MSAADA KIJANA MSOMI ANAWADANGANYA WAZAZI WAKE

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,096
9,216
Kuna familia moja hapa ninapoishi wana kijana wao (Ana uchu wa kusoma Elimu ya Juu) wameniomba msaada baada ya kuhisi kijana wao anawadanganya kuhusu masuala ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Nimelezwa kuwa awali kijana wao alipata nafasi ya kusoma Sheria MUCOBIS(FORMER cHUO CHA uSHIRIKA MOSHI) Bahati mbaya alidisko akiwa Mwaka wa Kwanza na akapoteza fursa ya Mkopo na Elimu pia.
Hapo juu nilieleza kuwa huyu kijana yaelekea anauchu wa kusoma elimu ya juu! Baada ya kudisko alipigana kupta nafasi chuo Kingine kusomea BA Education (Naomba nikitaje jina) na akawaaminisha wazee wake kuwa amepata mkopo full!
Cha kushangaza sasa majuzi anawaambia wazazi wake kuwa anahitaji 900,000/= kwa kuwa Bodi ya Mkopo wameongeza mkopo maelezo ambayo hayaingii akilini!
Hoja:Ukweli ni kwamba wazazi wa huyu kijana ni wazee na hali ya uchumi sio nzuri,wamejitahidi kumsomesha kwa mbinde private hadi chuo alipodisko sasa nguvu zimeisha wanaishia kuingia kwenye VICOBA! Wameniomba niwasaidie kujua ukweli wa maelezo kama ni kweli kijana wao ana mkopo kutoka Bodi.
Msaada ninaohitaji: Nimejaribu kuingia kwenye website ya Bodi ya Mikopo sijapata taarifa yoyote,nimeingia pia website ya chuo sijapata ,naomba msaada niwape jibu wazee hawa!
 
1. Hao wazazi wamekula hasara mara mbili kama wewe ndo mshauri wao.
2. Unahitaji msaada ila jina la chuo na jina la mwanafunzi unafanya sirI (viroja)
 
Kwa haraka haraka tu...mwanafunzi aliekosa kigezo cha kuendlea katika chuo fulani ataruhusiwa kuomba mkopo pale apatapo nafasi chuo kingine ikiwa tu atalipia asilimia 25 ya deni la mkopo wa mwanzo.
Je!!huyo kijana aliweza kulipa hiyo asilimia kabla ya kupata mkopo tena??.
Naomba nisahishwe ikiwa nimekosea mahala
 
Kifupi huyo kijana mkopo hajapata,

Bodi ya mikopo hawawezi kukupa mkopo mara mbili mfululizo bila kulipa mkopo wa awali,
 
1. Hao wazazi wamekula hasara mara mbili kama wewe ndo mshauri wao.
2. Unahitaji msaada ila jina la chuo na jina la mwanafunzi unafanya sirI (viroja)
Mkuu naogopa kutaja jina la Chuo kwa sababu Elimu ni Biashara,mpaka nipate ushahidi wa haya anayodai kijana ,sisi tulisoma Karne iliyopita Taarifa nyingi hatuna....sas ajina la mwanafunzi linakusaidia nini!??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom