Msaada kuhusu hili suala la mbwa kuua mwizi na mmiliki wa mbwa kufunguliwa shtaka la mauaji

Oflam

Member
Nov 27, 2020
7
6
Msaada tafadhali juu ya scenario hii!

Kuna jamaa ana mji wake na katika mji huo ameweka ulinzi wa Mbwa hawa America Broiler pamoja na fensi, usiku kuna jamaa alienda kwa lengo la kuiba kwake alipofika eneo la tukio akaruka ukuta ili aweze kuingia ndani baada ya yeye kutua ndani akakutana na fujo za wale mbwa wakamng'ata mpaka jamaa akafa.

Mwenye nyumba kesho yake akaenda kutoa taarifa Polisi alipofika tu kutoa taarifa akakamatwa na kuwekwa kizuizini na kisha kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Je, hii iko vipi upande wa utetezi wa jamaa? Au jambo hili limekaa vipi kisheria?
 
Trespassing is against the law. Ndiyo mwizi alichofanya.

Though post mortem inaweza onyesha hakuuawa kutokana na majeraha ya mbwa ila trespassing is against the law.

Mwenye eneo akikuua anakua hana kosa.

Askari wanataka mpunga. Mwanasheria mzuri anamtoa jamaa.
 
Mbwa peke yake sio kazi rahisi kumuua binadamu mtu mzima
Kuna hizi breed ukikutana nazo zenye mafunzo kamilifu, kama mwenye mbwa hayupo umekwenda mbele ya haki

Jojo-Large-GSD-Female.jpg
e0f6aed279c6b23f9cdcb5dca8ae731a.jpg
 
Sikia ndugu io kesi lazima ifanyiwe uchunguz kwanza umejuaje km ni mwiz pili nn kilimuuq maana mbwa pekee yke not easy binadamu ana uwezo wa kuua mbwa ni minutes km upo strong
 
Sikia ndugu io kesi lazima ifanyiwe uchunguz kwanza umejuaje km ni mwiz pili nn kilimuuq maana mbwa pekee yke not easy binadamu ana uwezo wa kuua mbwa ni minutes km upo strong
Mtu ameruka ukuta, usiku mkubwa alafu unataka kujua kama alikuwa mwizi au laaa? Hapo iangaliwe kifo chake kimetokana na nini? Mbwa anakuuwa bila ubishi ndugu wewe sikia tu.
 
Msaada tafadhali juu ya scenario hii!

Kuna jamaa ana mji wake na katika mji huo ameweka ulinzi wa Mbwa awa America Broiler pamoja na fensi, usiku kuna jamaa alienda kwa lengo la kuiba kwake alipofika eneo la tukio akaruka ukuta ili aweze kuingia ndani baada ya yeye kutua ndani akakutana na fujo za wale mbwa wakamng'ata mpaka jamaa akafa.

Mwenye nyumba kesho yake akaenda kutoa taarifa Polisi alipofika tu kutoa taarifa akakamatwa na kuwekwa kizuizini na kisha kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Je, hii iko vipi upande wa utetezi wa jamaa? Au jambo hili limekaa vipi kisheria?
Hapa hata mimi kama ningekuwa polisi ningekuwa na mashaka. Inahitajika uchanguzi ufanyike kabla ya maelezo ya mwenye nyumba kukubaliwa.
1. Hakusikia kelele za mbwa wakati wanamshambulia?
2. Huyo aliyeuawa hakupiga kelele wakati anashambuliwa?
3. Kama aliuawa usiku ni kwanini alisubiri mpaka kesho yake ndiyo akatoe ripoti?
4. Majirani walisikia kelele? Ni nini maelezo yao?
Kuna mashaka mengi sana. Moyo wangu unakataa kuwa huyu ''kibaka'' aliingia kwenye uzio na mbwa wakamuua.
5. Hakuna uwezekano ''kibaka'' aliua nje ya uzio na mwili wake kuingizwa ndani?
6. Kuna uhakika gani alikuwa mwizi?
 
Msaada tafadhali juu ya scenario hii!

Kuna jamaa ana mji wake na katika mji huo ameweka ulinzi wa Mbwa hawa America Broiler pamoja na fensi, usiku kuna jamaa alienda kwa lengo la kuiba kwake alipofika eneo la tukio akaruka ukuta ili aweze kuingia ndani baada ya yeye kutua ndani akakutana na fujo za wale mbwa wakamng'ata mpaka jamaa akafa.

Mwenye nyumba kesho yake akaenda kutoa taarifa Polisi alipofika tu kutoa taarifa akakamatwa na kuwekwa kizuizini na kisha kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Je, hii iko vipi upande wa utetezi wa jamaa? Au jambo hili limekaa vipi kisheria?
SUALA NI MAUAJI YALIYOTOKEA HAPO. HAKUNA SHERIA INAYOSEMA MWIZI UKIMPATA BASI UMUUE. HAO MBWA NI MWIONGONI MWA WENYE HASIRA KALI
 
Hapa hata mimi kama ningekuwa polisi ningekuwa na mashaka. Inahitajika uchanguzi ufanyike kabla ya maelezo ya mwenye nyumba kukubaliwa.
1. Hakusikia kelele za mbwa wakati wanamshambulia?
2. Huyo aliyeuawa hakupiga kelele wakati anashambuliwa?
3. Kama aliuawa usiku ni kwanini alisubiri mpaka kesho yake ndiyo akatoe ripoti?
4. Majirani walisikia kelele? Ni nini maelezo yao?
Kuna mashaka mengi sana. Moyo wangu unakataa kuwa huyu ''kibaka'' aliingia kwenye uzio na mbwa wakamuua.
5. Hakuna uwezekano ''kibaka'' aliua nje ya uzio na mwili wake kuingizwa ndani?
6. Kuna uhakika gani alikuwa mwizi?
Hiyo ndio polisi nimeuliza hapo juu watu wakaniona mimi mjinga lazima wakuulize una uhakika gani kama ni mwiz na sio kusema tu ni mwizi kisa karuka ukuta
 
Ni American Pitbull au American Broiler? Navyojua broiler ni aina ya kuku wa kisasa maalum kwaajili ya nyama (Wanakua kwa haraka na wakubwa).

Anyway, turudi kwenye mada husika.

Sheria inasema unapoweka ulinzi wa kutumia "WANYAMA WAKALI au UMEME" ni lazima uweke kibao kwa nje kwenye geti la kuingilia nyumbani au ukutani kinachotoa "TAHADHARI/ONYO (Warning Sign)" juu ya uwepo wa hivo vitu.

Mfano, TAHADHARI KUNA MBWA WAKALI" au "TAHADHARI KUNA FENCE YA UMEME".

Ukifanya hivo ukaweka tahadhari nje ya uzio wako, basi atakaeingia ndani kwako iwe mwizi au mtu unaemfahamu au jirani tu, akapata madhara, unakua hauhusiki kwa lolote litakalo mtokea. Anakua amekaidi tahadhari uliompa.

Ila usipofanya kuweka tahadhari, basi mtu yoyote akidhurika utawajibika kwa tatizo lolote litakalo tokea kutokana na hivo vitu vyako vya ulinzi.

NOTE: Nia na madhumuni ya kuwepo kwa sheria, ni kwaajili ya kulinda haki za watu (hata kama mtu ni mwizi au muuwaji ila kuna sheria zinazolinda utu wake).

Hata kwenye matumizi ya silaha za moto kwaajili ya ulinzi, mwizi anapoingia ndani kwako sheria hairuhusu umpige moja kwa moja na kumdhuru. Kuna hatua za kuzingatia kabla haujampiga risasi za moto.

1) Kama mwizi amekuja na silaha ndani kwako basi unaweza kujilinda na kulinda mali zako kwa kuitumia hio silaha dhidi yake.

2) Kama hajaja na silaha ya aina yoyote (Bunduki, Panga, Sime, Shoka) basi kabla ya kumpiga au kumjeruhi unapaswa;

a) Kumpa tahadhari/onyo kwa kutumia mdomo (Tahadhari, nina silaha ya moto, na ukikaidi onyo ntaitumia dhidi yako).

b) Akikaidi tahadhari yako na akaendelea kutaka kufanya uhalifu, basi hatua ya pili unapaswa kupiga risasi juu kumpa onyo ya vitendo. Na baada ya hapo akikaidi na akitaka kukudhuru ndio unapswa kuitumia kumjeruhi (Sio kumuua). Hapo unakua hauna kesi ya kujibu.

#Mazingira ya kujihami kwa kutumia silaha yanatofautiana na tukio lenyewe na sehemu husika. Hivo wakati mwingine mazingira yanalazimu mtu kujihami kwa kutokufata hizo kanuni.
 
Msaada tafadhali juu ya scenario hii!

Kuna jamaa ana mji wake na katika mji huo ameweka ulinzi wa Mbwa hawa America Broiler pamoja na fensi, usiku kuna jamaa alienda kwa lengo la kuiba kwake alipofika eneo la tukio akaruka ukuta ili aweze kuingia ndani baada ya yeye kutua ndani akakutana na fujo za wale mbwa wakamng'ata mpaka jamaa akafa.

Mwenye nyumba kesho yake akaenda kutoa taarifa Polisi alipofika tu kutoa taarifa akakamatwa na kuwekwa kizuizini na kisha kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Je, hii iko vipi upande wa utetezi wa jamaa? Au jambo hili limekaa vipi kisheria?
Vipimo vikionyesha kuwa mbwa ndiyo kaua jamaa atakua na afueni tho bado anaweza akajitetea kwa sheria ya trespassing mti kuingia kwenye eneo la mtu bila ruhusa, ila kama ndiyo mbwa kaua kesi hapo hakuna, maana mbwa hana ufahamu kuwa kuua ni kesi ya mauaji, mbwa yeye yupo kwenye lindo kukutana na mwizi mbwa alijiami na kumkabili mwizi kwa kuwa alimuona ni adui,

Mimi sijasomea sheria ila naweza fanya utetezi juu ya hii kesi maana ina grounds za kukutetea.
 
Back
Top Bottom