Msaada:Kila nikishiba napenda Sana kupigana

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,466
20,212
Watu wa saikolojia njooni hapa,watu wa lishe,watu wa tiba na watu wa ndondi vilevile.
Mimi nina tatizo na waswahili kama kawaida yao hawakosi misemo,wanasema 'mficha gegedo hatii mimba'
Inshu yenyewe ni kila wakati baada ya msosi huwa napenda kupigana sana na mara nyingi ukubwa wa ugomvi hutegemeana na aina ya chakula, mfano chakula nikipendacho cha wali maharage ugomvi wake huwa mkubwa sana.
Juzi nilikuwa cafe flani baada ya msosi mhudumu akaniuliza nimekionaje chakula,nilirusha ngumi kumbe jamaa alikuwa yuko njema,ukweli nilichezea kichapo.Wife nimeshamzingua mara kibao mpaka sasa hivi kaamua kunipunguzia share ya msosi(hamna pepa two tena)
Hii hali inaweza kuwa inasababishwa na nini?
Angalizo : Weka utani pembeni ,hapa naongelea hatari ya hata kufungwa.
 
huo ugonjwa wako hauna dawa
labda kwa kukusaidia ukishashiba kuepuka kichapo
mtafute bodyguard born town anaitwa lemutuz
 
matatizo ni pale utakapo pata reaction ya chakula na tumbo la kuharisha kuja ghafla, sijui utawahi kule ofisi kuu ya nyumba.
 
Kula kdogo
Inaonyesha wew kula lala maana unakula alafu unakaz zakufanya
 
Kwa kitaalamu tatizo hilo huanzia kwenye mshipa wa puru hivyo baada ya kula tafuta mtu akukune (1:4)
 
Hali hiyo inasababishwa na utapiamlo, msosi unaopewa ni wa jana au juzi ndio maana wanakuuliza umekionaje chakula.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom