Msaada kunitajia movie ambazo sitakiwi kuangalia na watoto

Movie ni nyingi
Nani atakutajia hayo majina?.

chagua ulizowahi ona zinafaa ziweke pembeni ndio uwape watoto

binafsi nikiwa na muda mi ndo nachagua movie ikiwa na maadili mazuri naiweka folder la Family Movies

sipendi kutizama na familia kitu sikijui
Ni fedheha yakitokea ya ovyo..
Na vipi kama huna muda!!?
 
Movie zote wameweka miaka , unaweza kuangalia kama ni cd wataandika au kama ipo katika softcopy/digital pia wana rating na info za age
kuna zingine utakuta zimeanzia kati au zimetolewa zile intro...
 
Ule wa nyimbo nyimbo nimesahau heading yake
 
nilizoea kuishi mwenyewe..ila kwa sasa kuna watoto flan nitakuwa nao..so kwa vile mm ni mdau wa movie sana muda wote...naomba majina ya movie ambazo sitakiwi kuweka kwenye folder/flashdisk au dvd ,zile ambazo zina kwich kwich sana...maana hawa watoto wataharibika bure..
Wadau wanaweza kukusaidia, lakini, kuna changamoto pia. Watataja nyingi tu, lakini wanaweza wasitaje moja tu,ikakugharimu. njia nzuri ni wewe kufuatilia tahadhari zinazotolewa na walioandaa movie wenyewe. Mara nyingi huandikwa kwenye cover, wanaonesha miaka ya watazamaji ama wanatahadharisha kilichomo ili mtazamaji uchukue tahadhari. Kama upo siriaz na unajali, ukikosa taarifa, chukua jina/title ya movie yako kisha google upate maelezo yake. Ninadhani hutazami movie 100 kwa siku. Hivyo, kufuatilia movies moja ama mbili si mzigo.

Hongera kwa kujali watoto
 
Back
Top Bottom