Kilimo cha Bamia: Fahamu kuhusu mbegu bora, mazingira sahihi ya kulima, magonjwa na namna ya kuyakabili

hili.zao lina pesa we acha tu nililima kwa majaribio kila baada ya siku mbili navuna kisado na nauza 4000
nipo kiluvya. DSM

1467457277585.jpg
 
hii kitu ina pesa we acha tu
njoo soko la tandale au mabibo kiroba huwa kinafika hadi 80,000

1467459619433.jpg
 
Ndugu usiamini kila kitu unachosikia kwa watu, fanya utafiti wa kitu unachotaka kukifanya huu ndio uwe msingi mkuu na muongozo wako katika maisha ya kilimo.

Mimi naishi kwenye kilimo but bado najifunza kilimo pia, msingi mkubwa wa baada ya kutafiti bei ya soko husika nilazima utafiti na nyakati kwakuwa ni jambo muhimu sana hilo kwa kuwa wakati huamua bei pia .

Pia lazima uangalie gharama za kilimo, shamba la kwako au kukodi, ghalama za kupata maji ninamaana hayo maji unayapata vipi toka kwenye chanzo cha maji mpaka shambani. Umezungumzia pump nivizuri hivyo inaonyesha kuendesha pump utatumia mafuta au umeme.

Kitu cha muhimu au AU SIO CHA MUHIMU umbali kutoka shambani mpaka sokoni, nimeandika. Muhimu sio muhimu tena kwa herufi kubwa kwa kuwa unaweza kuangalia mwenyewe kama utauzia hapo shambani au utapeleka sokoni mwenywe.
 
ALF,
Aksante sana Mkuu kwa ushauri wako, naamini nimejifunza kitu kupitia wewe.
 
hii kitu ina pesa we acha tu
njoo soko la tandale au mabibo kiroba huwa kinafika hadi 80,000
Mkuu nitafika hapo muda ukifika,acha kwanza nipambane shambani...kwa kweli umeniongezea nguvu ya ziada,aksante sana.
 
Nilifanya kilimo cha bamia, halikawii kupoteza nuru baada ya kuchumwa kutoka shambani, hakikisha unakuwa na wateja especially gengeni watakao chukua jumla kila unapochuma fresh na uwe na usafiri.
 
Mungu akubariki,aksante kwa elimu mkuu bila shaka umenipa faida kubwa.
 
Nikweli alichosema Sky huwezi kuchuma bamia alafu ndio uanze kutafuta soko, bamia nimoja ya zao linahitaji nidhamu ya muda ya hali ya juu, lazima kuwa na soko ili kuweza kulichuma kwa wakati, Msingi mkuu ni kuchuma unapokuwa na mteja ili usiliuze likiwa limeanza kunyauka, na usipo kwenda na muda kinyume chake ukichelewa litakomaa shambani.
 
Nikweli alichosema Sky huwezi kuchuma bamia alafu ndio uanze kutafuta soko, bamia nimoja ya zao linahitaji nidhamu ya muda ya hali ya juu, lazima kuwa na soko ili kuweza kulichuma kwa wakati, Msingi mkuu ni kuchuma unapokuwa na mteja ili usiliuze likiwa limeanza kunyauka, na usipo kwenda na muda kinyume chake ukichelewa litakomaa shambani.
Na ukiliacha kidogo shambani linakomaa, kama unavyosema nidhamu inabidi iwe ya hali ya juu, kuvuna ni kila baada ya siku 2/3.
 
Nilifanya kilimo cha bamia, halikawii kupoteza nuru baada ya kuchumwa kutoka shambani, hakikisha unakuwa na wateja especially gengeni watakao chukua jumla kila unapochuma fresh na uwe na usafiri.
Aksante Sana Kwa Ushauri Nitazingatia Hilo
 
Msimu wa kulima bamia ni upi? Je naweza kulima Kibaha kwenye eneo la hela 3.5 kwa maji ya mvua?
 
Msimu wa kulima bamia ni UPI? He naweza kulima Kibaha kwenye eneo LA hela 3.5 kwa maji ya mvua?
nimekumiss sana.
Kibaha unaweza kulimia ila hizi mvua zinasumbua sana,
angalau kuwe na chanzo cha maji mvua zikipotea umwagilie.
 
Mkuu umeelezea kwa uzoefu sana unaonekana unalima sana.
Mashine ya kupulizia dawa (solo) linauzwa 35000/= lenye ujazo wa lita 16. Kwanini usinge nunua ili kupunguza cost nyingine? Mimi nalima kipindi cha kiangazi na wala sio masika, pia ukizungumzia kuhusu nyanya bado ukungu na utitiri mwekundu hushambulia.

Na kulima nyanya ni gharama kuliko bamia. Heri utoke kwenye nyanya uhamie bamia kuliko kinyume chake maana nyanya zinahitaji uangalizi zaidi maradufu kuliko bamia. Pia inategemea kipimo cha mche hadi mche ni cm ngapi na mstari hadi mstari ni cm ngapi hivyo kufanya idadi ya miche uwe nayo mingapi katika eneo.

Je, ni mbolea gani ulitumia ili kufanya mmea upate mizizi mingi na matawi mengi? Je mauwa yalipokuwa yakitoka ulikuwa ukipulizia dawa gani ili kufanya mauwa yawepo kwa wingi? Vipi kuhusu soko je uliuzia shambani au sokoni? Mwezi wa nne na watano mwaka huu 2016 bei ilikuwa 160000/= kwa kila kiroba cha kilo 50 soko la ilala.

Mwezi wa sita na saba hadi kufikia tarehe 25/07/2016 ilala bei ilikuwa ni 100000 kwa kila kiroba cha kilo 50 soko la ilala. Kwa sasa ni 500000 yaani mwezi huu wa nane.
 
Back
Top Bottom