Msaada kuhusu hili suala la mbwa kuua mwizi na mmiliki wa mbwa kufunguliwa shtaka la mauaji

Wewe usiyejua Mbwa na kimbembe chao ni bora ukaufunga mdomo tu. Kuna jomba mmoja Mbezi ya chini kule alikuwa ni shamba boy na alikuwa anawahudumia hao ma GS, hiyo siku akawafungulia halafu akatoka kwenda kutafuta kiroba. Wakati wa kurudi akakuta geti limeshafungwa na hakumtaarifu mtu alipokuwa anatoka. Akaona hapa heri aruke fensi kuingia ndani, ile kutua tu chini wale mbwa walikuwa watatu wakamtaitisha! Bwana bwana, waliondoka na Kende za yule jamaa, kupiga kelele wanakuja kuangalia ni nani kumbe shamba boy, wakamuwahisha hosp akakatikia njiani.
Duh kwa hiyo hao mbwa walimsahau hadi mfanyakazi wa hapo,kama ni hvyo hawana masihara
 
Usichofahamu hata raia wa kawaida kama unamiliki bunduki halafu ukaua muhalifu lazima ushtakiwe kwanza, hata wale walinzi wa kampuni binafsi ambao wamepewa bunduki wakiua lazima washitakiwe
Naomba elimu zaidi hapo,hizo bunduki wanazomiliki hao raia wa kawaida kazi yake ni nini sasa?
 
Katika yote unaposhambuliwa na mbwa akiwa mmoja basi jitahidi upate upenyo umpige kabali ya kuuwa,unahakikisha hajizungulushi akachomoa kichwa,yaani unahakikisha hisia zako unazipeleka kwenye shingo na mkono wako,unabamiza kikweli kweli ,ukiliweza hilo basi dakika mbili nyingi unafanikiwa kumzima. na unapovamia nyumba yenye mbwa vaa mnguo magumu na maarapu rapu yalio luzi yaani xxxxl.
Sio unavaa tight ka unaenda kucheza singeli.
xxxxl duh sipati picha hilo bwanga sijui lipoje
 
Mbwa peke yake sio kazi rahisi kumuua binadamu mtu mzima
Zipo species wanaoshambulia mpaka kuua...ila sijui sheria zetu zikoje juu ya ufugaji wa aina fulani ya Mbwa.

Kuna nchi haziruhusu Mtu binafsi kufuga aina fulani ya Mbwa kwani anaweza hata kuchoropoka kwa bahati mbaya akaenda kuua Mtu asiye na hatia....na hao wakishaanza kushambulia Mtu au hata Mbwa mwingine hawaachii hata wewe mmiliki uende uongee kila unachokijua.
 
Pole kwa huyo Muhusika ingawa hapo ni maelezo ya upande mmoja tu, ni ngumu sana kutoa uamuzi kwa kumsikiliza Mtu wa upande mmoja...vipi kama ni Mtu aliyeamua kumfungulia Mbwa baada ya kutoelewana wakiwa kwenye mazungumzo hapo hapo ndani?. huenda Polisi wana taarifa tofauti na anazotoa huyo Mlalamikaji.
 
Sikia ndugu io kesi lazima ifanyiwe uchunguz kwanza umejuaje km ni mwiz pili nn kilimuuq maana mbwa pekee yke not easy binadamu ana uwezo wa kuua mbwa ni minutes km upo strong
Binadamu huyo wa kuua mbwa peke yake Labda Rambo na Arnold swatziniger,,

Tena kwenye movie.
 
Ni American Pitbull au American Broiler? Navyojua broiler ni aina ya kuku wa kisasa maalum kwaajili ya nyama (Wanakua kwa haraka na wakubwa).

Anyway, turudi kwenye mada husika.

Sheria inasema unapoweka ulinzi wa kutumia "WANYAMA WAKALI au UMEME" ni lazima uweke kibao kwa nje kwenye geti la kuingilia nyumbani au ukutani kinachotoa "TAHADHARI/ONYO (Warning Sign)" juu ya uwepo wa hivo vitu.

Mfano, TAHADHARI KUNA MBWA WAKALI" au "TAHADHARI KUNA FENCE YA UMEME".

Ukifanya hivo ukaweka tahadhari nje ya uzio wako, basi atakaeingia ndani kwako iwe mwizi au mtu unaemfahamu au jirani tu, akapata madhara, unakua hauhusiki kwa lolote litakalo mtokea. Anakua amekaidi tahadhari uliompa.

Ila usipofanya kuweka tahadhari, basi mtu yoyote akidhurika utawajibika kwa tatizo lolote litakalo tokea kutokana na hivo vitu vyako vya ulinzi.

NOTE: Nia na madhumuni ya kuwepo kwa sheria, ni kwaajili ya kulinda haki za watu (hata kama mtu ni mwizi au muuwaji ila kuna sheria zinazolinda utu wake).
Duu!! Kwahyo mwizi asipojuwa ndani kwangu kuna mbwa.,,
Akaruka ukuta,,
Aking'atwa kosa ni langu?

Sheria mbovu kabisa!!
 
Utetezi wake ni pamoja na uwepo wa onyo/warning getini kwamba mbwa wakali.

Pili, "tress passer tresspasses at his own peril". Hiyo ni legal principle kwamba ukiingia kwa mtu kinyume na taratibu ni shauri yako. Likupatalo usilaumu.

Kama ulishaona wenye fence wire. Kuna vibao vipo pale vimeandikwa "danger, electric fence, Kv...". Vile havipo bahati mbaya ni kuutaarifu umma kwamba jamaa anajilinda na umeme kwa hiyo kaa chonjo
 
Ukute upelelezi ulionesha mwizi aliuawa pia baada ya kushambuliwa na binadamu pia. Sema akipata mwanasheria makini kesi ni nyepesi sana hiyo.
Mkuu Huyo jamaa hapo kwenye avatar yako,jamaa lilikuwa kichwa sana.nimemsahau jina somebody kinyondo.
 
Ni American Pitbull au American Broiler? Navyojua broiler ni aina ya kuku wa kisasa maalum kwaajili ya nyama (Wanakua kwa haraka na wakubwa).

Anyway, turudi kwenye mada husika.

Sheria inasema unapoweka ulinzi wa kutumia "WANYAMA WAKALI au UMEME" ni lazima uweke kibao kwa nje kwenye geti la kuingilia nyumbani au ukutani kinachotoa "TAHADHARI/ONYO (Warning Sign)" juu ya uwepo wa hivo vitu.

Mfano, TAHADHARI KUNA MBWA WAKALI" au "TAHADHARI KUNA FENCE YA UMEME".

Ukifanya hivo ukaweka tahadhari nje ya uzio wako, basi atakaeingia ndani kwako iwe mwizi au mtu unaemfahamu au jirani tu, akapata madhara, unakua hauhusiki kwa lolote litakalo mtokea. Anakua amekaidi tahadhari uliompa.

Ila usipofanya kuweka tahadhari, basi mtu yoyote akidhurika utawajibika kwa tatizo lolote litakalo tokea kutokana na hivo vitu vyako vya ulinzi.

NOTE: Nia na madhumuni ya kuwepo kwa sheria, ni kwaajili ya kulinda haki za watu (hata kama mtu ni mwizi au muuwaji ila kuna sheria zinazolinda utu wake).
Umedadavua vizuri sana,
 
Katika yote unaposhambuliwa na mbwa akiwa mmoja basi jitahidi upate upenyo umpige kabali ya kuuwa,unahakikisha hajizungulushi akachomoa kichwa,yaani unahakikisha hisia zako unazipeleka kwenye shingo na mkono wako,unabamiza kikweli kweli ,ukiliweza hilo basi dakika mbili nyingi unafanikiwa kumzima. na unapovamia nyumba yenye mbwa vaa mnguo magumu na maarapu rapu yalio luzi yaani xxxxl.
Sio unavaa tight ka unaenda kucheza singeli.
Hizi train ndiyo unawapa kikosi chako sio
 
Back
Top Bottom