Msaada kujua anuani (ajira portal)

Ngao ya Sponji

JF-Expert Member
Jul 26, 2018
341
541
Wakuu natumaini mpo Salama:

Moja Kwa Moja niende Kwenye mada husika, kama Kichwa kinavyojieleza;

Tovuti ya Serikali ya Ajira haiweki wazi anuani ya Mamlaka au Shirika lililotangaza Nafasi za kazi Wala haitoi taarifa kwamba barua Ziandikwe kwenda kwa nani Hivyo kuweka ugumu kujua anuani ya sehemu husika.

Mara nyingi huwa najaribu kuingia katika tovuti zao lakini sio zote zinaweka Anuani na nyingine Huwa hazina Tovuti kabisa.

Mfano mzuri ni Mamlaka ya Maji safi na Mazingira Nzega (NZUWASA) amabayo wametangaza Nafasi ya Ajira lakini haijulikani Barua inaandikwa kwenda kwa nani na Anuani Yao ni ipi, Tafadhali naomba mwenye uelewa juu ya Hili anisaidie. nawakilisha
 
Niaje mkuu?
Anuani huwa ni moja tu ipo mwishoni mwa kila tangazo la kazi kutoka utumishi. Nimekuwekea hapa;

Secretary,
Presidents Office,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
University of Dodoma (UDOM), Utumishi Building/Asha Rose Migiro Buildings - Dodoma.
 
Niaje mkuu?
Anuani huwa ni moja tu ipo mwishoni mwa kila tangazo la kazi kutoka utumishi. Nimekuwekea hapa;

Secretary,
Presidents Office,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
University of Dodoma (UDOM), Utumishi Building/Asha Rose Migiro Buildings - Dodoma.
Shukrani sana Mkuu Kwa Muongozo, Kwa maana hiyo ni kwamba Ajira zote za Serikali nitatumia Anuani Moja tu si ndio?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom