msaada kuhusu kutoa talaka

Evmem

Member
Oct 20, 2010
95
12
I was married to a Tanzanian man who has been mistreating me so much and insulting me and even beating me up and chasing me out of his home, I decide to leave and I want to divorce him. I was married in RC church , talaka itakuaje sasa? siitaji ushauri penzi langu kwake hamna tena, please assist:sad:
 
Ndoa ya namna hiyo inaweza kuvunjwa na mahakama, baada ya kuridhika na madai utayopeleka. Ila si rahisi, labda kwa vile details zaidi unazo wewe, labda zitasaidia.

Kwa upande mwingine, si vizuri kuamua tu kuwa hutaki ushauri. Hata kama umewahi kupewa ushauri huko nyuma ambao hukukusaidia, haina maana hata leo huwezi kupata ushauri utakaosaidia kurudisha ndoa yako katika hali ya amani na furaha. Je mafundisho uliyopewa kanisani wakati unafunga ndoa uliyazingatia?
 
Kila kitu namwachia, all I need is Amani tu basi na kurudi kwake sio rahisi kwa vile hata penze langu kwake hamna
 
I was married to a Tanzanian man who has been mistreating me so much and insulting me and even beating me up and chasing me out of his home, I decide to leave and I want to divorce him. I was married in RC church , talaka itakuaje sasa? siitaji ushauri penzi langu kwake hamna tena, please assist:sad:

kwa wakristo if you can prove beyond any doubt hapo talaka itatoke or stage fumanizi
 
What do you mean 'i was married to a Tanzania man'?? au una ujumbe kwamba wanaume wa kitanzania ndivyo walivyo hawafai au Wewe si Mtanzania ndio maana unauliza ushauri maswala ya divorce Tanzania yanakuwaje? Kama nyote ni Watanzania unaelewa fika wapi pa kuanzia ni mahakamani na si kwingineko. Kama ndoa yako ilifungiwa Tanzania kama mwanaume ni mzungu mhindi mwarabu mtanzania sheria ni ile ile..
 
Sister Pakawa sio wote wanaojua pa kuanzia ikiwa wanataka talaka whether ni Watanzania au raia wa nchi nyengine.

Wewe muelimishe tu.
 
I was married to a Tanzanian man who has been mistreating me so much and insulting me and even beating me up and chasing me out of his home, I decide to leave and I want to divorce him. I was married in RC church , talaka itakuaje sasa? siitaji ushauri penzi langu kwake hamna tena, please assist:sad:

Alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe! (Mk. 10:9) Kama unamwacha kwa sababu ni mzinzi sawa lakini kwa habari nyinginezo utamfanya kuwa mzinzi akioa mke mwingine na wewe ukiolewa utakuwa unazini na huyo mume mpya! (Mt. 5:32.)
 
kaka/dada hayo maandiko tu lakini hayaheshimiwi. Kunja ndoa inawezekana, Cha kufanya Huyu dada aende kwa padri amweleze kilichomsibu na pia aende kwa ustawi wa jamii, kabla ya mahakama, mahakama inataka uthibitisho kwa aliyefungisha ndoa kwa maelezo ya kueleweka yaliyotolewa both mume na mke, pia ustawi wa jamii unatia mkono wake kisha ndo aende mahakamani kwa kuvunja ndoa rasmi.

Ugumu uko kwa mapadre hawa ni ma Concevative acha kabisa kukubali ni issue, ukipata bahati akakubali basi mahakamani inakuwa issue ndogo, inatakiwa uwe na uwezo wa kukonvice mapadre other wise usubili kifo kiwatenganishe.

mapadre wana msimamo sijapata kuona. wagumu sana.

Hafu dada kama huhitaji kitu kwake amani tu, hakuna haja ya mahakama si usikae naye tu kila mmoja aishi kivyake kama anataka kuoa aoe au roho itakuuma, mi naona hata bila mahakama unaweza kumpiga chini, ukachukua hamsini zako na zake. Kwani atakushitaki au bado unampenda.

Hafu kwa nini huwa anakupiga? Hivi mtu anaweza kupigwa hivi hivi tu from no where? na wewe utakuwa mtata kiasi fulani.
 
Mungu anafurahia ndoa kama mafuta yatiririkayo kwenye ndevu za haruni. Ila shetani anafanya juu chini kuhakikisha ndoa nyingi zinavunjika.
Inawezekana dada hao washauri wako wa mwanzo pia ni washabiki wa kutaka kuvunja ndoa yako. Chunga ndoa yako, au ukishindwa kabisa tafuta washauri makini uwaeleze matatizo yako.
 
