Msaada kuhusu: Tufundishane Ujasiriamali

Fatmas

Member
Aug 28, 2008
16
0
Jamani naomba contact za mjasirimali mwenye pizza store au bakery naomba kusoma kutoka kwake.
Pia naomba fundi wa umeme atakaenisaidia kuconvert mashine zinazotumia umeme wa Marekani ziweze kutumika Tanzania.
Natanguliza shukrani
 
Nakushuri uoneshe hamasa ya ndani(THE DESIRE of what u want) kwanza ili uweze kuwashawishi watu ni namna gani uko makini na kweli ukisaidiwa utafanyia kazi msaada na ushauri utakaopewa hapa.
Mi nimesoma post uliyoituma kwenye "Tufundishane Ujasiriamali" hapo tu ilionesha kuwa ulitakiwa kuligudua swala la kuanzisha thread yako mwenyewe, na hata uliposhauriwa kufanya hivyo ulichofanya ni ku-copy & paste kile kile ulichokiandika awali, kama hiyo haitoshi ukaa mua kutumia heading ile ile ya post ya "Tufundishane Ujasiriamali" sana sana ulichokifanya ni kuongezea maneno mawili tena ambayo haoneshi USHAWISHI. Ndio maana watu wengi wameshasoma post yako na kukaa kimya kwakuwa hawaelewi waanzie wapi na hawajui fikra na mtazamo wako kwasababu jinsi unavyojieleza ndio watu wanavyo kuweka katika fungu fulani.
Hebu jaribu kushughulisha ubongo kidogo na utaona jinsi tunavyoweza kufanya
mambo makubwa kama tukiamini katika uwezo tulionao.
Kila mtu anaweza kufanya chochote anachotaka kama ataamini anaweza.
Don't limit your self that you can't do this or that.
Think think think.
 
Jamani naomba contact za mjasirimali mwenye pizza store au bakery naomba kusoma kutoka kwake.
Pia naomba fundi wa umeme atakaenisaidia kuconvert mashine zinazotumia umeme wa Marekani ziweze kutumika Tanzania.
Natanguliza shukrani
Ndugu yangu Fatma ningependa nikupe mwanga kidogo kuhusu ujasiriamali, ni kwamba kwanza ilipaswa utambuwe kuwa hakuna njia ya mkato katika biashara ya aina yoyote ile.( kutokana na maelezo yako una mawazo ya kuleta mitambo toka Marekani na kisha kupata mtaalamu akufunze kuandaa pizza, tayari unaanza Mkahawa wako) Haiko rahisi kihivo na kwa mfano hai ni sawa na kijana anayetaka kuingiza gari highway kabla ya kulijua gari lenyewe linaendeshwaje? gea ndio ipi?, accelerator, breki, indiketa nk. Umenielewa?
Ujasiriamali ni safari ndefu na ningekushauri kabla ya kuanza hii safari yako, hakikisha una uelewa wa baadhi ya mambo haya muhimu ambayo inapaswa kuyazingatia kwanza kabla ya kujikita kwenye hii venture yako. (it is critical you understand this!)
Kwanza lazima uwe na clear vision (mwanga tosha) wa nini unataka kufanya, umetaja Bakery na Pizza hii inaonyesha huna clear vision ya biashara ipi umeamua uifanye.
Pili lazima uwe na passion, determination and motivation (sijui niite nguvu, ari na kuthubutu) kwani utakutana na vikwazo vingi tu na bila ya mambo haya matatu utaachia njiani na kuishia kupata hasara
Elimu ya kina (in-depth knowledge) ya hio biashara, fanya feasibility study kati ya matarajio ya mapato ukilinganisha na gharama, eneo unalotaka kufanyia hii biashara jee utapata wateja wa kutosha? Gharama ya kodi, wafanyakazi? Upatikanaji wa umeme, maji,na jinsi ya kukabiliana na power cut/water supply shortage, upatikanaji wa vitendea kazi (mfano unga, matunda,viungo, nyama nk. Usalama (security) Competitors Jee sehemu uliyokuwepo kuna migahawa mingapi ya aina hii ama wewe utaboresha huduma kivipi kuwashinda washindani wako?
Ukiridhika na hatua zote hizi na kuwa na confidence ndipo uingie hatua ya pili ya kutafuta mtu ama chuo kujifunza mapishi ya pizza na jinsi ya kuendesha mkahawa na mwisho ndio uanzishe hio biashara, venginevyo utaishia na hasara tu ndugu yangu.
 
Ahsanteni sana muliochangia. Mungu awabariki. Ni kweli "Kila mtu anaweza kufanya chochote anachotaka kama ataamini anaweza."
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom