Msaada kwa anaejua Vitu muhimu unapoenda kufatilia cheti cha kuzaliwa pamoja na gharama zake.

Super women 2

JF-Expert Member
Nov 16, 2016
5,165
6,531
Habari.
Kwa anaejua vitu muhimu vya kwenda navyo unapoenda kufatilia cheti cha kuzaliwa pamoja na gharama zake.

Kabla sijaenda niwe navyo.
Ahsanteni
 
Muhimu hii kama mama ako amefunga ndoa na baba ako nenda na cheti cha ndoa, na jina la mama la pili atatumia la baba ako, ila kama hawajafunga ndoa mama ako atumie jina la baba ake mzazi. Mfano.....baba ako akiwa ni Yohan kiroba basi mama ako atumie kiroba au Yohan lile lililopo kwenye cheti cha ndoa.
 
Nenda ofisi ya mkuu wa wilaya yako, ukiwa na picha mbili za passport za anayehitaji hicho cheti. Kama ni chini ya miaka10 ni buku4 tu. Zaidi ya hapo ni buku10.

Kama unataka kwa uharaka zaidi, niPM ili nikuserereshe. Japo kwa kamlungula kadogo.
Nakihita kwa haraka Zaidi
 
Muhimu hii kama mama ako amefunga ndoa na baba ako nenda na cheti cha ndoa, na jina la mama la pili atatumia la baba ako, ila kama hawajafunga ndoa mama ako atumie jina la baba ake mzazi. Mfano.....baba ako akiwa ni Yohan kiroba basi mama ako atumie kiroba au Yohan lile lililopo kwenye cheti cha ndoa.
Asante
Ila sijaelewa
 
Habari.
Kwa anaejua vitu muhimu vya kwenda navyo unapoenda kufatilia cheti cha kuzaliwa pamoja na gharama zake.

Kabla sijaenda niwe navyo.
Ahsanteni
kukushauri kwanza tujue umri wako kila umri una masharti yake mwaka 1-5, 10-40, 50-
 
umri mdogo wanapewa bure, kuanzia miaka 10 unalipia 10,000 ukiwa na umru kuanzia 50 hawakupi cheti cha kuazaliwa utakuwa unatumia Affidavit
 
Back
Top Bottom