Msaada juu ya ufafanuzi wa sheria ya ardhi

Pseudomonas

Member
Dec 9, 2011
45
126
Salam wakuu,
Juzi kuna mdau alianzisha uzi juu ya watu wenye kuhitaji ufafanuzi na usaidizi katika sheria ya ardhi sasa naona mods wamefuta/wamehamisha na siuoni tena ule uzi na niliuliza swali la msingi lenye kuhitaji ufafanuzi na kuna mdau alinijibu wakati nafungua uzi nikaambiwa invalid topic kwa hiyo ukiona swali limejirudia usichoke kutoa ufafanuzi tena.
Tatizo lenyewe ni kuna taasisi moja ya kidini ilimilikishwa eneo la ardhi zaidi ya hekari 300 ambapo maeneo hayo yalikua ni mashamba ya wananchi kwa shughuli za kilimo sasa kwa kuwa yalikua ni maeneo ya urithi wengi walipewa tu kifamilia bila nyaraka zozote na waliendelea na shughuli zao bila shida. Baada ya muda baadhi yao walitaka kuyaendeleza maeneo yao kwa shughuli za ujenzi hivyo kwenda ofisi za ardhi za wilaya kwa ajili ya kupata utaratibu wa kupimiwa maeneo hayo huko ndio walipokutana na janga. Walitaarifiwa kuwa maeneo hayo tayari kuna taasisi ilishapimiwa tangu mwaka 2007. Sasa maswali yakaja inawezekanaje watu maeneo yao apimiwe mtu mwingine na kumilikishwa bila mwenyekiti wa kitongoji, mtendaji kata au hata wao wamiliki wenyewe kuwa na taarifa? Kwa nini maeneo hayo ilipewa hiyo taasisi bila hata wahusika kuitwa kulipwa fidia?
Sheria ya ardhi kwa kesi kama hii inasemaje? Naomba ufafanuzi wajuvi wa sheria.
 
Ardhi iliyopo katika eneo la kijiji (vijijini) huwa chini ya usimamizi wa serikali ya kijiji kwa mjibu wa sheria namba 5/1999. Pia mtu/taasisi (i.e any legal entity) anaweza kupata Ardhi kwa njia zifuatazo:
- Kununua (purchase)
- Kupewa/kumilikishwa (Gift/Grant)
- Kurithi (inhertance)
- Kufyeka eneo ambalo halina mtu e.g pori (Clearing virgin land) lakin njia hii ni ya kizaman kwa sasa sio rahisi.

Kwamba kutumia Ardhi ya mtu mwingine bila idhini yake ni kosa kisheria linaloitwa UVAMIZI WA ARDHI (TRESPASS TO LAND) ambapo mwenye shamba/Plot ana mamlaka ya kumtoa huyo MVAMIZI kwa njia ya kawaida ama kwa kwenda mahakamani/Baraza.

Hivyo basi mtu wa kudili nae ni yule aliyomo ndan ya shamba lako bila idhini yako (maana ndo anaekuzuia kufanya shughuli zako kwny shamba hilo) halafu yeye ndo atamtaja nani alimruhusu kutumia, km atamtaja mwingine na yeye (ie alietajwa) unamwingiza kama mshitakiwa mwenza (co-defendant).

NOTE;
Kwa mjibu wa swali lako hvyo ndoo sheria ilivyo. Bt km utafikia uamzi wa kwnd kudai haki yako kwny vyombo vya sheria. Nitapost kuhusu procedure ya kwnd huko. Kwa sasa nijibu swali lako pekee.
 
Shukran kwa maelezo yako nimekupata vyema, kuhusu kwenda kudai haki ya hilo eneo ni process ambayo imeanza mwaka jana mwezi wa 9. Sakata hilo lilifika ofisi ya ardhi ya wilaya na wakasema watalishughulikia ambapo waliwaita hao waliopimiwa maeneo hayo (taasisi ya kidini) na mwakilishi wa wananchi wa eneo hilo ambae walimchagua mtendaji wa kata husika, awali taasisi hio ilikana ila baadae documents zikatolewa wakakiri kuwa ni kweli wao ndio wamiliki (hapa kunatatiza). Hilo shauri lilizuka ktk mkutano wa mkuu wa wilaya na wananchi hivyo akamuamuru mkurugenzi alifanyie kazi ila kimya kingi kimetawala kukiwa na tetesi kuwa wanakutana huko ofisini wakubwa wa taasisi na hao afisa ardhi wa wilaya. Mpaka sasa wameshikilia maeneo ya watu huku wananchi wakiwa hawajui la kufanya. Si mkuu wa wilaya wala mkurugenzi wote wako kimya.
Naomba utaratibu/hatua gani za kwenda kutafuta haki kwenye vyombo vya sheria kwa sababu muda wa kusubiri kukiongelea kwenye mabaraza ya ardhi na huko ofisini umetosha toka mwaka jana mpaka mwaka huu hakieleweki.
USHAURI
Jitadhimin kwnz ww km una mamlaka/uwezo kisheria wa kudai shamba hili kulingana na wewe ulilipataje (maana umesema kwa urithi). Je wewe kweli ni mrithi halali (legal heir) Je marehemu kafariki lini?? (i.e imepita miaka 12) je wewe ndo msimamizi wa mirathi??? (Una ushaidi hilo)...........jijadili kwanza ww kwan mahakamani huwa tunaenda tukiwa na mikono misafi (clean hands)

Kama kweli kuna ushahid kuwa Halmashauri ndo waliwapa hao wa dini angalia thamani ya shamba lako km inazidi 3M fuata yafuatayo;

1. Muone mwanasheria alie karb nawe atamwandikia Halmashauri (w) notisi ya siku 30 ya kusudio la kumshtak (i.e kwa mjibu wa sheria Na 7/1982 (Cap 287 R.E 2002). Bila notisi kwa H/W utatwanga maji kwny kinu. (i.e utakutana na P.O)

2. Baada ya muda wa notisi kupita mwanasheria atakwandalia hati ya mdai yko (i.e Land Application) ambayo wewe utakuwa mwombaji (Applicant) ukiwashitaki...(i) bodi ya wadhamini wa hiyo taasisi ya dini (km mjibu maombi namba 1) na (ii) Halmashauri ya (w) ya.... (km mjibu maombi namba 2).

3. Atakwandalia madai yako unayodai pamoja na maelezo kidogo juu ya umiliki wako na chanzo cha mgogoro km sheria ya Ardhi inavyotaka. Vipengele vya maelezo yako na viambatanisho km vipo (i.e annextures).

4. Peleka hati hiyo kwny baraza/mahakama yenye uwezo wa kusikiliza shauri hilo kulingana na thamani ya shamba (>3,000,000 hadi 50,000,000 baraza la Ardhi na nyumba wilaya (i.e DLHT) >50,000,000 mahakama kuu.

5. Km utaenda DLHT (i.e thaman ya shamba is >3M but <50M) hati hiyo utampa karan wa baraza atafanya prcocess za usajili wa shauri, na utalipia ada ya usajili wa shauri kulingana na thamani ya shamba uliyoweka kwny hati (km ni < 10,000,000 utalipa ada sh 40,000 km ni >10,000,000 utalipa ada sh 120,000) hapo utakuwa umesajili kesi yako na wadawa watapewa samansi (summons) kuja barazani. Km utaenda mahakama kuu (thaman >50M) hati utampa msajili wa mahakama masjala ya wilaya atakupa maelekezo yote ni waungwana sana hawa watu!.

Naomba niishie hapo....mwanasheria utakaempata anajua utaratibu wote baada ya shauri kufunguliwa!. Kwa sasa nimejib kwa kuwa hujapata Lawyer..ukipata sitakiwi kisheria kugongana nae!. (Double service)
 
Shukrani sana mkuu kwa maelezo yako nimekupata vyema, kwenye hicho kipengele cha mirathi sio mimi mmiliki wa mirathi ila huyo aliyeachiwa umiliki atakua ashapata pa kuanzia kwa maelezo haya pindi nitakapomfikishia ujumbe huu.
shukrani sana kwa ufafanuzi huu tutakapofika tutaleta mrejesho
Good!...
Cheers!
 
Back
Top Bottom