Msaada kuhusu biashara ya kuagiza laptops nje ya nchi

kikiboxer

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
3,044
8,064
Wakuu salaam sana.
Nimepata kamtaji kidogo nataka nijiongeze nianzishe biashara ya kuagiza laptops used toka Uk.

Tayari nina contacts na suppliers kadhaa ambao wameonesha utayari wa kufanya nao biashara.

Tatizo langu kubwa na lilofanya niombe ushauri ni kuhusu kiwango cha kodi wanachotoza kama ushuru wa customs kwenye aina hii ya bidhaa nisije nikatelekeza mali yangu kwa wazee wa TRA baada ya kununua na kulipia mzigo kabisa.

Kama kuna yoyote ana uzoefu na hii kitu au anajua naomba msaada tafadhali.
 
Hakuna watu wenye ujuzi huu humu maana hata Mimi nilishawahi kuuliza Kama maswali ya hivi Kama mawili lakini sikujibiwa,kukushauri ingia kwenye mtandao search TRA dar es salaam uchukue contacts zao kisha piga uwaulize, ila siku za kupiga simu ni jumaatatu hadi ijumaa kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni ndo mda mzuri wa kuwapata,
 
Ukiamua kubadili supplier kwenda China nina connection ya uhakika na usafiri pamoja na kodi ni usd 50 per pc
 
Asante sana mkuu.
Kwa haraka haraka wewe uliwacheki na walikupa taarifa yoyote ambayo unaweza kushare?
 
Ukiamua kubadili supplier kwenda China nina connection ya uhakika na usafiri pamoja na kodi ni usd 50 per pc
Poa mkuu hii kodi ni standard kwa laptop zote au ni baadhi tu.?
Then ukichukua mzigo toka china kodi itakuwa chini kuliko huko UK? Naomba ufafanuzi.
 
Kodi huwa ni asilimia fulani kwa kila aina ya bidhaa sikumbuki vizuri, ila unapoagiza mzigo inategemea unaupitisha wapi? na anaye clear ni nani? Cha msingi ni kuwa jua kwanza kodi halisi then check shorts cuts.....
 
Mkuu mimi sijui habari za UK, nina uzoefu na uchina tu.
Hiyo bei nimesema ni usafiri pamoja na kodi na ni flat rate kwa zoooote.
Lakini ni dhahiri ukiagiza UK gharama zitazidi kutokana na means za usafiri kutoka UK kuwa ngumu kuliko China
 
Vyombo vya elektroniki vilisamehewa kodi kama sijakosea!!, lakini wasiliana na jamaa wa TRA wakati wa kutafuta TIN watakupa mwongozo. Lakini pia wakati wa kuomba leseni ya biashara utapata majibu yote kulingana na biashara unayoilenga.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom