Msaada kuhusu Salary Loan

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,093
1,894
Wakuu salama,

Nilikuwa na ajira ya kudumu serikalini, nikakopeshwa mkopo mkubwa na bank ya biashara kama salary loan.

Ikiwa makato yote yanafanyika kila mwezi kutoka kwenye mshahara wangu.

Nikapata safari ya masomo nje ya nchi, mwajiri hakukubaliana na mimi kunipa ruhusa japo mwanzo niliambiwa haina shida nitapata ruhusu, hivyo niliacha maombi yangu ya ruhusa na kuanza safari.

Nikiwa safarini nje ya nchi, mwajiri kakataa ruhusa na kufuta ajira yangu.

Bank wanakuja juu ni muda sasa hawapati makato yao, moja ya makubaliano ilikuwa kuchukua mafao yangu kufidia mkopo, lakini sasa wanatishia kutangaza magazetini na kuchukua hatua zaidi.

Hakuna sehemu nimepinga kulipa, lakini pia nimewaomba muda ili niendelee kulipa kila mwezi nikiwa nje ya nchi, wakaniambia wananipa siku 14 tu nitafute kila jinsi kulipa, siku hizo zimeisha jana na hakuna jinsi nimeweza kutuma makato yaliyochelewa, nimewajulisha hali hiyo pia.

Je, kuna namna gani hapa kitaalamu/ kisheria naweza weka suala hili vizuri, maana vitisho vinazidi na nia yangu ya kulipa deni ni njema.

Msaada wadau katika hili, wale vijana washule na ambao bado hamjawa na uzoefu wa mambo haya, tupisheni kidogo tujifunze kwa wazoefu wa mambo haya.

Ahsante sana, nawakilisha.
 
Hakuna sheria ya kukwepa deni.

Rejea terms za makubaliano yenu uone cha kufanya ikibidi uwaombe kufanya re-scheduling ya marejesho japo hiyo inaweza kuongeza riba pia.
 
Umefanya kosa kubwa mno kwenda masomoni bila ruhusa ya mwajiri. Najua hata kibali cha kusafiri kwenda nje ya nchi hukuomba!

Je umepata ufadhili wa masomo au unajilipia? Kama una ufadhili, kwanini hutumii hiyo pesa ya stipend kulipa deni la bank?
 
Back
Top Bottom