Msaada: Kuku kuacha kuatamia Mayai

TIASSA

JF-Expert Member
Jun 17, 2014
2,894
3,423
Habari wakuu

Kuna kuku tulimpa Mayai 13 Atamie. Ila cha ajabu ametotoa vifaranga 2. Siku ya jumanne, leo siku ya ijumaa kwanzia asubuhi hataki Tena kutamia , shida ninini?

Je haya Mayai 11 yaliyobaki tunaweza kuhamishia kwa kuku wengine wanao tamia?
 
Shida ni kwmba kamalza kuatamia na watoto wanahitaji kutoka kwenda kusaka msosi na mama yao ila ukimuwekea kuku mwngn km hajaaribk yanawez kutotolewa
 
Hajaacha kutamia lakini ametotoa tayari,

Awamu ingine ukitaka kuku aendelee kutamia ikiwa ametotoa vifaranga vichache unatakiwa uvitoe vifaranga umwache kuku na mayai tu,

Hayo maya yaliyobakia yanaweza kutotolewa na kuku mwingine kama yalitagwa na kuku aliyepandwa na jogoo utayaamisha kwa kuku mwingine isipite masaa masaa 5 bila kuamisha
 
Mkuu jaribu kutumia pia mbinu ya incubator. Kuna watu wanafanya biashara ya kutotolesha mayai kwa bei nafuu(300 au 400) kwa yai moja ,japo utaingia gharama kwenye kuwakuza
 
Habari wakuu

Kuna kuku tulimpa Mayai 13 Atamie. Ila cha ajabu ametotoa vifaranga 2. Siku ya jumanne, leo siku ya ijumaa kwanzia asubuhi hataki Tena kutamia , shida ninini?

Je haya Mayai 11 yaliyobaki tunaweza kuhamishia kwa kuku wengine wanao tamia?
Huyo kuku mle tu mbona hasara sasa
 
Naunga mkono hoja ila inabidi awe na egg tester maana watotoleshaji nao ni wasanii unaweza ukapeleka mayai Mia wakakwambia mayai hamsini yote ni mabovu
Mkuu jaribu kutumia pia mbinu ya incubator. Kuna watu wanafanya biashara ya kutotolesha mayai kwa bei nafuu(300 au 400) kwa yai moja ,japo utaingia gharama kwenye kuwakuza
 
Naunga mkono hoja ila inabidi awe na egg tester maana watotoleshaji nao ni wasanii unaweza ukapeleka mayai Mia wakakwambia mayai hamsini yote ni mabovu
Na hapa pia ndio msingi wa tatizo lake ulipoanzia.kuku aliyetotoleshwa kwa incubator hawezi akalalia mayai akatotoa with efficiency
 
Back
Top Bottom