Msaada kuhusu proceedures za mimba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kuhusu proceedures za mimba

Discussion in 'JF Doctor' started by Penny, Jun 17, 2009.

 1. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Za leo wandugu wapendwa,

  Jamani napenda kutoa shukrani kwa wana JF wote wa umoja wenu katika maswa mbalimbali. Leo ningependa kupewa all the proceedures(vyakula, uvaaji n.k) za mama mjamzito kuanzia mwezi wa kwanza mpaka wa mwisho. Mwenye huo ujauzito ni mimi mwenyewe baada ya kupata mafunzo mazuri kupitia hapa JF. Asanteni sana matunda yenu yameonekana. Karibuni sana wandugu katika hili, asanteni.
   
 2. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Penny hongera sana kwa kuwa mama mtarajiwa, Hiyo ni hatua muhimu sana kwenye maisha yako na ni vizuri kwa kuwa inaonesha umejiandaa kimwili na kiakili. Ni vizuri pia kama mwenzi wako pia akawa karibu na wewe kipindi hiki muhimu cha maisha yenu kama wazazi watarajiwa.
  Kwa kawaida kipindi cha ujauzito kimegawanywa katika makundi matatu ya takriban miezi mitatu kila kundi. Miezi mitatu ya kwanza ni kipindi muhimu kuliko vyote kwa sababu ndo viungo vya mtoto vinaundwa na vipindi vingine ni ukuaji wa kawaida. Utumiaji wa dawa na vyakula vyenye kemikali ambazo zinaathiri mgawanyiko wa chembechembe za mwili ( cell division) haitakiwi kabisa kwa sababu zaweza kuharibu maumbile ya kiumbe au hata kuharibu mimba. Ni vizuri kupata maelekezo ya daktari kabla ya kutumia aina yoyote ya dawa.
  Kwa upande wa vyakula ni vizuri kutumia chakula bora ( balanced diet) ni muhimu kwa ukuajia wa mtoto na kwa afya yako pia.
  Vyakula vinavyoongeza damu ni muhimu sana matunda na mboga za majani, ni muhimu pia kunywa maji kwa wingi.
  Ukifikisha miezi mitano ya ujauzito anza clinic ya wajawazito kwenye hospitali au kituo karibu nawe.
  mambo muhimu ya kuzingatia:
  Damu au maji kutoka ukeni
  mtoto kupunguza kucheza
  maumivu makali ya tumbo
  Homa
  Kuvimba miguu
  Kuongezeka uzito kwa kasi sana ( > 5kg per month)
  etc..........
  Uwaone wataalamu mapema.
  Otherwise kwa niaba ya wana JF nakutakia miezi tisa yenye utulivu na kila la kheri kwa kipindi chote cha ujauzito wako.
  regards
   
 3. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Penny

  Hongera kwa kuwa Mama Mtarajiwa.
   
 4. S

  Sweet Mary New Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Penny, Hongera sana mama.
   
 5. R

  REOLASTON Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Penny hongera sana. uashauri aliokupa M/Jadi ni mzuri na cha kuongezea ule samaki kwa wingi na usifanye kazi nzito
   
 6. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,820
  Likes Received: 2,535
  Trophy Points: 280
  Asante mganga wa jadi kwa ushauri mzuri.

  Kwa kuongezea tu fanya mazoezi ya kutembea kila siku hii itasaidia kupunguza uvimbe wa miguu na kuwa na nguvu mungu akikujalia kufika siku husika ya kupush.

  Be good woman hapo ndo sehemu pa kumshukuru mungu kwa kuweza kuhakikishiwa uzima wa kizazi chako.Kama mnyaji wa bia tumia pia Guness bia walau chupa moja kwa wiki inasaidia sana kuongeza damu kwa wingi ila ina alcohol content 7.5.Nazungumzia hivyo kwa kuwa mke wangu naye amepitia hatua hizo na sasa tuna mtoto wa kiume ambaye alizaliwa akiwa na kg 5. one week ago.
  God bless you Penny.
   
 7. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,820
  Likes Received: 2,535
  Trophy Points: 280

  Kutofanya kazi nzito inategemeana na tabia za mimba.

  Reolaston.Kila mama mjamzito huwa anabehave tofauti kuna mwingine kuanzia day one mpaka mwisho ni mchapa kazi hivyo inategemeana na aina ya kazi uisemayo kama ni ya kutumia akili sana au uzito wa ukubwa (kgs tani)

  Mke wangu kuanzia day one mpaka mwisho alikuwa akifanya kazi na hakupa bed rest hata moja na wala hajawahi kutapika na uchungu umeaupatia kazini hivyo inategemana kwakweli siyo uniform kwa kila mtu.

  Nawasilisha.
   
 8. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jamani nashukuruni sana tena sana. Simnaujua tena ukiwa tena mbali na wazazi inabidi mtu uulize mambo kwa wazoefu. Yani kwa kweli nimejisikia kama niko nyumbani kweli. Umoja wa JF uendelee hivi hivi jamani. Nitayafanyia kazi maushauri yenu ya nguvu. Mungu awabarikini sana tena sana.
   
 9. S

  Sumji R I P

  #9
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Penny, ushauri wa mzee wa jadi ni sahihi kabisa! ila nataka kuongezea jambo kidogo maana namimi nimemaliza ngwe hii miezi sita iliyopita. Kuhusu kuhudhuria kriniki, siku hizi kama huna tatizo lolote wanashauri uhudhurie kriniki mara nne au tano tu. Inashauriwa katika kila kundi kama alivyotanabaisha Mganga wa jadi angalu mara moja. kwahiyo nashauri angalau uanze Kriniki miezi mitatu (Kundi la kwanza) baada ya hapo daktari ndo atakwambia urudi lini, kufuatana na utakavyoamabiwa. Lakini pia chagua kriniki nzuri sio ili mradi kriniki. Na pia angalia hakikisha kila kipimo kilichooneshwa katika kadi ya kriniki unakifuatilia na kujua kinamaanisha nini. Wakati mwingine nesi anaweza akakupima BP akairekodi bila kukuambia kama iko juu, chini au kawaida na vipimo vingine kama mkojo, kiasi cha damu nk ni muhimu kupima katika kila hudhurio la kriniki. Nakutakia kila laheri Mungu akulinde wewe na mtoto ili mwisho wa yote tabasamu lako lizidi hilo ulilonalo sasa.
   
 10. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Wana JF hapo juu wamekupa ushauri mzuri wa ujumla kuhusu matunzo ya mimba, ushauri zaidi utaupata kiliniki kulingana hali yako, jitahidi kuuliza maswali bila kuogopa, kwa kuwa ushauri mwingine utakuwa specific kwako kulingana na watakavyokupima. Pia hakikisha vipimo vifuatavyo vimefanyika- Uwingi wa damu (Hb), kundi la damu na rizazi (BG&Rh), Kaswende (VDRL) na HIV. KUMBUKA HAKUNA MIMBA ILIYO SALAMA MPAKA UMEJIFUNGUA SALAMA, Nakutakia safari njema kuelekea LABOUR ROOM.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tafadhali usiache kufanya mapenzi mnaweza kuendelea hata siku moja kabla ya kujifungua, hii huweka strong bond kati ya mtoto na babayake tangia akiwa tumboni! Pia hii husaidia kujifungua salama!!! Mengine wajuzi wameisha yaweka hadharani!
   
 12. dmaujanja1

  dmaujanja1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  KWANZA-Penny hongera sana dada Mungu akupiganie vya kutosha ktk kipindi chote cha ujauzito wako Siha njema akujaalie na Shari akuepushie.
  PILI-Mganga wa Jadi vyakula vya kuongeza damu nivip namboa na mifano plz.
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu naona kimesahaulika:
  Penny unatakiwa as much as possible uwe na mawazo mazuri kila mara, acha kukasirika ovyo na kisirani pale inapowezekana kama mimba haikusumbui. Kuna vijitabia vya watoto tunakuwa tumewapatia sis wenyewe katika process ya kubeba mimba.Uwe na raha na pia kumsemesha mwano aliye tumboni - hasa mweleze mnavyompenda n akumtarajia!

  Sijui mwenzio mliyoshirikiana katika uumbaji naye anashiriki vipi katika safari yako kubeba tumbo miezi tisa.Na yeye mpe nafasi - ashike tumbo lako, asikilize mateke pale mtoto atakavyoanza kucheza tumboni, akusindikize clinic, mpe card yako ya clinic asome na mweleweshe kinachoendelea.

  Kuzaa kwa mwanaume siyo kupanda mbegu tu, afuatilie hadi mazao yanapotokea.
  Good luck and enjoy the process of motherhood.
   
 14. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Vyakula vinavyoongeza damu ni pamoja na mboga za majani zilizopikwa vizuri, matunda, nyama (red meat), Mayai na samaki pia unywaji wa maji na juice fresh ni muhimu.
   
 15. N

  Nameless- Member

  #15
  Jun 23, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera mdada Penny! Kama alivyosema WOS kuhusu kujiepusha na hasira, hiyo ni moja ya sehemu ya usafi (moyoni), na kuwa na mawazo mazuri muda wote. Utaifurahia mimba na mtoto wako. Kwa kuongezea, kumbuka kuwa msafi na mtanashati mwilini pia. Kama ni mvaaji suruali, zipo zinazomfaa mama mjamzito, na vitop vinavyofaa kabisa. Kila la heri!
   
 16. D

  Dina JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  WoS, ndugu yangu, umpate huyo wa kukusindikiza..manake akina baba...whyuuuuu...kazi ipo.
   
 17. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2015
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,860
  Likes Received: 1,134
  Trophy Points: 280
  Hujapata mtoto wa pili Akili Unazo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...