Msaada kuhusu biashara ya mitungi ya gesi

genious wa kijiji

Senior Member
May 1, 2014
166
250
4hrs hamna reply hata moja! ingekua mambo ya mapenzi na kutongoza kungekua na replies nyingi sana. anyways, kuna uzi nimeona mzuri nimekopi hii...

Anza hivi
Mtaji ni million 15
Nunua kirikou
Budget weka mil 7 utapata nzur tu
Nenda kwa super dealer wa gas nunua
Mitungi ya gesi
Midogo 100
Mikubwa 40
Midogo tupu 23000 ukijaza 15800 jumla 38800 × 100=3,880,000
Mikubwa tupu 42000 ukijaza 38000 jumla 80000×40=2,400,000
Jumla mtaji gas n 6,280,000 ukijumlisha na kirikou 13,200,00
Kodi ya stock ya gas itakapokaa 50,000×6=300,000
Vibali +Kumodify body ya kirikou ges zikae ktk uzio wa machuma+mengineyo weka 500,000
Jumla mil 14,000,000 cash
Hio million moja baki nayo km balance kwa dharura
*unasupply kwenye maduka ya reja reja ya gesi
*wewe ndio dereva wewe ndio salesman
*mtungi mdogo unauzwa 17000 mkunbwa 41000 kwa wiki hukosi kusambaza 600units -400 units kwa daresalaam maana miduka n mengi sana
*kapge kazi mchanganuo huo hapo uje na ushuhuda hapa*

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
2,995
2,000
Huo mtaji. Mhh lkn ahsante kwa mchanganuo, umenifungua akili
Huo mtaji umechangamka na kwenye mchanganuo Kuna makosa kidogo ukiufuatisha Kama ulivyo mbeleni unakwama.
Kwa mfano kwenye bei ya kirikuu sio milioni 7 bali ni zaidi ya milioni 9.
Na kwenye kodi ya frem 50000tsh ni nje ya mji halaf mtaani ila Kama ni maeneo ya centre kodi inaanzia 150000tsh kwa mwezi.
Na Kuna vitu vingine vimekosekana Kama kodi ya tra n.k.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom