msaada kuhusu nafasi za kazi za vodacom

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,730
519
wakuu naombeni msaada wenu, kuna nafasi za vodacom watu walifanya interview mwezi uliopita,
tatizo langu ni kuwa kuna kijana wangu ninaishi nae, na alimaliza chuo 011, mda wote hajabahatika kupata ajira, kwa bahati nzuri kapata hizo nafasi, kwa mujibu wa yeye alipomaliza training, walishindwana na vodacom kwenye mkataba, anasema wanalipa kidogo mnoo, alafu masharti ya mkataba ni magumu, hivyo kaamua kuacha kazi,
naomba mwenye uelewa kuhusu huo mkataba anisaidie ni kweli mkataba una masharti magumu!
na je mshahara wanalipa kiasi gani?
 
ni kweli mshara ni mdogo sana yaani ni kama 240000 kwa mwezi na hapo anatakiwa ajigharamie kuanzia nouli,hela ya kula na mengineyo ila mi najua hawa ni kwa customer care na wako chini ya ero link,ero link ni kma madalali wa kazi kwani wao wanachukua tenda voda alafu mshahara wako ndo mnagawana nao na huyo kijana alijua hilo ndo maana akaamua kuachana nao maana ni kama unyonyaji kweli
 
Wewe ndio mhusika mwenyewe! unasaidiwa halafu unaringa kufanya kazi, kafanye kazi acha mambo ya k.ke!
 
Amefanya uamuzi wa busara sana,angepoteza muda wake na energy yake bure..Voda pale boss mpya aliyekuja kawaambia erolink wafanyakazi wote customer care watakuwa wanalipwa laki mbili na ushee km wakishindwa waache..mbaya zaidi ata wale wa zaman wanarudishwa kwenye mishahara mipya na kuna watu wa siku nyingi walifikisha hadi laki tano sasa watu wanaangaika kukimbia..kifupi hapafai na serikali sijui inafumbia macho kwa nini aya mambo au sababu kampuni ni ya Rostam
 
acha uswahili.kama ujui kitu nyamaza...sasa mshahara wa 240000 si bora utafute biashara ambayo ataingiza faida ata buku10 kwa siku kwa mwezi anakua na laki 3..kuliko kukesha na kusimamiwa kama mharifu masaa yote alafu unapewa laki2,chakula juu yako usafiri juu yako sometime atatoka shift ya usiku achukue bajaj hakuna daladala ata kama njaa sio kiivo.
 
ni kweli mshara ni mdogo sana yaani ni kama 240000 kwa mwezi na hapo anatakiwa ajigharamie kuanzia nouli,hela ya kula na mengineyo ila mi najua hawa ni kwa customer care na wako chini ya ero link,ero link ni kma madalali wa kazi kwani wao wanachukua tenda voda alafu mshahara wako ndo mnagawana nao na huyo kijana alijua hilo ndo maana akaamua kuachana nao maana ni kama unyonyaji kweli
asante mkuu, nayeye aliomba customer care
 
Pole sana mi pia kuna jamaa angu alianza kazi pia lakini nashangaa kama wik hv imepita ananiambia japo sina kazi ndugu yangu lakini siwezi kuendelea na hawa jamaa sasa sijajua hawa jamaa wa Erolink na voda wanamatatizo gani sababu yeye kazi alipata kupitia Erolink! Inawezekana kuna matatizo huko!
 
Amefanya uamuzi wa busara sana,angepoteza muda wake na energy yake bure..Voda pale boss mpya aliyekuja kawaambia erolink wafanyakazi wote customer care watakuwa wanalipwa laki mbili na ushee km wakishindwa waache..mbaya zaidi ata wale wa zaman wanarudishwa kwenye mishahara mipya na kuna watu wa siku nyingi walifikisha hadi laki tano sasa watu wanaangaika kukimbia..kifupi hapafai na serikali sijui inafumbia macho kwa nini aya mambo au sababu kampuni ni ya Rostam

afadhali kidogo nnaanza kumuelewa, bora atulize akili awekeze nguvu nyingi kutafuta kazi nzuri
 
fanyeni kazi acheni kuchaguchagua
sasa nanyie mnasapoti huhu ujinga! ulaya watu wanabeba box na wanaishi
sembuse customer care!
 
Huyo dogo hajakosea. Apige dili nyingine.Laki 2 na then bila hata marupurupu mengine. Ni bora akafate Kanga na kuku wa kienyeji mikoani then aje kuwauza mjini faida ipo.
 
wakati sina kazi nilikuwa natamani hata kufanya kazi bure bila kulipwa kwani kitendo cha experience kilikuwa kinanipa shida sana, hivyo namshauri jamaa aongeze experience siyo sawa na kukaa mtaani.
 
fanyeni kazi acheni kuchaguchagua
sasa nanyie mnasapoti huhu ujinga! ulaya watu wanabeba box na wanaishi
sembuse customer care!

We unaejiita Obama wa bogo comment zako atakayekuelewa ni wale ambao hawana akili tu, machizi wenzio, haijalishi iwe customer care au kubeba mabox cha msingi hapa ni maslahi, ulaya wanabeba mabox lakini wanapata kipato kizuri, hawa vadacom wanatufanya watumwa kwenye nchi yetu na serikali ina inachekelea tu, nchi nyingine hawathubutu kufanya huo upuuzi,
 
  • Thanks
Reactions: kui
fanyeni kazi acheni kuchaguchagua
sasa nanyie mnasapoti huhu ujinga! ulaya watu wanabeba box na wanaishi
sembuse customer care!

Kinacholalamikiwa ni maslahi na sio kazi, hata kama ni kubeba box kama kunalipa mbona poa sana tu
 
tatizo ni malipo mkuu sio aina ya kazi, kama pesa inasoma tutaafanya tu, we huoni mbeba box ulaya akirudi anatumia hela, wewe hapo customer care si utakuwa na madeni kila siku? issue ni pesa kaka sio aina ya kazi, umenisoma??????
 
sure,issue ni pesa bhana,.240,000/= dah ndogo sana
 
Kinacholalamikiwa ni maslahi na sio kazi, hata kama ni kubeba box kama kunalipa mbona poa sana tu

naunga mkono hoja, hilo ndio la msingi, ama kubeba box au kuzibua choo, mradi maslahi tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom