Anayefahamu taratibu za kusajili NGO

Mar 1, 2011
20
1
Habari zenu.

Mimi ni kijana nina Stashahada ya kawaida (ordinary Diploma) Ya Ustawi wa Jamii pamoja na Uzoefu kidogo katika kufanya kazi za jamii nilioupata kabla ya kujiunga na Chuo kwa kufanya kazi za kujitolea katika mashirika tofauti.

Nina mapenzi makubwa na fani yangu lakini bahati mbaya ni kwamba Tangu nimemaliza Chuo Mwaka jana sijapata ajira na hivyo huwa nafanya kazi za muda mfupi pale ninapohitajika mahali fulani na hivyo najikuta natumia muda wangu bila kuwa na kazi rasmi.

Nikashauriana na familia yangu na kufikia Uamuzi wa kusajili Taasisi ambayo itafanya kazi za kijamii ambapo nitashiriki kwa kiasi kikubwa pamoja na kujenga uwezo kwa vijana waliopo vyuoni na wanaomaliza mafunzo kupata uzoefu.

Swali langu ni Je, kwa elimu yangu nina uwezo wa kuanzisha Taasisi na kupata Usajili?

Pia naomba mnielekeze taratibu za kufuata ili kusajili.

Nawasilisha.
 
Kwanza kwa kujua tu kwamba unaweza kuanzisha tayari ushaonyesha kupevuka. Anyway, elimu yako inakuruhusu kuanzisha taasisi kama hiyo. Jiulize walioanzisha WAMA wana elimu gani? Just go, go for it!
 
saf sana, wazo kama lako ni wachache sana wanaokuwa nalo, go ahead, kuhusu taratibu nakushauri ufuatilie hata katika NGOs uwaulize watakupa maelekezo mazuri zaidi ambayo yatakuwa na manufaaa zaid kwako
 
Hebu download hii document ...nafikiri itajibu maswali yako mengi!!
 

Attachments

  • 25_ngo_work_in_tanzania.pdf
    221.3 KB · Views: 1,144
Hongera sana kwa mpango wako ambao umeamua kuuweka kwenye utekelezaji.
usikate tamaa katika vikwazo utakavyokutana navyo kwani ndiyo mlango wako wa mafanikio.
 
Hebu download hii document ...nafikiri itajibu maswali yako mengi!!

Hapo Mkuu umeua kila kitu!!

Hebu huyo jamaa afuatilie jinsi hiyo doc inavyoelezea huo ndo mwongozo wa usajili wa NGOs. Wala hapaswi kuogopa ni wazo zuri ingawa awe amejiandaa kukabiliana na changamoto katika ukusanyaji raslimali (Fundraising). Kitu kikubwa ni kuwa mvumilivu asiwe na papara ya kutaka miradi mikubwa mikubwa!!
 
Ahsanteni,
Mawazo yenu yamenijenga na kunitia Moyo.
Naingia kwenye utekelezaji.
Naomba niwaombe tena, nitakapokwama nitarudi na msichoke kunisaidia.
 
Vizuri ndugu...kama upo dar es salaam nakushauli nenda katika ofisi usika ndiyo yatakuwa maelezo rasmi...sasa ni wapi? io moja...inategemea na NGO yako ipo katika uwanja gani?malengo yake?sehem yakufanyia shughuri zake?madhumuni yake? na vitu kama hivyo...nijuavyo mm zipo sehem kuu mbili chn ya sheria ya vyama ya jamhuri ya muungano wa tanzania...sehem ya kwanza ni wizara ya jinsia na watoto na sehem ya pili ni wizara ya mambo ya ndani hivyo fika uko kote utapata maelekezo zaidi...lakin mambo ya msingi kokote kati ya uko ni lazima muwe watu si chn ya kumi kama ya waanzilishi...muwe na katiba...muwe na viongozi watatu(mwenyekiti,katibu na muhasibu)...pesa ya kusajilia io asasi mfano;wizara ya mambo ya ndani nazani ni laki unusu na wizara io ya jinsia ni efu hamsin...so fanya fika uko...na ninyi kama waanzilishi muwe na minutes za vikao usika,aksante.
 
How Do i register an NGO? naomba msaada wa Taratibu za kusajili NGO,na inachukua muda gani kupata usajili kamili?

kuna vitendea kazi natarajia kutumia kutoka hapa nchini na baadhi kuagizia kutoka nje ya nchi ,JE kuna misamaha ya KODI ya aina gani ktk NGO.

asante in Advance
 
how do i register an ngo? Naomba msaada wa taratibu za kusajili ngo,na inachukua muda gani kupata usajili kamili?

Kuna vitendea kazi natarajia kutumia kutoka hapa nchini na baadhi kuagizia kutoka nje ya nchi ,je kuna misamaha ya kodi ya aina gani ktk ngo.

Asante in advance

mkuu inategemea na aina ya ngo, kwa sasa ngo za humu ndani ya nchi nazani zinasajiliwa maendeleo ya jamii , naz ile ambazo nikutoka nje ya nchi zinasajiliwa mambo ya ndani wizara.

Kwenye ishu ya misamaha, mkuu si rahisi kama unavyo fikilia kama huna mtu wa kukukingiz kifua, ni vigumu sana kupata msamaha na ukizingatia kwa sasa wameondoa baadhi ya misamaha ingawa sijajua ni ipi.

Kama una mtu yuko huko juu atakusaidia kwenye ishu ya msamaha wa kodi but kama huna sahau kuhusu misamaha.
 
How Do i register an NGO? naomba msaada wa Taratibu za kusajili NGO,na inachukua muda gani kupata usajili kamili?

kuna vitendea kazi natarajia kutumia kutoka hapa nchini na baadhi kuagizia kutoka nje ya nchi ,JE kuna misamaha ya KODI ya aina gani ktk NGO.

asante in Advance
sijakupata vizuri mkuu! unataka kuanzisha ngo ama kampuni ya biashara? fafanua please!!
 
sijakupata vizuri mkuu! unataka kuanzisha ngo ama kampuni ya biashara? fafanua please!!

Wewe nawe vipi?

Afafanue nini sasa wakati kitu kinajieleza wazi kabisa kwamba anataka kuanzisha na kusajili NGO? Wa-TZ bwana!! Kila kitu nyie mnaona ni mtego tu! Hata hilo nalo mpaka ufafanuzi?

Kuhusu usajili ndugu, nenda tu hapo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya mwone DAS wa hapo atakupa maelekezo yote maana taratibu za kusajili NGO zinaanzia kwa Mkuu wa Wilaya. Siyo kweli kwamba NGO za nje peke yake ndo zinasajiliwa Mambo ya ndani, hapana! Kama unataka NGO yako iwe ya ki-Taifa unapaswa kwenda kusajili Mambo ya Ndani (ofisi ya msajili wa vyama), lakini kama itafanya kazi kwenye wilaya moja tu basi usajili wako utafanyikia kwenye wilaya hiyo hiyo.
 
Kusajili Ngo mkuuni rahic sana jec nenda kwa mkuu wa wilaya kama ni ya wilaya i mean area of operation,kama ni mkoa nenda kwa mkuu wa mkoa pote hapo unapata fom unajaza then unalipia. Sijui cku hiz kama utaratibu umebadilika kipindi mm narejista ya kwetu na kwa kuwa inaoperate nchi nzima baada ya kupata fom na kujaza nlienda ofisi ya makam wa raisi pale ndo nilipeleka fom na katiba wakapitia na kurekebisha sehem nilizokosea then nikabind baada ya marekebisho afta one wik nkarudi kuchukua cheti, but cjui kama utaratibu umebadilika coz hiyo ilikuwa ni 2006.
 
