Msaada kujulishwa kiasi cha fedha kinachohitajika wakati wa maandalizi ya kujifungua

gluckkcom

JF-Expert Member
Jun 21, 2019
361
786
HABARI ZENU WANA JF

Kwa Majina Naitwa Tyron goodluck

Mwanzoni mwa Mwaka huu 25/1/ 2019
kuna msichana nilimpatia Ujauzito

Hivyo Nime mlea na sasa yuko ktk hatua zake za mwisho tayr kwa kwenda kujifungua

Shida yangu Ni kwamba Nilikua Naomba kufahamishwa kiasi cha fedha ambacho Uwa kina itajika pale mjamzito anapo kwenda kujifungua Hospital

Nje ya vifaa vile muhimu kama:
Vitenge ,Beseni, Dawa za kuzuia damu ,Groves ,na Bomba za sindano

Kwa Anaye fahamu naomba Msaada Juu ya hili
 
mkuu unampa mimba mwanamke kabla hujajua kuandika?? angalia usije ukaandika jina la mtoto ndivyo sivyo badala ya Ryan ukaandika Nyan.

garama za kujifungua hutofautiana na hosptal pia garama hutofautiana kama atajifungua kwa operation au njia ya kawaida.

kwa ushauri mpeleke kwenye hosptal za serekali kama uwezo ni mdogo kama unajiweza mpeleke private.
 
Hongera kwa kulea mimba hadi hatua hiyo.
Kiwango cha pesa kinategemea na wewe ulipo, aina ya hospitali utakayompeleka lakini pia aina ya Daktari, specialist au gp. Ni kati ya 150000 hadi mill 2. Inaweza zidi endapo kutatokea complications.

Ni muhimu sana wewe kuhakikisha kwamba unazijua dalili za hatari na kuwa tayari kumpeleka hospitali mara tu zinapojitokeza.

Kila la kheri.
 
Uzur

Uzur ni kwmba umenielewa na ndy maana umenijib uwaga clembi mwandiko humu mimi Ila nashkuru kwa ushauri wako ubarikiwe
 
Hongera kwa kulea mimba hadi hatua hiyo.
Kiwango cha pesa kinategemea na wewe ulipo, aina ya hospitali utakayompeleka lakini pia aina ya Daktari, specialist au gp. Ni kati ya 150000 hadi mill 2. Inaweza zidi endapo kutatokea complications.

Ni muhimu sana wewe kuhakikisha kwamba unazijua dalili za hatari na kuwa tayari kumpeleka hospitali mara tu zinapojitokeza.

Kila la kheri.
Ahsante sana god bless you
 
Usiogope sana baba kijacho. Kama upo kijijini zahanati zetu zile hata elfu sabini humalizi mchakato unakuwa umekamilika. Muhimu tuombe dua tu mama ajifungue salama . Hongera kwa kufikia hatua hiyo mkuu
 
Ahsante
 
Kwa mahitaji uliyokwisha andaa kama utajifungua government inaweza isizidi elf20 kama atajifungua salama bila operation so waweza andaa laki 2 kama dharura endapo utaenda hospital hizi za umma.
 
Hongera baharia...
Nakupa uzoefu kidogo kwa sisi ambao tumeshalea wazazi...

(a) Maandalizi ya awali...
....nepi
....sabuni ya unga kama ndoo moja ndogo..
....sabuni ya mche kama miche 15 hivi.
.....Nguo za mtoto zinazomfaa mtoto mchanga
.....Blanket zuri la mtoto na mama yake.
.....Andaa chumba maalumu cha kumtunzia mzazi...
....kama umezoea kuzurura, anza kujizoesha kukaa nyumbani au kuwahi nyumbani unapotoka kazini.
.....Hakikisha nyumba ina chakula cha kutosha...si kila siku kwenda kwa mangi kupima robo kilo.

(b)Wakati anaenda kujifungua .
....kama una gari, liwe na mafuta na kama huna gari andaa hela ya kukodi bajaji au taxi...si boda boda.
.....Andaa kama laki 5 kwani huwezi kujua atajifungua kwa upasuajiau kawaida...akijifungua kawaida utabakiwa na hela nyingi zitakusaidia baadae.
....andaeni kanga safi za kutosha, besini jipya na ndoo mya, pamba ya kutosha na vjngine utaelekezwa na nesi.

(c) Maandalizi baada ya kujifungua.
....Gunia mbili za mkaa...hizi ni za kupikia supu ya mzazi na si vinginevyo.
....Jaza mtungi wa gesi kama unao.
.....andaa kama laki 4na nusu...hii ni maalumu kwa supu ya mzazi mfululizo kwa kipindi kisichopungua miezi miwili....usimlishe mzazi ugali na matembele tu kwa miezi miwili ya kwanza..
....kama hauna bima ya matibabu, andaa laki moja ya dharura iwepo...mama au mtoto anaweza kupata homa ghafla.
.....Kama ni mlevi, acha pombe kipindi hiki..
.....Jiandae kufua nguo za mtoto na mama kama hauna uwezo wa dada wa kazi...mama hataruhusiwa kushika shika maji ya baridi miezi miwili ya mwanzo.
.....jiandae kisaikolojia kutokupendwa na mkeo, mapenzi yatahamia kwa mtoto..
Jiandae kukesha miezi mitatu ya mwanzo, watoto wachanga huwa wanalala mchana usiku wanakesha na mara nyingi wanalia..
....Jiandae kupkkea wageni wa mfululizo wanaokuja kumsalimia mtoto na mzazi...uwe na hela za kuwakarimu.

Mchanganuo niliokupa unaweza kuutumia kukisia bajeti ya kumuandalia mzazi.. roughly iatagonga milioni 1 mpak 1.5 ili uweze kumlea mzazi vyema bila stress na hapo mzazi atamaliza uzazi akiwa amenawiri sana..
We mwenyewe utampenda...

Kulea mzazi si kazi ndogo, ndiyo maana vivulana vingi vikishatia mimba vinakimbia kusikojulikana.

Nakutakia maandalizi mema
 
If you can't afford condom u can't afford kids I believe dic quotes is really men Ila ntapambana kwa uwezo wa mungu shukran sanaa mkuu
 
Duu, vijana hawataoa
 
Mkuu andaa fedha isiyopungua 3.5 hadi 4 mill. Wanaokushauri hawajui. Kujifungua ni nusu kifo so inawezatokea ukatakiwa operation. Pia vitu vidogovidogo baada ya mtoto kuja duniani hivi huchukua hela ndefu
 
duuh!!!! 4mil ngoja nijaribu kupambana ila sizani kama ntazipata maana urefu wa kamba yangu ni mfupi sana kuzifikia kwa muda huu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom