Msaada kuhusu First Aid Kit kwenye gari ndogo, nimekamatwa asubuhi hii na Traffic

pangalashaba

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
1,235
2,000
Habari za Jumamosi wanajamvi,

Tafadhali mwenye ufahamu wa masuala ya usalama barabarani naomba anieleweshe kuhusiana na hili.

Alfajiri ya leo nikiwa namsindikiza ndugu yangu stand kuu ya mabasi Arusha, nilisimamishwa na askari wa usalama maeneo ya USA River, akakagua kigari changu premio then akaomba first aid kit.

Hapo ndipo aliponikamata maana hiyo kitu mmi sina.Hii imekaaje wanabodi?

Maana mimi nafahamu first aid kit ni kwa magari ya abiria tu, au uelewa wangu ni mdogo kuhusiana na hii kitu kwenye magari.

Please mwenye uzoefu na haya mambo mana wameniwasha ten alfajiri ya leo.
 

blackdog

Member
Jan 9, 2011
90
95
du, hata mm ilishanitokea maeneo ya KIA. mara moja tu nilikuwa na haraka nakwenda Moshi sikuwaelewa nikaona tukibishana nitapoteza muda nikawaomba msamahani kwa kuwaambia nilikuwa sifahamu, nitanunua uko mbele walinielewa. lkn sina uhakika kama ni kosa kwa gari ya privet
 

Dezoizo52

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
426
1,000
Hiyo kitu ni kwa magari ya abiria na mizigo kwa magari madogo si lazima. Huyo Trafic hajielewi
 

BLACK MARXIST

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
2,368
2,000
Nilishawahi kukamatwa Buhongwa kwa kosa hilo, nikatoka nikaenda mbali kidogo kuongea na simu sijui walihisi nini baada ya kurudi wakaniachia. Ila ki ukweli hilo sio kosa wakigoma kukuacha nendeni mahakamani.
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
8,934
2,000
Hakuna kosa hapo kwa gari lako binafsi ni kwa magari ya biashara hata taxi sawa...USA hapo wakorofi sana wanatafuta makosa ili wapate rushwa...
 

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,099
2,000
Hao ni wataka rushwa rekodi tupia clip humu wakiwa wanapokea rushwa tuwatambue kwa sura zao.
 

Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,326
2,000
Kuliko kwenda kukalishwa na kupotezewa muda wako wape hela ya kununulia nyama wewe utembee zako! Traffic kwenye utawala huu wamekuwa wajinga wajinga sana kama mwenzao!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom