kilaboy
Senior Member
- Dec 11, 2011
- 150
- 97
Ndugu wanabodi habari za muda huu.
Mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Arusha nina mke na watoto wawili. Kwa sasa nimeajiriwa Kisiwani Zanzibar na mara baada ya kumaliza mkataba wangu natarajia kurudi kwetu Arusha. Lengo la kuandika uzi huu ni kuomba ushauri wa kisheria juu cheti cha kuzliwa.
Ni wiki ya pili sasa tangu mtoto wangu wa pili azaliwe hapa kisiwani Zanzibar na wakati tumetoka hospitali tumepewa tangazo (karatasi inayothibitisha kuzaliwa kwa mtoto) ambalo tunatakiwa kuipeleka ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya kufuatilia cheti za kuzaliwa.
Swali langu kwenu wanabodi
Je kuna matatizo yoyote ya kisheria hapo baadae tukirudi Tanzania bara mtoto wangu akiwa na cheti cha kuzaliwa kutoka Zanzibar?
Je iwapo Muungano utavunjika mtoto wangu atakua Mzanzibari au atafuata uraia wa sisi wazazi wake?
Nawasilisha wanabodi.