Msaada: Kodi zinazohusu nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Kodi zinazohusu nyumba

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KASRI, Dec 16, 2010.

 1. K

  KASRI Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanajamii, ninaomba msaada wa kueleweshwa kuhusu kodi iitwayo "Withholding" (Withholding Tax) kwenye nyumba za kupanga.Nimempangisha mtu kwenye nyumba yangu iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam - Tanzania. Tumekubaliana kuhusu kodi na kusainiana mkataba. Malipo aliyonipa ni pungufu na matarajio yangu, nilipomuuliza akasema amepunguza "withholding tax" ambayo atailipa TRA.Swali langu kwenu wanajamii;1. Ni nani anayepaswa kulipa hii kodi? I mean ni mwenye nyumba yeyote au kuna baadhi?2. Nisipolipa madhara ni nini? - asipolipa huyo mpangaji nani ataulizwa?3. Hii kodi ni asilimia ngapi ya kodi ya jengo?4. Hii kodi ni kwa baadhi ya maeneo au ni kila sehemu?Natanguliza asante kwa majibu yenu.
   
 2. L

  Lady JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kasri, With holding tax according to TRA kwa Residential houses ambazo kodi yake kwa mwaka inazidi laki tano, mpangaji anatakiwa alipe with holding tax, kwa residents ni 10% na kwa Non-residents ni 15%. Ila huwa naona wengi wa wapangaji wanaolipa kodi hii ni wa kwenye commercial buildings, lakini kwenye residential sioni ufuatiliaji wa hii kodi, so naona kama haina ulazima wa kuilipa hasa kwa watu ambao accounts zao haziwi audited.
   
 3. K

  KASRI Member

  #3
  Dec 17, 2010
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thanks Lady:Do we have any place where i can make reference; say an Act, Law ......
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Kwani kwenye mkataba kuna clause yoyote kuhusu yeye kulipa kodi hiyo? Kama hakuna basi lazima akupatie pesa yote na kama atabanwa na serikali basi ataonesha mkataba na wewe kudaiwa. Na kama kweli analipa basi akupatie nakala ya malipo hayo. Hakishindwa basi ujue huyo uwezo wake mdogo kuishi kwenye nyumba yako na aondoke kwani amekiuka mkataba.
   
 5. L

  Lady JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Check TRA website or any TRA office
   
 6. L

  Lady JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  This is a gud advice, lazima kwenye mkataba ionyeshe mlikubaliana alipe withholding tax, if not, amevunja mkataba, au akupe risiti aliyolipia TRA, akishindwa mwondoe tafutab anayekidhi vigezo vyako.
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Lady,

  Naomba nikusahihishe kidogo, kodi inachajiwa kulingana na sheria za kodi tulizojiwekea wenyewe kupitia bunge! Ku comply na sheria sio option ni lazima na wajibu wetu sote! Hivyo usiseme ni commercial landlords tu ndo hulipa kodi na hawa wengine wa residential hawalipi na hivyo huyu bwana asilipe kodi hii si kweli! mshauri alipe kodi kama sheria inavotakiwa.

  Pili, withholding tax on rental ni 10% kwa residents na non-residents. Kuna utofauti kweny wtax on service fees tu.

  Kasri,

  Sheria inayokufanya ukatwe hiyo 10% ni ile ya sheria ya fedha ya mwaka 2004 (ITA 2004) kifungu cha 82(1)(a) na Schedule 4 ya sheria hiyo hiyo.

  Pia kifungu cha 84 cha sheria hiyo kinamtaka withholding agent kupeleka kodi hiyo kwa kamishna ndani ya siku saba baada ya mwezi wa makato. Hivyo basi mwenye wajibu wa kukata na kulipa kodi hiyo ya zuio ni mpangaji wako na sio wewe mwenye nyumba.

  Kumbuka kodi hii kwa watu binafsi (individuals) ni final, huwezi kuja offset anywhere lakini ungekuwa na business, ingekuwa treated kama advance tax halafu mwisho wa mwaka ingekuwa offset against the final liability ya mwaka mzima.

  Hope this clarifies.

  NL
   
 8. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu kwa kuwaelimisha hawa landlords, kwa kuongezea tu ni kwamba according to sheria tajwa ..mpangaji anatumika kama agent wa kuikusanyia kodi TRA. Hivyo sheria inampa mamlaka mpangaji wako kuikusanya hiyo kodi na ukitaka atakuletea evidence ya malipo.
   
 9. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Hii ni moja ya faida za kusajili biashara au sio?
  Nikitaka kujifunza zaidi kuhusu hizi faida/sheria kitabu gani kitanifaa?
   
Loading...