Msaada kuhusu solar

Hamis Zmc

Member
Aug 25, 2016
45
26
nipo mkoa wa Mara, nina shida moja, natumia sunder solar watt 100, bettry ya sunder N 100, INVETER ya Solar Max watt 150, pia nina flt tv inch 32 yenye watt 50, 110-240v,, nina blender watt 350, subfer seapeano v 220-2240, na taa 3 watt5, shida ninkwamba moto unaisha haraka sana,nikiwasha tv tu inveter inasoma v100, tv inazma na pia bettry ikiwa full nikiwasha tv tu charge controller inasoma 25% kisha inveter inafel na tv inazima, msaada hapo nifanyeje
 
Mkuu hapo kwenye chanzo chako cha nishati ni kidogo kutokana na matumizi yako. Kwanza Solar panel ya watts 100 haiwezi kuichaji vizuri hiyo battery ya N100,Inatakiwa solar panel iwe na watts kubwa kuliko battery kwa hapo kwako Solar panel inabidi iwe hata ya 120watts ili iweze kuicharge vizuri battery yako.

Pia ktk matumizi yako bado yapo juu hata km Ukiongeza panel bado itakua ngumu kupata hicho unachokihitaji. Kwa ushauri hapo ungepata vifaa ambavyo vina option ya kutumia a.c na d.c ingekua bora zaidi maana zipo tv zinazotumia volt 12 kwa 110-220V a.c pia hizo sub woofer zipo za aina hiyo,hiyo angalau itakusaidia maana inverter hasa hizo za dukani zinawahi kuichosha sana battery ungepata ambayo imesukwa na fundi wa mkono ingekua bora zaidi na pia ungekua unaitumia pale ambapo kuna ulazima wa kuitumia hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nipo mkoa wa Mara, nina shida moja, natumia sunder solar watt 100, bettry ya sunder N 100, INVETER ya Solar Max watt 150, pia nina flt tv inch 32 yenye watt 50, 110-240v,, nina blender watt 350, subfer seapeano v 220-2240, na taa 3 watt5, shida ninkwamba moto unaisha haraka sana,nikiwasha tv tu inveter inasoma v100, tv inazma na pia bettry ikiwa full nikiwasha tv tu charge controller inasoma 25% kisha inveter inafel na tv inazima, msaada hapo nifanyeje
Ulipata msaada?
 
Nunua dc TV na solar TV zipo nyingi tu dukan lakin pia blenda za DC kibao tu una umeme mwingi sana kwa vyombo vya DC na una umeme mdogo sana kwa vyombo vya AC ambavyo nilazima uwe na inverter alafu solar ya watt 100 ni ndogo sana kwa battery la N100 ikiwezekana ongezea solar watt 50
Binafs Nina solar watt 50 na watt 20 jumla 70 na battery n 70 hapo kwa haraka beti kubwa na sola ndogo kubalance ilibid watt 100 kwa n 70 sio mbaya lakini Nina umeme mwing sababu TV yangu ni ya dc nch 15 sabufa a border DC balubu nnazo ka 7 ivi nachaj simu Nina redio ya kawaida ya vote 6 anatumia Bi Mkubwa nimeunga na DC adapter ya vote 5kushusha vote ya beti kutoka vote 12 to v 5 lakini bado umeme nnao mwingi alafu matumiz madogo na balubu ni watt 2 na 1 nnazo TV naangalia mpaka nachoka Mimi sasa nikalale na ninawasha total sabufa na TV then naunga AUX ya saut from TV to sabufa hapa wengi wanajua ni ivyo√√√√√√√
 
Binafsi nakushauli hivi kama vifaa vyote vinatumia sola, (DC V) achana na inveta , invet baadhi huitaji moto mwingi, kuna zile in veta zenye transifoma du zile zinaitaji moto mwingi, kuna sehemu tulikuwa tunatumia sola ikifika saa 12 tunazima kila kitu inabaki taa tu, lkn jirani yetu alikuwa anachaji cm na kupiga muziki kama kawa,tukaenda kumuhoji akasema ameacha kutumia inveta ndio tukajua kuuumbe chanzo ni hiki nasi tukaitia mvunguni mwa kitanda .
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom