Lifahamu kiundani zao la Nyanya chungu (Ngogwe) na jinsi ya kulilima

Kubota

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
532
1,089
1603024592551.png


Hatua za kufuata ukitaka kulima nyanya chungu
Nyanya Chungu ni zao la Kitropic linalotoa mazao yake kama matunda au kama mboga. Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyupe. Kuna aina mbalimbali za nyanya chungu ambazo ni ni nyanya chungu za asili na zingine ni chotara siyo chungu kama za asili.

Mazingira
Zao hili hustawi vizuri maeneo yenye baridi ya wastani na joto la wastani kuanzia nyuzi joto 25°C hadi 35°C, hupendelea udongo tifu tifu usiotwamisha maji na wenye rutuba. Kama utaweza kutumia mbolea za samadi na mboji au mbolea za asili pamoja , basi nyanya chungu hustawi vizuri sana.

Kuandaa shamba
Mbegu za nyanya chungu huandaliwa kwenye kitalu kwanza kabla ya kupelekwa shambani.

Maelekezo ya kuandaa kitalu cha nyanya chungu.
- Chagua eneo la kuanzisha kitalu kwenye maeneo yanayopatikana maji kwa urahisi.
- Inua udongo wa kitalu hadi kufikia kimo cha sm 20 na upana wa mita 1 na urefu wowote. Bonda bonda mabonge makubwa ya udongo ili kupata udongo laini.

- Weka mbolea ya asili iliyooza vizuri, changanya ndoo moja kubwa ya lita 20 ya mbolea hiyo kwa eneo la mita 1 kwa mita 1 (1 m2). Kwa hiyo kama tuta lako la kitalu lina urefu wa mita 5 na upana mita 1, utaweka ndoo 5 za mbolea za asili.

- Kama ni wakati wa kiangazi, mwagilia tuta lako kwa siku 3 mfululizo mpaka udongo uloane vizuri.

Kusia mbegu
Maelekezo ya namna ya kusia mbegu kwa usahihi
- Tengeneza vimifereji vyenye kina cha sm 2 kukatisha tuta, nafasi kati kimfereji kimoja na kingine ni sm 15 au nusu rula.

- Sia mbegu zako ndani ya vimifereji hivyo, halafu funika na udongo laini.
- Weka matandazo ya nyasi juu ya tuta ili kuzuia jua kali na matone ya maji ya moja kwa moja.
- Mwagilia maji kitalu chako juu ya nyasi asubuhi na jioni kila siku. Ila inashauriwa kumwagilia kitalu chako maji wakati wa jioni.

- Mbegu za nyanya chungu huota baada ya siku 10 hadi 14 tangu kusia. Baada ya mbegu kuota toa matandazo ya nyasi halafu yaweke matandazo hayo katikati ya mistari ya miche.
- Tengeneza kivuli cha matandazo ya nyasi juu ya kitalu chenye kimo cha mita moja, kivuli hicho cha nyasi lazima kiwe kinapitisha mwanga wa jua walau kidogo ili kuruhusu mwanga kuifikia miche.

Kupandikiza miche shambani
Miche huwa tayari kuhamishiwa shambani baada ya mwezi mmoja hadi mwezi mmoja na nusu tangu mbegu kuota. Nafasi ya kupandikiza nyanya chungu ni mita 1 kwa mita 1 (yaani mita 1 shina hadi shina na mita 1 mstari hadi mstari)

Kabla ya kupandikiza miche chimba mashimo yenye ukubwa kiasi, weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha mkono mmoja uliojaa, halafu fukia udongo kiasi. Baada ya kufukia udongo pandikiza mche wako, kila shimo mche mmoja. Kama ni kipindi cha kiangazi pandikiza wakati wa jioni, baada ya kupandikiza mwagili maji vizuri.

Kutunza shamba
Mimea jamii ya mbogamboga ikiwemo nyanya chungu haipendi bugudha ya magugu shambani, kwa hiyo hakikisha unafanya palizi wakati wote kuakikisha magugu hayaathiri ustawi wa mmea.
Dhibiti magonjwa na wadudu mabalimbali wanaoathiri zao hili, kwa kutumia madawa mabalimbali na matumizi ya mbolea mbalimbali za kurutubisha mimea pale inapobidi na iwe ya kilimo hai.
KUVUNA

Nyanya chungu huwa tayari kuvunwa ndani ya siku 90 hadi 120 tangu kupandikiza. nyanya chungu inaweza kuvunwa mara 1 au mara 2 kwa wiki. Matunda ya nyanya chungu yanatakiwa kuvunwa kabla hayajabadilika rangi kutoka nyeupe kwenda njano mpauko.

matunda haya ya nyanya chungu yanaweza kusindikwa kuwa unga. Ili kusindika nyanya chungu kuwa unga fwata hatua zifuatazo;

- Chagua nyanya chungu bora na zioshe kwenye maji
- Kata kata nyanya chungu hizo kutengeneza vipande vidogo dogo, halafu tandaza vipande hivyo kwenye mkeka au turubai safi

- Anika vipande hivyo vya nyanya chungu juani hadi vikauke.
- Baada ya vipande hivyo kukauka vizuri, visage kwa kutumia kinu au mashine ya mkono mpaka viwe unga.

- Tunza unga huo kwenye chombo kisafi ambacho hakingizi hewa.
- Unaweza kutumia unga huo kwenye maharage, karanga, nyama na mboga zingine, mboga iliyowekwa unga huu wa nyanya chungu inakua tamu mno na inakua na virutubisho vya kutosha.

Wadau ahitaji kujua zaidi kuhu kilimocha nyanya chungu na jinsi ya kupata masoko
Thanks Kubota kwa kuleta uzi huu. Shukrani pia kwa wachangiaji wote. Nina maswali machache kuhusu hili zao hope Kubota, Malila, Mama Timmy, Goodmother au yeyote atakaepitia huu uzi anaweza kunisaidia
1) Kigamboni Dar Es Salaam linaweza kustawi?
2) Kama jibu la kwanza ni ndio, ni miezi ipi mizuri ya kusia mbegu kwenye vitalu na miezi ipi mizuri ya kuanza kupanda?
3) Mavuno yake yakoje? Kwenye eka moja naweza toa kiasi gani (kilo, kiloba, ndoo etc) kwa muda (wiki etc) gani?
4) Soko lake likoje? Bei ya kuuzia ni sh ngapi na kwa kipimo kipi (kilo, kiloba, ndoo etc)
5) Nimeona kuna changamoto ya mbegu mbaya or fake, unaweza kunitajia exactly duka lenye mbegu nzuri na bora
6) Nimeona kuna changamoto nyigine ya mifugo kama kuku, mbuzi, hii nitajitahidi kupambana nayo
7) Kuna changamoto nyingine zaidi ya hizo?

Samahani sana kwa maswali naona yamekuwa mengi
----
Heshima kwenu wanaJamvi Nimelima eka1 ya nyanya chungu na Mahindi Mabichi MVUMI KILOSA Morogoro nashukuru mazao yamekubali sana khs Nyanyachungu Inatakiwa kila wk nivune nakuuza zikikaa sana znabadilika Rangi inakuwa C ishu ss Tatizo nililo nalo nina Mteja 1 kwakweli ananiua Nimeona nije kwenu nikiamini hamtakosa chakunishauri Natanguliza shukrani wandugu!​
----
Wakuu naomba ushauri na maelekezo namna ya kulima nyanya chungu zile zisizokuwa chungu,ambazo hutumika sana majumbani, tafadhari naomba msaada na hali ya masoko.

Wadau mbalimbali wachangia kuhusu zao hili la nyanya chungu
Linapokuja suala la ujasiliamali ni mazao yenye majina makubwa tu kama matikiti, vitunguu na Tomato hutajwa! Nyanya chungu ni zao lisilovuma sana japo linawatoa sana wakulima na linawalaji wengi sana. Nyanya chungu mfano aina maarufu kama YEBOYEBO ni zao linalonivutia sana kwa sifa zifuatazo:

1. Afrika ni nyumbani kwao linazaa sana hata wakati wa joto kali ambapo kwa tomato na hoho hubabuka sana kwa jua
2. Tomato na Hoho hupunguza sana kutoa maua na matunda kwenye joto kali YEBO YEBO hupeta tu
3. Mazao mengi ya bustani huhitaji madawa ya ukungu kupita kiasi majira ya mvua, nyanya chungu hazideki ki hivyo
4.Tomato na hoho usafirishaji wake ni kama mayai, nyanya chungu zisafirishwapo mara nyingi watu hukaa juu yake
5. Kipindi cha kuanza kuchuma hadi mmea kuchakaa kwa aina nyingi za tomato ni mwezi mmoja, hoho zenye ubora ni miezi 2, lakini nyanya chungu huchumwa kwa zaidi ya miezi 8 ili mradi zinamwagiliwa maji na mbolea.
6. Wakati bei ya Tomato ikianguka mkulima nae hugalagala chini asisimame tena lakini nyanya chungu haimtupi mkulima kivile

Kwa wenye mitaji midogo wanaotaka kuikuza ili waweze kupata nguvu kubwa ya kilimo bila kuwa na presha inayopanda na kushuka Nyanya chungu ni zao lenye uhakika mkubwa!

Swali ni kwa nini zao hili halitajwi sana yaani halivumi ?
----
Wapendwa Sabayi na Mama timmy, hapo juu nimeambatanisha ka-kipeperushi kenye taarifa nyingi ndani yake, fungueni hiyo attachment msome. Kwa ufupi zao la Ngogwe ama nyanya chungu halihitaji maji mengi kama ilivyo kwa Tomato na linahitaji mwanga mwingi. Halistawi sehemu zenye kutuamisha maji na sehemu zenye kivuli kikali.

Linastawi katika aina nyingi sana za udongo ikiwamo udongo wenye kichanga kiasi. Zao hili linastawi ukanda wote wa pwani, nyanda za kati na nyanda za juu. Kwa ujumla eneo lolote ambalo bilinganya na Tomato hustawi, linafaa pia kwa kilimo cha Nyanya chungu haya mazao niliyoyataja hapa ni mazao yenye undugu.

Nyanya chungu huchukua siku 45 kutoa kusia kitaluni hadi kuwa tayari kupandikizwa. Mavuno huanza miezi miwili baada ya kupandikiza. Likipatiwa matunzo ni zao lenye ukarimu na kamwe halina maringo wala nyodo kama TOMATO na Hoho.
-----
Ni kweli anza na zao ambalo ni low risk na lenye faida. Anza eneo dogo. Awamu hizi za kwanza zitakuwa ni darasa lako la vitendo ambapo utajifunza kwa vitendo utunzaji wa zao husika na changamoto zake na matokeo yake utayaona kwa macho. Pia itakuwa ni darasa lako la kujifunza mambo ya masoko na mbinu za uuzaji. Kuna mazao low risk ya shamba na kuna mazao low risk ya Bustani. Ni budi uwe wazi unataka kufanya uzalishaji wako eneo gani na iwapo kilimo ndiyo itakuwa full time employment kwako. Wakati ukiendelea kutafakari pitia kusoma ushauri niliowahi kumpa ALF kwenye thread yake ya "Msaada wa ushauri" huenda kukawa na kipengele kitakachokufaa.

Ninakusisitiza sana mtumie huyo jamaa yako ambaye tayari alishaingia kwenye gemu ili utumie uzoefu wake. Kama alilima kwa gharama ndogo namna hiyo akapata faida mtumie na ulime zao hilo hilo japo kwa eneo dogo. Huyo jamaa atakuwa tayari anajua wapi kwa kuuza, anajua wateja na anajua changamoto za zao hilo, huyo jamaa mchukulie kuwa ni sehemu ya mtaji wako pia. Usianze kulima zao ambalo huna taarifa zake zozote, hujui mbinu za kulilima, hujui soko lake na hujui changamoto zake usifanye hivyo katu!
----
UTANGULIZI

Nyanya Chungu au Ngogwe ni zao la kitropic linalotoa mazao yake kama matunda na kutumika kama mboga, kuna aina mbalimbali za nyanya chungu ambazo ni nyanya chungu ambazo ni za asili na zingine ni chotara siochungu kama za asili. Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na yakipevuka kabisa hugeuka mekundu.
Matunda yafikia hatua ya kupevuka huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga zingine. Pia hupikwa pamoja na ndi.

AINA ZA NYANYA CHUNGU
Gilo
Kumba
Shum

ASILI YAKE
Nyanya chungu asili yake ni Afrika Magharibi, lakini kwa sasa ime sambaa Afrika ya kati na mashariki. Kutokana na ugunduzi wake Afrika magharibi, zao hili pia linalimwa huko Visiwa vya Karibi, Amerika kusini na baadhi ya maeneo ya kusini-magharibi mwa Asia. Nyanya chungu hulimwa kwa matumizi ya chakula, matumizi ya dawa, na matumizi ya mapambo.

HALI YA HEWA
Nyanya chungu za aina zote hustawi sana sehemu yenye jua na udongo wenye kupitisha maji vizuri na udongo wenye pH kati ya 5.5 na 6.8. Gilo ni aina ambayo hustawi sana kwenye joto la mchana ni kati ya 25°C na 35°C (77°F na
95°F). Kumba ni aina hustawi maeneo yenye joto sana la 45°C na unyevu kidogo, Shum ni aina inahitaji joto na unyevu ili kustawi. Hakuna aina ya Nyanya chungu inayovumilia kwenye baridi kali na hali ya majimaji.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Lima shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Mbegu za nyanya chungu zinauzwa kutoka baadhi ya makampuni ila kuna njia ya kupata mbegu kutoka kwenye tunda. Chukua nyanya chungu iliyokomaa menya vizuri baada ya hapo kusanya mbegu zilizopo ndani ya tunda, baada ya hapo ziweke kwenye kipande cha karatasi ili zikauke katika sehemu isiyopitisha mionzi ya jua ya moja kwa moja. Mbegu zikisha kauka zinaweza kutunzwa kwa miaka mingi na kuendelea kutumika. mbegu lazima zioteshwe kwenye kitalu cha sentimita 15 (6 inch) au zaidi 20 cm (8 inch) ya safu. miche kutoka kitaluni inakuwa tayari kupandwa ikifika urefu wa
sentimita 15 mpaka 20 (6–8 inch) na iwe na majani 5–7. Mmea inatakiwa uwe na nguvu katika mashina na yenye nafasi ya sentimita 50 (20 inch) mbali ruhusu sentimita 75 (30 inch) ya
safu.

UPANDAJI
Kutoka kwenye kitalu miche ifikiapo kimo cha sentimeta 15 hadi 20 au majani manne 5-7 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50 kwa 75 au sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii kutegemeana na ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya “Ngogwe” hutunzwa kama bilinganya, huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa miezi miwili baada ya kupandikizwa, na uvunaji huendelea kwa muda mrefu kidogo.

MBOLEA
Zao hili unashauriwa kutumia mbolea za asili (samadi au mboji kuongeza uzalishaji wa mazao. Mmea wa nyanya chungu unahitaji sana madini.

UPALILIAJI & UNYEVU
Shamba la nyanya chungu linatakiwa lipaliliwe kwa kuondoa nyasi na liwe safi ili kudhibiti magonjwa na wadudu, unyevu unahitajika ili kuongeza mavuno.

MAGONJWA &WADUDU
Nyanya chungu ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na baadhi ya Magonjwa yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara yake si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha
tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.

UVUNAJI
Nyanya chungu huvunwa wakati zikiwa bado mbichi, hukomaa baada ya siku 100 mpaka 120 kutoka kupandwa, unashauriwa uvune kabla hazija badilika rangi . Ili ziweze kukaa kwa muda mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika,
inapendekezwa kuzichuma pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa kuzitayarisha kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi masoko ya mbali bila kuharibika.

SOKO
Soko la nyanya chungu linaonekana kuwa zuri maana wahitaji wake ni wengi, ila fanya utafiti ili kujiridhisha soko lake.
 
Funguka zaidi mkuu Inachukua muda gani tangu kupanda hadi kuvuna? ni maeneo gani inakubali vizuri?
 
Wapendwa Sabayi na Mama timmy, hapo juu nimeambatanisha ka-kipeperushi kenye taarifa nyingi ndani yake, fungueni hiyo attachment msome. Kwa ufupi zao la Ngogwe ama nyanya chungu halihitaji maji mengi kama ilivyo kwa Tomato na linahitaji mwanga mwingi. Halistawi sehemu zenye kutuamisha maji na sehemu zenye kivuli kikali.

