Kuna ufa kwenye nyumba, fundi kaziba mara mbili na magunia hajafanikiwa

Mama Nehemiah

JF-Expert Member
Sep 9, 2018
241
433
Habari,

Naomba ushauri wa kitaalamu au kutoka kwa mdau aliyepitia hii changamoto ya ufa kwenye ukuta wa nyumba baada ya kumaliza ujenzi.

Fundi alijaribu mara mbili kutumia magunia kuziba lakini naona bado umejitokeza tena.

Huu ufa uzibweje ili usijitokeze tena?
 
Yani unaziba ufa kwa magunia?

Ujenzi ni taaluma ambayo watu wanaisotea miaka minne chuoni.

Ndio maana tunashauri mtumie wataalamu mnasema ni gharama mnaishia kwa mafundi wa mtaani. Sasa ona nyumba inaanguka wakati ungetumia hata milioni chache tu haya yasingetokea.

Siku nyingine hata kama huna hela tafuta mtaalamu muombe atembelee site yako akifika site hata kama hujampa hela akiona kasoro lazima akuambie.
 
Kuna Aina nyingi za nyufa,

- Kuna ufa unatokana na kusinyaa ama kukauka kwa material Kama plasta(shrinkage)

- Kuna ufa unaotokana na kujishindilia kwa udongo chini ya msingi(settlement)

-Kuna ufa unaotokana na matukio ya Asili Kama tetemeko la ardhi.

-Kuna ufa unaotokana na mabadiliko ya halijoto na kukosekana kwa expansion joint nk.

Ili kuziba ufa inabidi kutafiti Kwanza kujua chanzo chake na ndipo itakuwa rahisi kupata suluhisho la kudumu.
 
Yani unazoba ufa kwa magunia?

Ujenzi ni taaluma ambayo watu wanaisotea miaka minne chuoni....
Hawa si huwa wanasema wanataaluma wana gharama kubwa sijui watafanyiwa na mafundi kitu bora, sasa wapambane na hali yao ya kuziba ufa kwa magunia 😆 😆 😆 😆
Hapo hajaeleza huo ufa umetokea chini kwenye msingi ndio ukapanda juu au umeanzia juu kwenye ukuta kushuka chini..

Ufa hauzibwi kwa magunia bali huwa unauacha for a while ili kuona kama bado unadevelop au umeishia then ndio uchague njia ya kuuziba kwa namna unavyoonekana.

Kuna materials maalum za kuzibia na pia kuna kutumia reinforcement( wire mesh au nondo) kwa namna yake kulingana na hali inavyoonekena.
 
Habari,

Naomba ushauri wa kitaalamu au kutoka kwa mdau aliyepitia hii changamoto ya ufa kwenye ukuta wa nyumba baada ya kumaliza ujenzi....
Ufa mara nyingi unasababishwa na msingi kutokuwa imara.

Achunguze vizuri kuanzia msingi na asizibe kwa gunia atumie ndozo za kukatiza maaru Z, yaani zichore zedi kukatisha ufa ndipo apige plasta
 
Umejenga kwenye njia?Kama ulipojenga palikuwa ni niia ya muda mrefu basi huo ufo utaendelea kuwepo.Ila endelea kujaribu kutafuta namna ya kuutoa kwa kuanzia chini.
Njia inasababishaje ufa?
 
Back
Top Bottom