Ni kweli mkuu,talaka ni halali imchukizayo mwenyezi mungu, hivyo tujizuie kutoa ushauri kufanikisha talaka kwani tutakuwa tunamchukiza mwenyezi mungu
 
I was married to a Tanzanian man who has been mistreating me so much and insulting me and even beating me up and chasing me out of his home, I decide to leave and I want to divorce him. I was married in RC church , talaka itakuaje sasa? siitaji ushauri penzi langu kwake hamna tena, please assist:sad:pa kuanzia ni ofisi ya ustawi wa jamii wilayani kwako na uwaeleze kuwa unataka talaka kutoka kwa mume wako na utatakiwa kueleza kama mna watoto ama vipi na namna wanavyoishi kwa wakati uo na unafikiri wataishije baada ya talaka kisha watakupa barua ya kwendea baraza la ushauri la ndoa la mahali uliko, mtaitwa na ikishindikana kusuluhishwa pale mtapewa barua kwenda mahakamani amabako nako ikithibitika kuwa ndoa yenu imeishavunjika kiasi cha kutoweza kurekebishika, hati ya talaka itatolewa. hiyo ni kwa mujibu wa sheria za tanzania, sijui kuhusu sheria za nchi zingine

Alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe! (Mk. 10:9) Kama unamwacha kwa sababu ni mzinzi sawa lakini kwa habari nyinginezo utamfanya kuwa mzinzi akioa mke mwingine na wewe ukiolewa utakuwa unazini na huyo mume mpya! (Mt. 5:32.)

mkuu hapo penye bold panahusika. ndoa ya kuogopa kutenganisha ni ile iliyounganishwa na Mungu tu na si vinginevyo. siku izi watu wanaunganishwa na mambo mengi sana kama pesa, uchawi, uongo nk. hapo huwezi kusema wameunganishwa na Mungu

Ni kweli mkuu,talaka ni halali imchukizayo mwenyezi mungu, hivyo tujizuie kutoa ushauri kufanikisha talaka kwani tutakuwa tunamchukiza mwenyezi mungu

tujizuie tusijizuie, talaka ni kitu kingine kabisa kuliko mnavyoifikiria. talaka hutolewa pale amabapo imethibitika kuwa ndoa husika "IMEVUNJIKA KIASI CHA KUTOWEZA KUREKEBISHIKA" kwa iyo yalaka haivunji ndoa, ndoa huvunjwa na nyinyi wenyewe na talaka ni uthibitisho wa kiserikali tu kwa ndoa iliyovunjika

kulingana na maelezo ya dada ni kuwa hakuna tena ndoa kati yao na kama kuna lolote juu ya kuvunjika ndoa yao ni juu ao wenyewe, sisi tunashauri namana ya kurejesha amani kama alivyoomba mwenyewe na tunashauri kwa lengo hilo. kumbukeni kuwa kuna ndoa amabazo zikishavunjika ndio wanadoa wanapata amani. si watu wote wamejaaliwa kuwa wanadoa.

mimi niliomba na kupata talaka miaka miwili iliyopita na sasa nina amani tele na furaha ya maisha na niko katika nafasi nzuri zaidi ya kiakili na kiuchumi kutunza mtalaka wangu, watoto wangu na ndugu wengine wanaonitegemea. utashangaa kuwa hadi leo mimi ndiye namtunza mtalaka wangu kwa kila kitu na ninafanya hivyo kwa upendo kabisa kwani nilimuacha kutokana na jeuri na vitimbwi vyake na mimi nilikuwa bado nampenda
 
mkuu hapo penye bold panahusika. ndoa ya kuogopa kutenganisha ni ile iliyounganishwa na Mungu tu na si vinginevyo. siku izi watu wanaunganishwa na mambo mengi sana kama pesa, uchawi, uongo nk. hapo huwezi kusema wameunganishwa na Mungu

Huyo mtoa hoja amedai kwamba amefunga ndoa katika Kanisa la RC kwa hiyo nikadhani kwamba amemshirikisha Mungu! Sijui wewe mambo ya pesa, uchawi, uongo, nk unayatoa wapi?
 