Kusajili Ngo mkuuni rahic sana jec nenda kwa mkuu wa wilaya kama ni ya wilaya i mean area of operation,kama ni mkoa nenda kwa mkuu wa mkoa pote hapo unapata fom unajaza then unalipia. Sijui cku hiz kama utaratibu umebadilika kipindi mm narejista ya kwetu na kwa kuwa inaoperate nchi nzima baada ya kupata fom na kujaza nlienda ofisi ya makam wa raisi pale ndo nilipeleka fom na katiba wakapitia na kurekebisha sehem nilizokosea then nikabind baada ya marekebisho afta one wik nkarudi kuchukua cheti, but cjui kama utaratibu umebadilika coz hiyo ilikuwa ni 2006.
Asante sana,NGO inalenga good governance and public rights + education and Access to information.nadhani italenga zaidi kimkoa na kitaifa.
 
wewe nawe vipi?

Afafanue nini sasa wakati kitu kinajieleza wazi kabisa kwamba anataka kuanzisha na kusajili ngo? Wa-tz bwana!! Kila kitu nyie mnaona ni mtego tu! Hata hilo nalo mpaka ufafanuzi?

Kuhusu usajili ndugu, nenda tu hapo kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya mwone das wa hapo atakupa maelekezo yote maana taratibu za kusajili ngo zinaanzia kwa mkuu wa wilaya. Siyo kweli kwamba ngo za nje peke yake ndo zinasajiliwa mambo ya ndani, hapana! Kama unataka ngo yako iwe ya ki-taifa unapaswa kwenda kusajili mambo ya ndani (ofisi ya msajili wa vyama), lakini kama itafanya kazi kwenye wilaya moja tu basi usajili wako utafanyikia kwenye wilaya hiyo hiyo.

una uhakika? Hakuna ngo hata moja inayosajiriwa kwa mkuu wa wilaya au kwa mkuu wa mkoa. Hata kama ina operate kwenye wilaya moja.

Muwe mnaandika vitu ambavyo una uhakika navyo na si kukurupuka tu. Kwa kifupi mwanzoni ngo zote zilikuwa zinasajiriwa wizara ya mambo ya ndani lakini hivi baadae wameamua wapeleke swala hilo wizara ya maendeleo ya jamii. Na wizara ya mambo ya ndani inasajiri zile za kimataifa tu kutokana na mambo ya kiusalama.
 
Asante sana,NGO inalenga good governance and public rights + education and Access to information.nadhani italenga zaidi kimkoa na kitaifa.

MKUU KWA KIFUPI NI KWAMBA HAKUNA HATA SIKU MOJA AMBAPIO MKUU WA WILAYA ANASAJIRI NGO. WATU WANASHINDWA KUTOFAUTISHA VITU HIVI,
1. KUSAJIRI
2. KUJITAMBULISHA. ili uanze shughuli.
KWA MKUU WA WILAYA UNAENDA KUJITAMBULISHA NA UNASAJIRIWA KWENYE DAFUTARI LAKE KAMA MMOJA WA WATU WANO FANYA KAZI KWENYE ENO LAKE LA UTAWALA.
mkuu wa wilaya hasajiri NGO hata siku moja
 
Sure,ni kutambulisha NGO au kutambulisha mradi kama mtapenda
MKUU KWA KIFUPI NI KWAMBA HAKUNA HATA SIKU MOJA AMBAPIO MKUU WA WILAYA ANASAJIRI NGO. WATU WANASHINDWA KUTOFAUTISHA VITU HIVI, 1. KUSAJIRI 2. KUJITAMBULISHA. ili uanze shughuli.KWA MKUU WA WILAYA UNAENDA KUJITAMBULISHA NA UNASAJIRIWA KWENYE DAFUTARI LAKE KAMA MMOJA WA WATU WANO FANYA KAZI KWENYE ENO LAKE LA UTAWALA.mkuu wa wilaya hasajiri NGO hata siku moja
 
Back
Top Bottom