo mzigo wako, kisha uwasiliane na kampuni inayosafirisha kwa kuwapa tracking code kisha watakwambia huo mzigo ulipo.

Endapo huo mzigo haujakuwa shipped, au hakuna tracking code basi unaweza kumuuliza muuzaji atakwambia mzigo wako ulipo.

Endapo muuzaji hakupi ushirikiano wa kutosha,ndio unaweza kwenda stage ingine kwa kufungua malalamiko kwa eBay.

Inabidi ufahamu kwamba, kama ulifanya malipo kwa PayPal kuna uwezekano mkubwa sana kurudishiwa hela yako endapo utakuwa hujapata mzigo wako.ila kma umelipa kwa njia zingine huwa kuna kuwa na matatizo sana unapohitaji kurudishiwa hela.

Mkuu paypal najiungaje?
 
mie nilinunua touch screen kwa bei nafuu sana maana huku waswahili walinichaji bei ghali sana nikaona ninunue ebey, niliponunua kioo, nikapewa touch screen, kioo, na screen protector, plus screw driver ambapo shipping ni free...
 
Inabidi ufahamu kwamba, kama ulifanya malipo kwa PayPal kuna uwezekano mkubwa sana kurudishiwa hela yako endapo utakuwa hujapata mzigo wako.ila kma umelipa kwa njia zingine huwa kuna kuwa na matatizo sana unapohitaji kurudishiwa hela.
Katika hili la kurudisha pesa, wengine ninaowakubali ni Clickbank; endapo kuna reasonable grounds za wewe kudai pesa yako; jamaa hawana noma kabisa kama ilivyo kwa paypal.
 
Mimi nimeshafanya purchase mara tatu na zinafika japo huwa zinachelewa zaidi ya muda husika. Lakini zitafika na zikikosa unawasiliana na ebay kuna sehemu ya kuclaim
 
mimi nimeshafanya purchase mara tatu na zinafika japo huwa zinachelewa zaidi ya muda husika. Lakini zitafika na zikikosa unawasiliana na ebay kuna sehemu ya kuclaim

mkuu,huwa zinachukua muda gani tangu kununua hadi kukufikia?
 
Back
Top Bottom