msaada kuhusu cycocell | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada kuhusu cycocell

Discussion in 'JF Doctor' started by salito, Jan 12, 2012.

 1. salito

  salito JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  docta na wana jf nadhan hamjambo!me sina ufaham na huu ugonjwa wa cycocell,naomba kufahamishwa nini chanzo chake!na unadalili zipi na matibabu kama yapo..
   
 2. n

  ngwana ongwa doi Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sicle cell ni disorder ya redblood cells ambapo cell inakuwa na shape isiyo ya kawaida ina kuwa kama mwezi mchanga na rigid, inakua vigumu kupita kwenye blood vessel matokeo yake kufanya damu isipite kwa urahisi au kuzuia kabisa,matokeo yake ni kusababisha upungufu mkubwa wa damu sehemu zingine za mwili(anaemia) ambayo huitwa sicle cell anaemia.kawaida cells ni round na ni flexible.

  Tabia nyingine ya sicle cell ni kufa mapema zaidi kuliko cell zingine kabla ya kuwa replaced,cell hizi hufa baada ya siku 10-20 na kusababisha anaemia,wakati cell za kawaida huchukua siku 120 ndipo hufa.

  Sicle cell ni disorder ambayo mara nyingi ni ya kurithi toka kwa wazazi,hali hii husababishwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida yanayotokea kwenye DNA,ambayo ndiyo huhusika na utengenezaji wa vinasaba(gene).DNA ni master plan ya cell so makosa yanapofanyika katika master plan hii husababisha magonjwa au disorder mbalimbali mwilini mfano sicle cell nk.s.cell huanza kujitokeza mtoto awapo kuanzia miezi 4 na kuendelea.

  Dalili zinazojitokeza ni.
  1.Kupugukiwa damu(anaemia).
  2.Maumivu kwenye mifupa.
  3.kuugua mara kwa mara.
  4.kuvimba miguu kutokana na upungufu wa damu.
  5.kushindwa kuona vizuri baadaye kadri ugonjwa unavyozidi.
  6.kuchelewa kukua mtoto nk.

  Matibabu:
  Hakuna tba yake ila ni kutibu dalili zinazojitokeza.
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nitakuja badae ku-comment complications mbalimbali za sickle cell disease na tiba zake.
  Kwa sasa mda umebana.
  Kazi kwanza.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Nakusubiri..
   
 5. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Usiondoke
   
 6. salito

  salito JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Asante sana kwa ufafanuzi mzuri maana kweli nilikuwa shalow hata spelling nimevuruga aha ha ha ha ha ha asante sana..
   
 7. salito

  salito JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Nakusubiri kwa hamu sana..usiache kurudi wajameni..
   
 8. n

  ngwana ongwa doi Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna shida ni common mistake kumbe namimi nimesahau k teheeeeh kazi kwelikweli
   
 9. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Spelled:
  Sickle Cell Disease.

   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sickle Cell Disease
  Kama alivosema ngwana ongwa...
  Ni tatizo la chembe hai (seli) nyekundu za damu ambazo ndo huhusika na kusafirisha hewa ya Oxygen mwilini.
  Hizi seli zilizoathirika zina-assume shape ya MUNDU (=sickle) hence the name of disease.
  Norma red cells ni mviringo bapa.
  Hebu cheki picha hii itawasaidia kucatch-up.
  [​IMG]
   
 11. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa Bantu stock inaitwa sickle cell na kwa semites inaitwa spherocytosis. Hii ni cingenita disorder. Unaweza kuwa carrier au deseased. Kama wazazi wote ni carriers basi watoto waweza kuwa deseased. Lakini kama mzazi mmoja tu ni carrier basi robo ya watoto watukuwa pia carriers. Red Blood Cells zinakuwa na shape ya mwezi mchanga sababu ya ukosefu wa enzyme inayo tumia follic acid kutengeneza cell membrane kwa hiyo haiwezi kubeba Oxygen vizuri.
   
 12. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  These Sickled red cells lacks deformability property of normal red cells.
  Hii ni kuwa inashindwa kubadili umbo kutokana na inakopita hasa kwenye njia nyembamba, capillaries.
  Even normal red cells can transform into sickled cell in situations kama homa kali, infection, baridi mwilini(hypothermia), Kuongezeka kwa tindikikali (acid) mwilini [au =ACIDOSIS], kupungua kwa maji mwilini(dehydration), n,.k, n.k.
   
 13. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Haya ni magonjwa mawili tofauti.
  Yote ni ya kurithi.
  Pathogenesis and Pathology diferrent
   
 14. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kutokana na shape yao, hizi sikled red cells zinapopita kwenye mishipa myembamba sana ya damu(capillaries), zinashindwa kupenya kwa urahisi, hivyo zinakwama na kuziba mshipa.
  [​IMG]
  Kinachoendelea baada ya blockage, u can guess!!
  No oxygen delivery to the tissues at the periphery.
  Chakula/nutrients can not reach tissues at the perphery.
  As a result, they literary suffocate to death.
  The process can occur at any part of the body: mapafu, mifupa( ndo common sana), tumboni, brain, n.k, n.k.....
   
 15. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Pia hizi Sicked red cells, zikipita kwenye spleen (=sijui ndo bandama), zinaharibiwa.
  In short, the life span of these cells are markedly reduced.
  Mgonjwa aweza kuonyesha dalili za upungufu wa damu(anemia). Ikumbukwe huu ugonjwa pia hujulikana kama SICKLE CELL ANEMIA.
  Mahitaji ya kuongezewa damu mara kwa mara hutokea hasa utotoni.
   
 16. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Pia hizi Sicked red cells, zikipita kwenye spleen (=sijui ndo bandama), zinaharibiwa.
  In short, the life span of these cells are markedly reduced.
  Mgonjwa aweza kuonyesha dalili za upungufu wa damu(anemia). Ikumbukwe huu ugonjwa pia hujulikana kama SICKLE CELL ANEMIA.
  Mahitaji ya kuongezewa damu mara kwa mara hutokea hasa utotoni.
   
 17. salito

  salito JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  asante sn kwa kutuelimisha wana jf,na sasa ni kweli eti umri unaokadiriwa kuishi kwa watu wenye ugonjwa huu ni miaka15?ikizid hapo ni bahati?na kama sio kwa ugonjwa huu ni ugonjwa upi mwingine unaosemekana kuwa hvy?
   
 18. salito

  salito JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mhh inatisha sn kwakwel MUNGU atusaidie tu.
   
 19. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  kwa kiswahili ndio unaitwa ugonjwa manjano?
   
 20. n

  ngwana ongwa doi Member

  #20
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafikiri mtu akishakiri makosa yake hakuna haja ya kuendelea kuyaonyesha makosa yake kwenye thr.ya hapo juu tumeonyesha jinsi tulivyo kusoea,najua wakati wowote mtu aweza fanya mistake may be wewe huwa haufanyi makosa hongera sana.
   
Loading...