Msaada kuhusu hili suala la mbwa kuua mwizi na mmiliki wa mbwa kufunguliwa shtaka la mauaji

Hapa hata mimi kama ningekuwa polisi ningekuwa na mashaka. Inahitajika uchanguzi ufanyike kabla ya maelezo ya mwenye nyumba kukubaliwa.
1. Hakusikia kelele za mbwa wakati wanamshambulia?
2. Huyo aliyeuawa hakupiga kelele wakati anashambuliwa?
3. Kama aliuawa usiku ni kwanini alisubiri mpaka kesho yake ndiyo akatoe ripoti?
4. Majirani walisikia kelele? Ni nini maelezo yao?
Kuna mashaka mengi sana. Moyo wangu unakataa kuwa huyu ''kibaka'' aliingia kwenye uzio na mbwa wakamuua.
5. Hakuna uwezekano ''kibaka'' aliua nje ya uzio na mwili wake kuingizwa ndani?
6. Kuna uhakika gani alikuwa mwizi?
all is possible mkuu! na inawezekana kabisa huyu mtu kuuwawa na mbwa hawo
 
Ni American Pitbull au American Broiler? Navyojua broiler ni aina ya kuku wa kisasa maalum kwaajili ya nyama (Wanakua kwa haraka na wakubwa).

Anyway, turudi kwenye mada husika.

Sheria inasema unapoweka ulinzi wa kutumia "WANYAMA WAKALI au UMEME" ni lazima uweke kibao kwa nje kwenye geti la kuingilia nyumbani au ukutani kinachotoa "TAHADHARI/ONYO (Warning Sign)" juu ya uwepo wa hivo vitu.

Mfano, TAHADHARI KUNA MBWA WAKALI" au "TAHADHARI KUNA FENCE YA UMEME".

Ukifanya hivo ukaweka tahadhari nje ya uzio wako, basi atakaeingia ndani kwako iwe mwizi au mtu unaemfahamu au jirani tu, akapata madhara, unakua hauhusiki kwa lolote litakalo mtokea. Anakua amekaidi tahadhari uliompa.

Ila usipofanya kuweka tahadhari, basi mtu yoyote akidhurika utawajibika kwa tatizo lolote litakalo tokea kutokana na hivo vitu vyako vya ulinzi.

NOTE: Nia na madhumuni ya kuwepo kwa sheria, ni kwaajili ya kulinda haki za watu (hata kama mtu ni mwizi au muuwaji ila kuna sheria zinazolinda utu wake).

Hata kwenye matumizi ya silaha za moto kwaajili ya ulinzi, mwizi anapoingia ndani kwako sheria hairuhusu umpige moja kwa moja na kumdhuru. Kuna hatua za kuzingatia kabla haujampiga risasi za moto.

1) Kama mwizi amekuja na silaha ndani kwako basi unaweza kujilinda na kulinda mali zako kwa kuitumia hio silaha dhidi yake.

2) Kama hajaja na silaha ya aina yoyote (Bunduki, Panga, Sime, Shoka) basi kabla ya kumpiga au kumjeruhi unapaswa;

a) Kumpa tahadhari/onyo kwa kutumia mdomo (Tahadhari, nina silaha ya moto, na ukikaidi onyo ntaitumia dhidi yako).

b) Akikaidi tahadhari yako na akaendelea kutaka kufanya uhalifu, basi hatua ya pili unapaswa kupiga risasi juu kumpa onyo ya vitendo. Na baada ya hapo akikaidi na akitaka kukudhuru ndio unapswa kuitumia kumjeruhi (Sio kumuua). Hapo unakua hauna kesi ya kujibu.

#Mazingira ya kujihami kwa kutumia silaha yanatofautiana na tukio lenyewe na sehemu husika. Hivo wakati mwingine mazingira yanalazimu mtu kujihami kwa k
 
Ni American Pitbull Mkuu Asante! pili tahadhari zote ziliwekwa vyema kabisa
 
acheni masihara na mbwa wazee,training dogs can kill in 5min,huyo mbwa anajua ni wap pakuanza na wap amalizie.mauaji yana utata kidogo.maybe planned or unplanned.
 
Siongei na mbwa, naongea na mwenye mbwa.
Kwa kesi hii binafsi sioni tofauti ya mbwa na bunduki, umefuga mbwa ambaye yuko trained kuuwa na siyo kukamata tu, hamna tofauti na kupiga risasi kuuwa badala ya kufukuza kwa kupiga hewani au kuvunja mguu jambazi, hatuwezi kuhukumu bunduki bali mfugaji wa bunduki/mbwa kwa matumizi yasiyofaa.
 
Back
Top Bottom