Msaada kuhusu utendaji kazi wa figo na ini kuna mahusiano Gani?

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,372
54,909
Naomba kujuzwa ushirikiano uliopo kati ya hivi vitu viwili FIGO ,INI.

Na pale inapotokea kushindwa kufanya kazi kipi kinaathirika zaidi ya kingine?

Msaada tafadhali.
 
Swali lako kwa kweli ni vigumu kulijibu kiurahisi. Ingawa upo uhusiano katika utendaji wa kawaida kimwili (physiologically), ni vigumu kujibu nini kitaathirika zaidi bila ya kufahamu sababu ya kuharibika huko. Vitu mbalimbali vinaharibu kiungo kimoja zaidi ya kingine. Labda ungefafanua zaidi tatizo ulilo nalo na sababu ya swali lako ungeweza kusaidiwa kiurahisi.
 
kuna mgonjwa kapata tatizo la figo na katika kupewa matibabu imegundulika kuwa hata ini halifanyi kazi na hii imenifanya kuuliza juu ya mahusiano ya vitu hv viwil na ni kipi huwa kinatoa msaada zaidi ya kingine kwenye mwili?
 
Ni tatizo gani alilokuwa nalo kwenye figo? Je kabla hajaanza matibabu ya figo ini lilikuwa halijaathirika? Ni tatizo gani walilokikuta kwenye ini? Majibu ya haya maswali yatasaidia kujua kama matatizo mawili yanahusiana au la.
 
figo zilishindwa kufanya kazi kwa maana hiyo wakadai na ini nalo pia halifanyi kazi
 
Inawezekana. Ila kwa kweli ni vigumu kukuelezea maana sina majibu ya maswali mengi muhimu juu ya mtiririko wa ugonjwa aliokuwa nao mgonjwa na dalili zake.

Kwa mfano tu, kati ya kazi ya ini ni kutengeneza aina fulani ya protein inayoitwa "albumin" ambayo husaidia damu na maji kukaa katika mishipa ya damu na kuboresha mzunguko wa damu na virutubisho sehemu mbalimbali za mwili ikiwa ni pamoja na figo. Sasa mtu anaweza akawa na tatizo la ini, tatizo hilo likasababisha upungufu wa albumin, maji yakapungua toka katika mishipa ya damu, ikasababisha upungufu wa mzunguko wa damu sehemu mbalimbali za mwili ikiwa ni pamoja na figo, na mtu akapata tatizo la figo (renal failure).

Huo hapo juu ni mfano mdogo tu, na hauna maana ya kwamba hilo ni tatizo alilokuwa nalo mgonjwa. Kwa kweli ningependa kusaidia wadau hapa kuelewa hili, lakini kwa maelezo uliyotoa hayajitoshelezi na nisingependa kukisia tu maana matatizo yanayoweza kusababisha hilo yapo mengi.

Nimetumia mfano huo hapo juu kwa ajili tu ya kuonyesha uhusiano unaoweza kuwepo kati ya viungo hivi viwili na sina maana kwamba hilo ndiyo tatizo alilo nalo mgonjwa. Naomba nieleweke hivyo.
 
Back
Top Bottom