Linastawi katika aina nyingi sana za udongo ikiwamo udongo wenye kichanga kiasi. Zao hili linastawi ukanda wote wa pwani, nyanda za kati na nyanda za juu. Kwa ujumla eneo lolote ambalo bilinganya na Tomato hustawi, linafaa pia kwa kilimo cha Nyanya chungu haya mazao niliyoyataja hapa ni mazao yenye undugu.

Nyanya chungu huchukua siku 45 kutoa kusia kitaluni hadi kuwa tayari kupandikizwa. Mavuno huanza miezi miwili baada ya kupandikiza. Likipatiwa matunzo ni zao lenye ukarimu na kamwe halina maringo wala nyodo kama TOMATO na Hoho.
 
Wapendwa Sabayi na Mama timmy, hapo juu nimeambatanisha ka-kipeperushi kenye taarifa nyingi ndani yake, fungueni hiyo attachment msome. Kwa ufupi zao la Ngogwe ama nyanya chungu halihitaji maji mengi kama ilivyo kwa Tomato na linahitaji mwanga mwingi. Halistawi sehemu zenye kutuamisha maji na sehemu zenye kivuli kikali. Linastawi katika aina nyingi sana za udongo ikiwamo udongo wenye kichanga kiasi. Zao hili linastawi ukanda wote wa pwani, nyanda za kati na nyanda za juu. Kwa ujumla eneo lolote ambalo bilinganya na Tomato hustawi, linafaa pia kwa kilimo cha Nyanya chungu haya mazao niliyoyataja hapa ni mazao yenye undugu.

Nyanya chungu huchukua siku 45 kutoa kusia kitaluni hadi kuwa tayari kupandikizwa. Mavuno huanza miezi miwili baada ya kupandikiza. Likipatiwa matunzo ni zao lenye ukarimu na kamwe halina maringo wala nyodo kama TOMATO na Hoho.

Tunashukuru Kwa taarifa mkuu ubarikiwe.
 
Nami nilikwenda Ruaha kwa nia ya kulima kitunguu lakini mwenyeji wangu akanipa wazo la kuanza na nyanyachungu. MUNGU akijalia kuanzia wiki ya mwisho ya January nitaanza kuokota moja moja. Nitawajuza.

Tafadhali toa Mrejesho itasaidia kutupa moyo wengine.
 
Ukitaka livume ghafla, basi tangaza kwamba linatibu kitu fulani ambacho kinasumbua sana jamii kwa sasa!
Malila kaka yangu kwani haujui kama nyanya chungu ni dawa na inasaidia sana kwenye mmeng'enyo wa chakula?au mpaka itangazwe inatibu?
 
Malila kaka yangu kwani haujui kama nyanya chungu ni dawa na inasaidia sana kwenye mmeng'enyo wa chakula?au mpaka itangazwe inatibu....?.

Mpaka itangazwe ndio tuta-ipromoti kibiashara. Zamani ukionekana unakula ubuyu watu walicheka sana, lakini ilipotangazwa kuwa inapunguza makali ya mibuyu ilipata shida ya kupopolewa hata kabla ya muda wa kuvuna. Miaka michache alovera ilikuwa majani pori yasiyo na maana kabisa, eti siku hizi watu wanatengeneza hadi juisi!

Nyanya chungu hazijapata mbunifu azitoe kichochoroni ziliko.
 
Mpaka itangazwe ndio tuta-ipromoti kibiashara. Zamani ukionekana unakula ubuyu watu walicheka sana, lakini ilipotangazwa kuwa inapunguza makali ya ibuyu ilipata shida ya kupopolewa hata kabla ya muda wa kuvuna. Miaka michache alovera ilikuwa majani pori yasiyo na maana kabisa, eti siku hizi watu wanatengeneza hadi juisi!

Nyanya chungu hazijapata mbunifu azitoe kichochoroni ziliko.
Hiyo ni kweli kabisa kaka yangu.unaonaje Kama tukianza kuipigia chapuo ngogwe ili ipae.ni zap Zurich sans. Nikitulia kwenye sungura a njiwa nitaingia kwenye nyanya chungu kwani hazideki kabisa.
 
Back
Top Bottom