Msaada: kuezeka nyumba yenye square metre 371 gharama kiasi gani?

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Habari.

Kuna kibanda cha square metre 371 kimefikia hatua ya kupaua na kuweka bati , je makadirio ya gharama inaweza kuwa shs ngapi?

Natangiliza shukrani.
 
Square meter 371, ambayo ni 19×19 mkuu hii nyumba mbona kubwa sana, duh hapo kwenye kupaua na finishing yake jiandae kisaikolojia, nilijenga nyumba ya square meter 99 kupaua na finishing haikuwa rahisi
 
Ya kwangu moja ya 11 x 14 ilichukua 12m; kwa hiyokulingana na ukubwa wa nyumba yako inawezezekana wewe ujiandae kwa kuanzia 27m
Kupaua tu kuanzia mil 27? Mbona tunakatishana tamaa jamani?
 
Kupaua tu kuanzia mil 27? Mbona tunakatishana tamaa jamani?
12 milioni 11×14 umeingiza hela nyingi mno
Haiwezekani

Siyo kukatishana tamaa wala ku-inflate gharama. nadhani inatagemea zaidi unanunua wapi vifaa vyako. Kwa nyumba yangu ile ilichukua bati za aluminium nyekundu 155 @ TSh 45,000 halafu kulikuwa na misumali ya bati kilo 30@8000, mbao (papi) zote za kench zilikuwa 260 @7000, misumali ya kench kilo 30@3000, Fishboard pcs 20@7000 pamoja na waya za kenchi piece 8 @ 2400, mbao za upenu 30@9000, pamoja na gharama za usafirishaji wa vifaa, gharama za mafundi pamoja na vibarua. Hesabu yote ilikuwa m11 laki 7 ndiyo maana nilipiga raundi ya m12.

Bati za Aluminium zinazouzwa kwa piece moja ni ghali sana kuliko bati za kawaida zinazouzwa kwa bando.
 
Fanya estimation cost ni = 371 x 1.5 x 25,000 = Bati tu 13,912,500/= kwahiyo waliosema andaa 12m ,14m wakpo sahihi.
 
Square meter 371, ambayo ni 19×19 mkuu hii nyumba mbona kubwa sana, duh hapo kwenye kupaua na finishing yake jiandae kisaikolojia, nilijenga nyumba ya square meter 99 kupaua na finishing haikuwa rahisi
mkuu naomba ramani yako nimependa sana ivyo vipimo 10M kwa 9.9M
 
Ya kwangu moja ya 11 x 14 ilichukua 12m; kwa hiyokulingana na ukubwa wa nyumba yako inawezezekana wewe ujiandae kwa kuanzia 27m
Mmmh mkuu sio kwamba unamtisha sna jamaa. Bati za namna gani hizo?
 
Fanya estimation cost ni = 371 x 1.5 x 25,000 = Bati tu 13,912,500/= kwahiyo waliosema andaa 12m ,14m wakpo sahihi.
Hii ni kwa bati aina gani mkuu? Unaweza kutoa ufafanuzi hiyo 1.5 na 25,000 zina stand for index gani?
 
Hii ni kwa bati aina gani mkuu? Unaweza kutoa ufafanuzi hiyo 1.5 na 25,000 zina stand for index gani?

Mkuu kuna sehemu nilitoa hiyo formula kujua gharama za kuezeka yaani bati+mbao+materials.

Ni kama kujua gharama ya ujenzi wa nyumba za contractor wanatumia formula ya sqm x 500,000/=

Kwahiyo hiyo kuezeka wewe tafuta size ya nyumba x 1.5 x 25,000/= Unapata Estimation Cost....Ukiambiwa estimation ni makadirio kwahiyo inaweza ikazidi au ikapungua ila itarange humo humo + or - 10%.
 
mkuu naomba ramani yako nimependa sana ivyo vipimo 10M kwa 9.9M
kwa hapa sina mkuu ila ni 11 kwa 9 ambapo niliigawa mara tatu.
1. upande wa kwanza kuna master na choo chake, pia choo cha public,
2. upande wa pili ni sitting room, dining na kitchen.
3. Upande wa tatu ni vyumba viwili vya watoto na vyoo vyake. Vyumba vya watoto ni 3x3, vyoo vimegawanywa kutoka kwenye ile 3x3 nyingine nakuwa nimekamilisha 9. Upande wa pili sitting ina upana wa 4.2 , master ina 3.8.
 
naipataje boss wangu.
 
Back
Top Bottom