Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

ComputersDAR

JF-Expert Member
Jan 21, 2013
213
240
Habari zenu Wana JF,

Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.

Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?

Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?

Asanteni kwa msaada.
 
JKT kupoteza muda tu na kutesa vijana wetu wameshachoka na mitihani hata hawajapumzika waend tena kulima huko na kukimbiakimbia, hao wa kujitolea tu hawawaajiri wanazeekea makambini na kurejea mitaani.
Binafsi sioni faida ya kwenda huko, labda kama una ndoto na jeshi unaweza kwenda ukapata connection otherwise piga chini, chuo utaenda tu.
 
Nakubaliana na wewe aslimia 200 lakini nini madhara ya kukwepa huu ujinga? Wanatafuta nguvu kazi ya bure kwa kisingizio cha uzalendo hilo ni wazi kabisa.
 
Watoto wa sasa hivi ni lonyolonyo sana, nashauri mbunge litunge sheria iwe ni lazima kwenda JKT.

Kiukweli mnatusikitisha sana Toto lipo high school bado linasimamiwa na wazazi hawezi hata kujisimamia.

Kizazi hiki bila kukipitisha jeshini tunaandaa msiba mkubwa kwa Taifa.
Wangefanya JKT iwe mandatory kwa wanaume tu kama nchi nyingi za Ulaya. Kwa wanawake iwe hiyari. Sababu huko kuna changamoto nyingi ambazo siyo rafiki kwa wasichana.
 
Watoto wa sasa hivi ni lonyolonyo sana, nashauri mbunge litunge sheria iwe ni lazima kwenda JKT.

Kiukweli mnatusikitisha sana Toto lipo high school bado linasimamiwa na wazazi hawezi hata kujisimamia.

Kizazi hiki bila kukipitisha jeshini tunaandaa msiba mkubwa kwa Taifa.
Acha zama za ushamba na ujima.

JKT haina maana sababu hakuna zana za kufundishia watu.

Huko zaidi ya kulima hakuna la maana.

Wakitaka watu waende watangaze kuwa lazima upite huko mwaka ndo upate mkopo na kazi
 
Kama kijana aliyemaliza A level anaweza kukwepa kadhia ya kuripoti JKT bila kukumbana na serious consequences kuhusu future yake sidhani kuna mtu angeripoti kambini. Ndiyo hoja yangu ya msingi.
Kupita JKT haimaniishi utapata faida zozote sema kutokana na umasikini wa pesa na fikra wazazi huwapeleka watoto wao jkt ili angalau wabaatishe nafasi za majeshi Kama ulinzi , police ,jwtz nk .

Na sio kila Mtu anayekwend jkt atapata hizo nafasi za majeshi.
 
Nakubaliana na wewe aslimia 200 lakini nini madhara ya kukwepa huu ujinga? Wanatafuta nguvu kazi ya bure kwa kisingizio cha uzalendo hilo ni wazi kabisa.
KAZI ipo
IMG-20230525-WA0045.jpg
 
JKT wangekuwa hawachoki kila mara kuwaelimisha Vijana sababu, faida na madhara ya kujiiunga au kukataa kujiunga na taasisi yao. Lakini naona kipaumbele chao ni kutangaza orodha tu kila mwaka kwa wanafunzi wanaotakiwa kuripoti kambini bila ya kufafanua kwanini, kwa sheria zipi, manufaa yapi na madhara yapi wakiripoti au wasiporipoti kambini. Kuweka tu orodha ya Wanafunzi na vitu wanavyotakiwa kuwa navyo wakati wana ripoti kambini bila ya kuwafahamisha kwa nini waripoti ni dharau.
 
Back
Top Bottom