Msaada: Kama watu alifunga ndoa wakiwa dini fulani, wakihama dini hiyo watahitajika kufunga tena ndoa?

GIBRALY

Member
Mar 14, 2017
31
35
"Eti, ikitokea watu wawili wamefunga ndoa ya KIKRISTO pindi wakiwa wakristo, halafu baada ya muda wote wawili wakaamua kuslimu na kuwa waislamu. Je watafunga tena ndoa ya kiislamu?

Darasa huru, huu mjadala nimeukuta mahali katika pitapita zangu ila sijfanikiwa kupata jibu... Kama hujui like tu kisha pita soma maoni ya watu na ww utajifunza kitu.
 
Ndoa hufungwa kiserikali na kubarikiwa kidini. Mtu anapokwenda kanisani "kufunga" ndoa, basi kasisi anakuwa na cheti cha serikali na mamlaka ya kiserikali kufunga hiyo ndoa, lakini anakuwa na mamlaka ya kidini pia "kubariki" hiyo ndoa. Huyo mtu akibadilisha dini ile ndoa inabaki "imefungwa" na cheti cha ndoa kinabakia kuwa kinatumika. Akienda dini nyingine basi ni juu ya hiyo dini kuamua kama inataka "kuibariki" tena.
 
Hapana hawatofunga tena Ndoa Sheria ya kiislam inatambua ndoa za watu hao ndio maana hata Maswahaba ambao kabla hawakuwa Waislam ilibali wameoa walivyoingia kwenye Uislam hawakufungishwa tena Ndoa
 
Inapendeza sana, Inavyoonekana kwenye Uislam hilo jambo halina shaka., Je, ikiwa Walikuwa Waislam wakaingia kwenye Ukristo hali ipoje??
 
Ndoa hufungwa kiserikali na kubarikiwa kidini. Mtu anapokwenda kanisani "kufunga" ndoa, basi kasisi anakuwa na cheti cha serikali na mamlaka ya kiserikali kufunga hiyo ndoa, lakini anakuwa na mamlaka ya kidini pia "kubariki" hiyo ndoa. Huyo mtu akibadilisha dini ile ndoa inabaki "imefungwa" na cheti cha ndoa kinabakia kuwa kinatumika. Akienda dini nyingine basi ni juu ya hiyo dini kuamua kama inataka "kuibariki" tena.
Ndugu yangu unapoizungumzia ndoa unazungumzia jambo la kutekeleza amri ya mungu,hakuna ndoa ya serikali.
Huwezi kukurupuka ukasema ndoa dini inapewa baraka na serikali!!!!huna dini wewe.ndoa hufungwa kidini ktk kutimiza agizo la mungu na kuacha katazo lake la zinaa.hivyo veti vimekuja miaka kadhaa baada ya Uhuru na ndoa zilikuwepo before.tunapewa vyeti kuthibitisha ndoa baada ya changamoto kuzidi kwny ndoa ikiwemo ya wanandoa kukanana.
Wanandoa wasio waislam wanaposilimu na kuwa waislam ndoa yao wataifunga upya sababu ndoa hiyo ya awali ilikua nje ya uislam.
Nje ya uislamu ndoa hiyo ni batili sababu kuna nguzo za ndoa ya kiislam lzm zifuatwe na nje ya uislam wana njia zao pia.
Kinachorudiwa upya ni ndoa si harusi.
 
***Kama wameingia Kwenye uislam na kuwa waislam jina basi cheti cha serikali kitawafaa zaidi

***Lakini Kama wameingia Kwenye uislam na kutaka kuwa waumini bora wakislam na kutaka kufata nguzo tano za kiislam

1) Shahada ya Imani

Ushahidi wa Imani ni kusema kwa kusadikisha, “La ilaaha illAllaah, Muhammadur Rasulullah.” “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (Allaah), na kwamba Muhammad ni Mjumbe (Mtume) wa Mwenyezi Mungu.”

2) Swalah (kuswali Swala tano)
Waislamu huswali Swalah tano kila siku. Kila Swalah huchukuwa muda mfupi wa dakika chache tu.

3) Kutoa Zakaah (Kuwakunjulia Wenye Dhiki):

4) Kufunga katika Mwezi wa Ramadhaan Kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani.

5) Kuhiji Makkah.

Itawapasa wafunge ndoa upya ya kiislam Ili wapate kuzitimiza hizi nguzo tano za kiislam
 
Kinachohalalisha ndoa Ni cheti.
Cheti Ni Cha Serikali.
Iwe Ni Muislamu au mkristo Cheti Ni kile kile.
Mkuu hicho Cheti kinahalalisha ndoa kwa mujibu wa nani? Kama Cheti ndo kinahalalisha Ndoa, Kanisani kinachofanyika ni nn?
 
Ndugu yangu unapoizungumzia ndoa unazungumzia jambo la kutekeleza amri ya mungu,hakuna ndoa ya serikali.
Huwezi kukurupuka ukasema ndoa dini inapewa baraka na serikali!!!!huna dini wewe.ndoa hufungwa kidini ktk kutimiza agizo la mungu na kuacha katazo lake la zinaa.hivyo veti vimekuja miaka kadhaa baada ya Uhuru na ndoa zilikuwepo before.tunapewa vyeti kuthibitisha ndoa baada ya changamoto kuzidi kwny ndoa ikiwemo ya wanandoa kukanana.
Wanandoa wasio waislam wanaposilimu na kuwa waislam ndoa yao wataifunga upya sababu ndoa hiyo ya awali ilikua nje ya uislam.
Nje ya uislamu ndoa hiyo ni batili sababu kuna nguzo za ndoa ya kiislam lzm zifuatwe na nje ya uislam wana njia zao pia.
Kinachorudiwa upya ni ndoa si harusi.
Acha uongo wewe,kama hujui kitu ni bora ukae kimya kuliko kupotosha..kama wanandoa wakisilimu ndoa inabaki vilevile wala haiguswi hata kidogo mzee..
 
Ndugu yangu unapoizungumzia ndoa unazungumzia jambo la kutekeleza amri ya mungu,hakuna ndoa ya serikali.
Huwezi kukurupuka ukasema ndoa dini inapewa baraka na serikali!!!!huna dini wewe.ndoa hufungwa kidini ktk kutimiza agizo la mungu na kuacha katazo lake la zinaa.hivyo veti vimekuja miaka kadhaa baada ya Uhuru na ndoa zilikuwepo before.tunapewa vyeti kuthibitisha ndoa baada ya changamoto kuzidi kwny ndoa ikiwemo ya wanandoa kukanana.
Wanandoa wasio waislam wanaposilimu na kuwa waislam ndoa yao wataifunga upya sababu ndoa hiyo ya awali ilikua nje ya uislam.
Nje ya uislamu ndoa hiyo ni batili sababu kuna nguzo za ndoa ya kiislam lzm zifuatwe na nje ya uislam wana njia zao pia.
Kinachorudiwa upya ni ndoa si harusi.
nakua napata hasira sana kama mtu akiliongelea jambo la dini yangu kwa kutokujua au kupotosha..ushawahi skia wanandoa wamesilimu wakafunga tena ndoa?kwa taarifa yako ndoa inatambulika hata kama mlifunga ndoa ya kimila lakini mkisilimu ndoa ile ile
 
Hadi hii page inajaa naona hakuna jibu moja kila mtu ana mtizamo wake.

Ndoa ni ndoa tu. Dini hizi zimeletwa na kabla ya hizi dini tulikuwa na ndoa na jamii ilikuwa swafiii na salama salimini.

Tusijiwekee vigezo uchwara kwa fikira zetu za kutengeneza mwisho wa siku maisha yakawa magumu.
 
Hii debate haijapata mjuvi wa kisheria akatufungua.
Maana kumekuwa na makundi mawili bishani! Pia mjadala umeegemea kubadili na kuingia uislam, hakuna popote mjuvi amedadavua kuhusu muislam kwenda ukristu hasa ukatoliki.
Wanajamvi tupate mjuzi hasa wa sheria za ndoa atuondolee kitendawili fikirishi hiki.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom