Msaada: Kuna Mume kapigwa na kitu kizito, naomba tuwashauri

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
24,139
56,600
Iko hivi hawa mke na mme wanaishi nchi tofauti ila hapo nyuma walipendana sana tena sana na.wana watoto kadhaa. Sasa mme akapata michepuko hapa Tanzania.

Na kuna mchepuko aliupenda sana sana kupita mingine. Mke wake anaishi London na watoto. Sasa kuna siku mme akampigia mkewe simu akimwambia kuwa hamtaki tena na huyo mke anaweza endelea na maisha yake.

Mke alichanganyikiwa ila mme alisimamia msimamo wake. Basi ikabidi mke aikubali hiyo situation.

Hapo ilikuwa katikati ya 2020.Mke alihitaji mtoto mwingine hivyo akaamua kwenda kupandikiza mimba ya sperm donner asiyejulikana.

Maisha haya jamani. Kumbuka mme alimuacha huyu mke kwa matusi na udhalilishaji ingawa hawakupeana talaka rasmi.

Bwana we 2022. Mme yakamfika hapa. Akaamua kwenda UK kumuona mke na watoto. Si akakuta mwanamke ana Mimbaaaaa.

Mwanaume alidata. Hapa ndo patamu ilibidi mwanaume ageuze kurudi Dar eti akimlaumu mke why kabeba mimba ya mtu mwingine?

Tuwasaidieje hawa jamani hasa mwanaume. Maana alimuacha mwenzake kwa matusi leo analia jamoooni.

Wana MMU najua mnabusara tuwasaidie hawa jamani kiushauri.
 
Jamaa akimaliza kulia arudi kwa mkewe akasilimie wowote asepe,
kama anampenda mkewe aombe maelezo ya hiyo mimba na mama akiridhia basi waendelee na ndoa.
Mke kasema kapandikiza hiyo mimba kwa kutumia sperms za unkown sperm donner. Shida hapa mme anamlaumu mke eti kamchanganyia damu. Kumbuka huyu mme alimuacha huyu mama kwa matusi. Ingawa hakukuwa na talaka rasmi.
 
Kwa mujibu wa maelezo

Inaonekana wewe ndyo unahtaji MSAADA Wala sio hao WATALAKA

JAPO HATUJUI UNATAKA MSAADA GANI
Msaada wasameheane na kuendelea na ndoa au watalikiane ?Maana mme anamlaumu mke kubeba mimba ya mwanaume mwingine nje ya ndoa.
 
Mke kasema kapandikiza hiyo mimba kwa kutumia sperms za unkown sperm donner. Shida hapa mme anamlaumu mke eti kamchanganyia damu. Kumbuka huyu mme alimuacha huyu mama kwa matusi. Ingawa hakukuwa na talaka rasmi.
Asilaumu kwasababu yeye ndiyo chanzo, kama hataki huyo mtoto wa maabara amuache mama wa watu hapo.
 
Wanaume wengi wanachepuka lakini wenye akili huwa wanawaheshimu sana wake zao pengine kuliko hata wanaume wasio na michepuko...

Mwanaume anayechepuka na kuleta mazereu, huyo hana upendo kwa mkewe na ni wa kupigwa chini...
Yaani hata mimi ninampa big up huyu dada. Maana kampiga kitu kizito sana huyu mme aliyejua kumuona choo dada wa watu. Unaambiwa dada anasema huyo mme alimuabuse sana kisaikolojia.Mme aliona mchepuko ndo unafaa. Sasa kabakia kutoa tuhuma eti mkewe kaamua kuzaa nje ya ndoa. Hii kali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom