Msaada: kuna fundi anadai nilipe 70k kwa ajili ya Oxygen sensor ya 1JZ engine, eti ndio bei yake hiyo?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,035
40,700
Nikadude kanacho fanana kama plug ya piki piki tu, kanafungwa kwenye manifold ya exhaust, eti ndio 70k, ni kweli eti?
 
Nenda kaulize dukani mwenyewe kama uko Dar nenda Ilala.pita duka moja moja uliza.Ila usinunue maana huijui wewe unaweza ukauziwa mbovu.pata bei halafu ndiyo ubishane na huyo fundi wako
Daah, nilikuwa na haraka sana, sikuwa hata na muda wa kuzunguka, baada ya kuona sijibiwi nililipa tu, ila imepona.
 
Bei inaweza fika 150,000 au 200,000 mpya kabisa. Yangu nilinunua 200,000 pale Toyota Tz Kkoo.

Ukimpa 70,000 anaenda kunyofoa kwenye gari iliokaa hapo garage muda mrefu anakuwekea wewe.
Duuh, aiseee! Kumbe ndio vinabei hivyo?!
 
Ndo bei zake mkuu 60K, 70K mpaka 120K, kwa used. Ukitaka mpya weka budgete ya kuanzia 220K na kuendelea
 
O2 sensor kwa 70k kama si bei mbaya kama bado ipo kwenye hali nzuri...

Kuna hivi vijitu vidogo dogo MAF sensor, O2 sensors hivi vidude vikizingua unaweza kuchukia gari.
Kwa MAF sensor nawashauri mwende pale liqui molly mikocheni nunua sensor cleaner inauzwa 30,000 ifanyei service ya kukaosha kila baada ya miezi 6 (recommend time), maana kakizingua ni balaa hata hizo O2 sensor zina namna ya kuzi clean, ingia tu youtube. Nime recommend uende mikocheni sababu hakuna mtu mwingine anauza hiyo cleaner zaidi ya hao liqui molly, gari yangu ilikuwa inaniwashia taa za malfunction za mara maf sensor mara O2 sensor zimesafisha sasa imetulia
images.jpeg
 
Kwa MAF sensor nawashauri mwende pale liqui molly mikocheni nunua sensor cleaner inauzwa 30,000 ifanyei service ya kukaosha kila baada ya miezi 6 (recommend time), maana kakizingua ni balaa hata hizo O2 sensor zina namna ya kuzi clean, ingia tu youtube. Nime recommend uende mikocheni sababu hakuna mtu mwingine anauza hiyo cleaner zaidi ya hao liqui molly, gari yangu ilikuwa inaniwashia taa za malfunction za mara maf sensor mara O2 sensor zimesafisha sasa imetuliaView attachment 2018265

Liquimoly niliwapigia last year wakasema hizi hawaingizi tena mkuu.

We umeinunua lini Last time?
 
Liquimoly niliwapigia last year wakasema hizi hawaingizi tena mkuu.

We umeinunua lini Last time?
Ni kweli hawakuwa nayo muda mrefu, ila wiki tatu zilizopita walinipigia simu wakanambia zimefika, na nliikuta kwa hiyo bei
 
Back
Top Bottom