ninavyojua mimi, watu hawaunganishwi kanisani/misikitini/ofisi za ma-DC. na kuna watu wanafika kufunga ndoa rasmi makanisani, misikitini/ serikalini wakiwa tayari na watoto na huwezi kuwaita wale watoto kuwa ni wa nje ya ndoa. pale kanisani/misikitini/kwa DC huwa wanaenda kukamilisha tu taratibu za madhehebu yao na/au serikali, na kimsingi wanaenda kukamilisha "sherehe" lakini huwa ndoa imeishafungwa siku nyingi sana pale walipoahididiana/kukubaliana kwa moyo wa dhati kuwa watajenga familia moja na kama ni ahadi walshazitoa zamani sana hata kabla wazazi hawajashirikishwa. sasa at those earlier stages ndiko hayo niliyotaja yanaweza ku-influence uamuzi na ahadi ya ndoa.

nafikiri saa tuko ukurasa mmoja mkuu
 
kaka/dada hayo maandiko tu lakini hayaheshimiwi. Kunja ndoa inawezekana, Cha kufanya Huyu dada aende kwa padri amweleze kilichomsibu na pia aende kwa ustawi wa jamii, kabla ya mahakama, mahakama inataka uthibitisho kwa aliyefungisha ndoa kwa maelezo ya kueleweka yaliyotolewa both mume na mke, pia ustawi wa jamii unatia mkono wake kisha ndo aende mahakamani kwa kuvunja ndoa rasmi.

Ugumu uko kwa mapadre hawa ni ma Concevative acha kabisa kukubali ni issue, ukipata bahati akakubali basi mahakamani inakuwa issue ndogo, inatakiwa uwe na uwezo wa kukonvice mapadre other wise usubili kifo kiwatenganishe.

mapadre wana msimamo sijapata kuona. wagumu sana.

Hafu dada kama huhitaji kitu kwake amani tu, hakuna haja ya mahakama si usikae naye tu kila mmoja aishi kivyake kama anataka kuoa aoe au roho itakuuma, mi naona hata bila mahakama unaweza kumpiga chini, ukachukua hamsini zako na zake. Kwani atakushitaki au bado unampenda.

Hafu kwa nini huwa anakupiga? Hivi mtu anaweza kupigwa hivi hivi tu from no where? na wewe utakuwa mtata kiasi fulani.

we casava usipotoshe mamabo. fuatilia utaratibu nimeuweka vizuri katika post # 12 hapo juu uone procedures za kupata talaka. hao mapadri wala si ishu, wanaweza kukubali au wakatae lakini hawana say kuzuia talaka ninayoijua mimi. ni kwamba baraza la usuluhishi likona ni vyema na busara linaweza kuwarudisha kanisani kwenu au hata kwenye vikao vya kiukoo kabla halijatoa uamuzi wake (kuwapa barua ya kupeleka mahakamani). na hii si lazima, itattegemea aina ya mgogoro wenu na hatua mlizopitia, wakiona labda wazee wanaweza kuwapatanisha watawarudisha huko, wakiona dini zenu zinanafasi watawapeleka huko. mkikataa, watatoa recommendations zenu bila kurudishwa huko nyuma.

mimi nilikataa kurudishwa kanisani na nilipewa barua ya mahakamani moja kwa moja.
 
Binadamu wote wanamapungufu yao, usdhani ukiondoka kwake ndo huko kwingine ni kuzuri, why dont you solve it kuliko kukimbia? mie sijui bana, utamkumbuka tu, yaani wazazi wetu wangefanya hivyo mbona leo wote tungekua watoto wasio na wazazi
 
jamani ninyi mliobahatika kupata wenza wema mshukuruni mungu badala ya kubeza. jamani kuna ndoa zina mateso acha. mimi mwenyewe tumetengana na mke wangu. niulikuwa silali, mara aanze kuimba, mara muziki kwenye cm, akianza kutukana. imagine masaa 12 ucku hupati muda wa kulala, yeye mchana analala, mimi kibaruani. we dada tengana naye. kutengana pia ni proof ya mahakma kutoa talaka
 
Pole sana, hapo ni mahakamani tu, jamaa yangu alikuwa na shida kama yako mahakama ikamaliza hiyo kitu fasta, nenda kafaili kesi haraka.
 
mi nadhani hapa akipatikana mwanasheria anayeijua vizuri sheria ya ndoa na namna ndoa inavyoweza kuvunjika itatusaidia wote, kuliko kila mtu kuongea anavyodhani ni sahihi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom